Gharama za kusafiri Kigali

Kama upo Arusha nakushauri upitie Nairobi badala ya Bukoba. Ukifika Nai upande Modern Coast moja kwa moja hadi Kigali. Ni mabasi ya kisasa kabisa, utahisi kama umepanda Qater airways!
Ahsante Kwa ushauri mzuri.
 
Chukua basi la Arusha-Kahama.Kuna mabasi kila siku kutoka Kahama-Kigali. Ni mwendo wa masaa 8 na shs 25000 kwa mtu mmoja mmoja one way mabasi ni mengi pale ila nakushauri upande Trinity express ambayo huondoka kahama kila siku asubuhi saa kumi na mbili. Malazi inategemea na chaguo lako kulingana na bajeti yako ile inaanzia Rwf 6000 single bed kwa siku, Guest za bei ya kati ni kuanzia Rwf 20000 kwenda juu. ukiwa na laki za Tanzania utapata kitu kama Rwf 36000. Vyakula bei ni za kawaida sana Rwf 1500-2000 kwa mlo.Safari njema mkuu, Ukirudi uje utupe mrejesho.
Ahsante mkuu.
 
Hujamuuliza kwanini kachagua kupita kule na ukahisi yeye hajui hicho unachomwambia
 
Watu wanatishana sijui ukiwa na pesa ya Tanzania kubadili kwa Rwandan Francs(Rwf) pesa inashuka pesa ni ile ile thamani ni ile ile mfano una $200 kwa exchange rate ya 2284 = 456,800 Tshs, 1 Rwf ni sawa na 2.64 Tshs hivyo ukichukua hio 456,800 ÷ 2.64 Rwf = unapata 173,030 Rwf na pointi kadhaa wakati huo huo 1 US Dollar ni sawa na 865 Rwf hivyo tukichukua 173,030 Rwf ÷ 865 = $ 200 sema kinachoweza kutofautisha ni exchange rate ya unapokwenda kubadili hela maana zingine zipo juu zingine zipo chini, hivyo jeuri ya $200 itakua ile ile uwe Rwanda au Tanzania ni kitu kile kile nimeandika hivi sababu ninao mpango wa kwenda kushangaa huko kwa huyo dikteta wao Kigali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom