Gharama za kufunga harusi

mozambiqueone

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2014
Posts
241
Reaction score
132
Wadau, sikutaka harusi kwa sasa ila mwanamke analilia hiyo, nimemwambia hali si nzuri anaumia sana.

Sasa,Tshs. milioni 2 inatosha harusi ya namna gani, ndio hela iliyopo.

Wazoefu nipeni hesabu.

Ni Dar es salaam hapahapa.
 
analilia ndoa kwanini?
Hana kwao?
Ana kazi?
Elimu yake ni ipi?
Umri wake?
 
Dah hii kali mil 2? Hata ukumbi haitoshi
 
Ona hii.....fanya watu ni 50 yaani harusi ya kawaida
 
Bia mbili 50 x 2 x 2200, then msosi plate 50 x 7500, then maji chupa 50 x 350 , then usafiri laki 3 ukumbi laki 7 na mapambo laki 3 then nguo zenu na malizia na MC na mziki. Nipe jibu
 
Hiyo inatosha kwa kuwaita ndugu na jamaa wakuchangie, ndugu harusi si peke yako lazima ubebwe na watu kama nawe si mtu wa watu kweli kazi ipo. Muulize naye ametenga fungu gani?


Halafu muulize anataka NDOA ama HARUSI?? Kama harusi huyo hakufai anataka kujionyesha naye kaolewa,kama Ndoa kwa kuweka kumbukumbu hiyo hela mtafutie shela nawe tafuta suti yako nendeni na wasimamizi mkafunge Ndoa kanisani,siku mkija barikiwa mtafanya jubilee yenu mtakula na ndugu na jamaa mpka msaze.
 
NDUGU INATEGEMEANA NA NETWORK YA WATU ULIO NAYO WEWE NA FAMILIA YAKO.

Harusi nyingi nimeona sisi raia ndio tumezifanya kwa michango yetu... Bwana harusi anajinunulia mavazi, pete etc na vitu vya bibi harusi pia... then anatoa laki kadhaa au milioni kwenye kamati ya kuzugia then wanakamati ndio wanaibeba shughuli... So far ni Harusi moja tu naifahamu ambayo tulialikwa tu na mwenye sherehe bila kumchangisha mtu chochote.... michango yetu tukanunulia tu zawadi.

So far so good ndio uhalisia unaojitokeza kwenye jamii nyingi hapa sasa hivi
Wadau, sikutaka harusi kwa sasa ila mwanamke analilia hiyo, nimemwambia hali si nzuri anaumia sana. Sasa,Tshs. milioni 2 inatosha harusi ya namna gani, ndio hela iliyopo. Wazoefu nipeni hesabu. Ni Dar es salaam hapahapa.
 
Ndoa za kulazimishana ni mtihani

aafu cha ajabu siku hizi wadada yupo tayari ukatoe mahari na ahamie kwako.

akishaingia tuu ndio unaona fujo za ‘baby tufunge ndoa’ na sanaa zingine.
 

Harusi yako na Kasinde Ukumbi na vinywaji juu yangu.........lolest
 
Last edited by a moderator:
Inatosha na chenji inabaki tafuta mpishi wa sahani 60 kwa 5000 ambapo sawa na laki3,tafuta mc wa kitaa mpe laki,soda crate 3 sh 45k bia crate mbili 130k,maji chupa 120 za nusu lita 60k unakodisha costa mbili tena zile za kusanya kanisani to ukumbini then ukumbini to nyumbani kwa 160k(unawaacha wakafanye yao ila warudi ukimaliza) unakodisha gari mbili ndogo saloon kwa 100000 na mafuta ya elfu 60 unatafuta ukumbi mdogo tu wa laki 2 zipo nyingi tu basi hapo unabakiwa na laki 6 nzima ukitaka kucomplexate hiyo mil2 ni ukumbi tu pale delux au mika nitafute PM kwa mchakato mzima wa kila kitu vitu vyote ntasimamia mimi kuanzia usafiri,ukumbi hadi chakula hiyo ni bajeti ya watu 60 tu,mziki ni 100k tu,shooting cameraman ni 100 tu.
 

uko vizuri mwanakamati mzoefu kamati ya vinywaji inakufaa
 
tukianza na usafiri....TSH.5000

IKIZIDI SANA TSH.7500 MSHIKAKI....

3 LOAVES ARE MORE THAN ENOUGH AS CAKE SUBSTITUTE...

maakuli....kijamaa zaidi......

alternatively.....
 

Attachments

  • harusi.jpg
    60.7 KB · Views: 1,598
kaka fanya kile moyo wako unapenda na una-uwezo nacho, kwanini uumie kisa watu wakuone kisha kesho unabaki unalia ooh nimemaliza mtaji wangu wote kwenye harusi... watakucheka haohao waliokuimbia, kula na kunywa bure siku ya harusi yenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…