ALPHA2012
Member
- May 9, 2012
- 12
- 8
Wana JF, nimeandika Kitabu kizuri cha ECONOMICS Paper 1. Kwa kweli ni kizuri kwa kuwa nimeshaanza kukiuza kwa shule chache na kwa baadhi ya wanafunzi. Wanafunzi wote wamekisifia kwamba ni kizuri. Lakini nin shida moja. Sina Mtaji wa kutosha kutoa nakala nyingi ili nikisambaze nchi nzima au hata mikoa kadhaa tu. Kama kuna mtu anayefahamu namna ambavyo nitaweza kuprint nakala za kutosha kwa gharama nafuu, au kama kuna mtu ambaye anaweza kuingia Ubia na mimi ili tuki print na tutalipana baadae kwenye mauzo. Kitabu kinauzika vizuri sokoni. Kina kurasa 270 na kina TOPICS zote 11 zinazopaswa kufundishwa Kidato cha tano kulingana na Syllabus ya mwaka 2009. Kwa sasa nilikuwa ninakiuza kwa sh. 25,0000 (bei ya jumla) na sh. 30,000 bei ya rejareja. Lakini kuna watu wamenishauri nifanye large scale printing ili kupunguza gharama na ndipo nitaweza kukiuza hata kwa sh 15,000. Kwa sasa huwa natoa nakala 100 tu kwa wakati mmoja na gharama za kuprint zinakuwa juu sana. NAOMBA MSAADA WAKUU.