Gharama za kutoa gari bandarini

Gharama za kutoa gari bandarini

Masterproud

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2012
Posts
441
Reaction score
118
Wandugu please naomba kwa mwenye ufahamu wa kukokotoa toka TRA calcutator, Agent wa magari ama yeyote aliyepata kuagiza gari aina ya Toyota Raum (2005), c.c. 1490 CIF $3100. ainisaidie kunipa gharama zote za kutoa gari hiyo Bandari ya DSM. Nahitaji kujua estimates hizo ili nijipange wakati mzigo upo njiani pls.
 
Ushuru wake jumla kwa calculator ya TRA ni 2.6mil. ukijumlisha na hiyo $3100 ambayo ni kama 5.1mil utapata jumla ya fedha yote. Sina hakika na gharama za agent ambaye atai clear hapo bandarini. Ila total taxes ni 2.6mil.
 
Asante sn boss kwa msaada. je gharama hii ni bila kujali siku itakayokaa hapo bandarini?
 
Kuhusu agent, nliongea na watu wa Be forwad wanatoa kwa Tsh 250,000
 
Ushuru wake jumla kwa calculator ya TRA ni 2.6mil. ukijumlisha na hiyo $3100 ambayo ni kama 5.1mil utapata jumla ya fedha yote. Sina hakika na gharama za agent ambaye atai clear hapo bandarini. Ila total taxes ni 2.6mil.

Calculator ya TRA inapatikana wapi? Msaada Tafadhali
 
Wandugu please naomba kwa mwenye ufahamu wa kukokotoa toka TRA calcutator, Agent wa magari ama yeyote aliyepata kuagiza gari aina ya Toyota Raum (2005), c.c. 1490 CIF $3100. ainisaidie kunipa gharama zote za kutoa gari hiyo Bandari ya DSM. Nahitaji kujua estimates hizo ili nijipange wakati mzigo upo njiani pls.

sory kwa kudandia ndege kwa mbele! Vp? kuhusu malori kama fuso au canter inakuaje hapo mkuu.
 
Ushuru wake jumla kwa calculator ya TRA ni 2.6mil. ukijumlisha na hiyo $3100 ambayo ni kama 5.1mil utapata jumla ya fedha yote. Sina hakika na gharama za agent ambaye atai clear hapo bandarini. Ila total taxes ni 2.6mil.

Mkuu nashauri kama inawezekana ungetoa mchanganuo mzima wa namna ya kupata jumla ya kodi maana tupo watu wengi tunashindwa namna ya kuitumia calculator ya TRA. Ahsante.
 
Mkuu nashauri kama inawezekana ungetoa mchanganuo mzima wa namna ya kupata jumla ya kodi maana tupo watu wengi tunashindwa namna ya kuitumia calculator ya TRA. Ahsante.
Usihofu mkuu, ukifungua webpage ya TRA, utaona link ya Calculator. Ukibofya hapo utapata EXCEL Window ambayo itakuongoza, utaijaza kwa kuingiza taarifa sahihi za gali lako kama vile unavyojaza fomu ya kawaida tu, baadaye ukibofya ENTER itakuletea mahesabu yako...
 
Kawaida kwenye calculator utaona Customs Value ambayo kwa gari unayoizungumzia ya mwaka 2005 ni USD$ 2,900, na Tax ni 2,614,811. Lakini kwa sababu value unayosema iko juu than value iliyowekwa watatumia greater of the 2 - kwa hiyo wakitumia USD$ 3,100 Tax ni 2,795,196. Gharama ya CFA inaweza kuwa Tshs 200,000 - 250,000.

Exhange Rate inayotumika utaiona kwenye website ya TRA always updated.
 
Kwa ufahamu nilionao kama mtu anahitaji kukokotoa gharama za ushuru kwenye calculator ya TRA pale aagizapo gari kuna mambo kadhaa ya kuzingatia. Pitia specification la gari husika ikiwemo. (KAMA NITAKOSEA NAOMBA KUREKEBISHWA.)

1.car make, (Toyota)
2.car model, (Allion)
3.model code (CBA-NZT240)
4.year of manufacture, (2005)
5.engine capacity (1490cc).
NOTE: Hivi utavipata kwenye car specs.

Baada ya hapo, kama umeshapakua kikokotozi cha TRA, kuna sheet 2, ya kwanza inaitwa "calculator", ya pili ni "price list". Anza kwa kuweka EXCHANGE RATE kwenye calculator sheet (kuna mahali pa kuweka hii rate). Pili, nenda upande wa PRICE LIST, tafuta gari ambalo unataka kuagiza (bofya CTRL+F, ingiza jina la gari kurahisisha utafutaji halafu bonyeza ENTER) kwa kuzingatia hivyo vitu hapo juu na utaona upande wa kulia RETAIL SELLING PRICE.

1. Nakili hiyo bei ya gari (RSP) halafu rudi kwenye sheet ya kwanza (Calculator), na andika hizo tarakimu kwenye Current retail selling price.
2. Depreciation details zipo kwenye calculator upande wa juu kulia, angalia umri wa gari utakalo halafu ingiza asilimia hizo mahala husika.
3. Kwenye freight pale ingiza gharama za kulisafirisha toka huko liliko ila mpaka hapo total taxes itakuwa ishakupa gharama halisi za ushuru wote.

ZINGATIA: Kuingiza taarifa mahala husika hasa kuhusiana na CC za engine na pia umri wa gari. Data za gari la 2500cc ukiweka mahali pa gari za chini ya 1000cc jua utapata gharama zisizo sahihi.

Marekebisho yanaruhusiwa.
 
Back
Top Bottom