Gharama za kivuko kigambon zapaa

Kuanzia tarehe 1 mwezi januari mwakani nauli ya kuvuka kwenda na kutoka kigamboni itakua shiling mia mbili kwa mtu mmoja,na gari zitatozwa sh elfu mbili!
Walalahoi tujipange kufunga mikanda,
Ongezeko la asilimia mia (100%)
 
DSC00760.JPG

Daraja letu liko mbioni.
Tunajua sana kubuni model ila kuweka structure i-exist?!
 
Kimsingi sipingi ongezeko la bei za kivuko cha hapo kigamboni kwani garama za uendeshaji zipo juu sana kama ukiwa mdadisi mzuri. ila sasa kwa hao wakusanya ushuru nao wawe ethical isiwe wamepandisha bei mapato yakabaki yale yale
 
Kama mmesoma makala ya Mbwambo kwenye Raia mwema wiki hii ametoa tahadhari ya umma kujiandaa na hali ngumu zaidi 2012 kuliko hii ya sasa kwani serikali imekwama haina tena mbinu mbadala za kujiongezea mapato zaidi ya kuwakamua wananchi.
Wakati ukitafakari kuhusu hili la kivuko,tujiandae kuanzia january 2012 gharama za umeme juux3.
 
Jk sijui tukuelewe je kwani kuna vitu havijawahi kupanda zaidi ya miaka 20 iliyopita japo hali ya maisha na kushuka thamani ya hela kushuka kama nauli ya wanafunzi ilikuwa sh. 50 kwa muda mrefu sana ila tangia uingie madarakani imepanda mara 2 kwenda mia na sasa 150 na nahisi mpaka uondoke madarakani 2015 kama waTz wataendelea kuwa wavumilivu yaani wasipokuondoa kwa nguvu ya uma tunategemea itakuwa zaidi ya 300, kivuko kinapanda bei ambayo ilidumu kwa muda mrefu tena inapanda kwakudable, Nishati za mafuta na umeme tunapata kwa mgao, je wanauchumi wako na uchumi uliosomea pale mlimani ndo ulikufundisha kuwa taifa linaendelea pasipokuwa na nishati kama hizi? Yafaa ujiulize na kuchukuwa uamuzi ambao utakuwa na faida kwa taifa na kuwafurahisha wengi kwakujiuzulu kwa manufaa ya taifa mliloliweka rehani mdomoni mwa simba mwenye njaa kali

Eee wakazi wa Dasalama hiyo hali c salama acheni kulalama na kutoa lawama kwani mnalea dhahama vinginevyo bora kuhama! Huku mombasa kuvuka kivuko cha likoni apa bure. Ivi Jk una washauri ww au...? Umeme-juu,nauli zote juu,mafuta juu/hakuna,faini za barbarani-juu,ada za shule na vyuo-juu:nyingi ya hizo ni higher cost of input . Ogopa sana madhara ya cost-push inflation, sikilza ushauri wa kweli!
 
Nahama Mji Mwema wacha nikajibane na wahindi na kina FF katikati ya mji maana kukaa mbali foleni kero kigamboni niliona ujanja sasa inakuwa kero na kuogelea naogopa kuliwa na samaki mimi.

nhc wamepandsha kodi mdau
 
Kimsingi sipingi ongezeko la bei za kivuko cha hapo kigamboni kwani garama za uendeshaji zipo juu sana kama ukiwa mdadisi mzuri. ila sasa kwa hao wakusanya ushuru nao wawe ethical isiwe wamepandisha bei mapato yakabaki yale yale

na kipato cha watz, je kipo chini au JUU?
 
Hivi hili la kivuko nalo limo kwenye jurisdiction ya SUMATRA? Wadau (watumiaji wa kivuko) wamehusishwa kwa kiasi gani katika hili? Maana ni hatari kuachia upande mmoja kujiongezea tu nauli wanavyotaka kwa kisingizio cha kupanga kwa gharama za uendeshaji (hata kama nyingine zinaepukika/zinaweza kupunguzwa!).
 
Wakazi wa kigamboni itabidi tuandamane kupinga hili, haiwezekani nauli ipande bouble, hivi mshahara wa mtu kiasi gani? Gari lenyewe nimekopa ofisini na bado sijamaliza kulipa!!!! Nauli 4000 kwa siku na wengine tufanya kazi mpk jumamosi nikivuka na kagari kangu ka mkopo itanicost 100,000 deni la gari let say 50,000 bado matumizi ya nyumbani, mshahara wenyewe 250,000. Dah kama kuna mtu anataka kununua gari anitafute jamani kwa hali hii siwezi bado mafuta hapo
 
bado dhumuni ifike 300 kama daladala kwa hiyo ndio maana wameanza kidogo kidogo..
maana kuna watu wameanza kubishabisha ngoja tuone..
 
Nimesahau kitu, hapo bado sija include gharama zingine zisizo lasmi, asubuhi kausingizi kamenoga nimechelewa kuamka ili nisifukuzwe kazi namhonga poti 2,000 anipitishe No Entry. Sasa je kupanda kwa nauli watafanya na jitihada za kupunguza foleni au hali itabaki ile ile?
 
Hii inasikitisha badala ya Serikali kutoa huduma sasa inafanya biashara. Nakubaliana na anayesema kuwa ni ujanja wa kuwahamisha wanakigamboni wapisha mji mpya. Wananchi wanalipa kodi mbalimbali na wanalipa kodi kwa kila huduma wanayopata, sasa badala ya serikali yao kuwapa huduma inawakamua zaidi. Mungu tunusuru na serikali hii isiyojali wananchi wake.
 
Mbunge wa Kigamboni upo? Haya ya nauli ya Kivuko kupaa umeyasikia, umechukua hatua gani?
 
Back
Top Bottom