Gharama za harusi kwa bwana harusi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gharama za harusi kwa bwana harusi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by TheChoji, Dec 2, 2011.

 1. TheChoji

  TheChoji JF-Expert Member

  #1
  Dec 2, 2011
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 672
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Kuna thread moja inahusu michango ya harusi imenikumbusha mbali. Hivi jamani, mnazijua gharama anazoingia bwana harusi hadi anapooa? Katika hali ya kawaida kabisa, kama wewe ni mwanaume na unataka kuoa, jiandae kwa mambo haya:

  1. Kujitambulisha ukweni. Hapo utatakiwa uende kijijini alikozaliwa mkeo mtarajiwa ukajitambulishe huko. Kama mfano mkeo anatokea Mwanza, na mnaishi Dar, andaa nauli ya watu wawili, malazi kwa siku mbili, na utagharamia shuhuli hiyo ya utambulisho. We tenga 500,000. Hapo tuna assume mkeo atajitegemea. Otherwise 800,000 itakutoka.
  2. Kumtambulisha mkeo kwenu. Kama nyie nyumbani ni Arusha, utatakiwa umpeleke huko Ngarenanyuki. Sio umlete hapo Tabata mlipopanga. Hapo sio kwenu! Andaa nauli yako na atakaekusindikiza, nauli ya binti na mwenzie, na gharama za vinywaji na chakula siku hiyo. Utahitaji kama 700,000
  3. Kifuatacho ITV ni kuwaalika wakwe zako nyumbani. Uwatoe watu kama nane Mwanza, uwalete Arusha. Wale, walale, wajisaidie, kwa gharama zako. We acha ubishi, tenga 800,000 tu.
  4. Kwani we wazazi wako wanajua unakooa? Sasa je? Wasafirishe kwenda Mwanza! Watu watano. Utahitaji kuwa na 500,000. Beba pia ATM card yako, kuna imejensi.
  5. MAHARI ndio topic inayofuata sasa. Ukiwa mjanja, unganishia kwenye hiyo safari hapo juu uue ndege wawili. Pamoja na hayo, itabidi ubebe 2,000,000.
  6. Sasa kijana unaweza kumvisha mchumba wako pete. Nunua ya kawaida kabisa ya dhahabu. 350,000. Tukio lenyewe la kumvisha pete unaweza ita marafiki wawili watatu ukatumia 200,000. Au fanya sherehe kabisa. Mi simo
  7. Oke, sasa unaweza kuitisha vikao vya harusi. Tengeneza kadi za mwaliko wa kamati kwa 200,000, kikao cha kwanza gharama zote ni juu yako. Andaa 500,000. Swali la kwanza kwenye kikao: “We una shing ngapi?” Sema 1,000,000.
  8. Utahitaji 100,000 ya sms na simu kukumbushia michango. (Shukuru Mungu kuna cheka time)
  9. Wakati vikao vinaendelea, utatuma 200,000 kwa m-pesa ili mambo ya kimila yaendelee kule nyumbani. We unaelewa
  10. “Darling, sasa mi kwenye kitchen party ntavaa nini?” 300,000!
  11. “Darling, kuna mahali nimeona gauni zuri la send…” 400,000!
  12. “Baby, rafiki yangu alinunua gauni la harusi China yani lilimpende…..” 700,000!
  13. Wakati huo wewe mwenyewe hujajua utavaa nini, hujanunua pete za harusi, hujamvalisha best man na mkewe. Tuseme unahitaji kama 1,500,000 maana utalia lia sana. Kumbuka, gharama hizi huchangiwi na kamati. Wala hutarudishiwa.
  14. Siku ya send off lazma uende Mwanza. Utaenda mwenyewe? Ndugu wawili watatu na mshenga 600,000. Kwenye send off utatakiwa kutoa sijui blanketi la bibi, vitenge vya mashangazi, na vikorokoro kibao. Nunua hivyo vitu 300,000 uende navyo ili kupunguza gharama. Beba 200,000 za wale mashangazi watakaoibuka ghafla!
  15. Mshonee baba mkwe suti 100,000 mama mkwe yeye atavaa gauni la 50,000.
  16. Fotokopi hiyo hapo juu (namba 15) kwa wazazi wako. 150,000
  17. Watu watakaopenda kuvaa sare wajitegemee! Mimi sina hela! Ila utavishonea nguo vile vitoto kwa 80,000.
  18. Siku mbili kabla ya harusi, utaanza kupokea wageni. Unatakiwa uwatafutie malazi na chakula. Kwa ujumla utahitaji kama 500,000
  19. Jioni watoe auti mashemeji zako ambao hawajawahi kufika Dar ukawanunulie bia ili wakuone wa maana. 200,000
  20. Siku ya harusi bibi harusi na mwenzie na watoto na ma maids watatakiwa wakapambwe saluni. 200,000
  21. We na mwenzio mtaenda kunyoa hapo kwa nanii. Ndevu na nywele 10,000
  22. Siku ya harusi beba sadaka 10,000. Wakati huo umeshamtuma kijana akakulipie hoteli mtakayofikia baada ya harusi. Kamati haitoi hela hiyo, so utalipa malazi ya siku mbili 200,000
  23. Kama mtaenda honeymoon sehemu yoyote nzuri nzuri nje ya mji, si chini ya 800,000 kwa angalau siku 5.
  24. Wakati uko huko honeymoon, huna hata kumi, mwanakamati mmoja ambae hakuchanga anakupigia simu “ Sasa tunavunja lini kamati?” Pesa yote iliyochangwa ilitumika kwenye harusi, sasa gharama za kuvunja kamati ni za nani?? 500,000!
  25. SASA MNAANZA MAISHA YA UNYUMBA. 14,150,000 poorer.
   
 2. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ndio maana wajanja tunapiga mimba kwanza halafu baadae mengi yanjifuta yenyewe.
  Ukitaka kuitwa mtakatifu dunia hii utaumia sana.

  Ushauri wa bure "MIMBA FIRST"
   
 3. TheChoji

  TheChoji JF-Expert Member

  #3
  Dec 2, 2011
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 672
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  We piga mimba, usipige ukija kufanya harusi lazma nyingi kati ya garama hizo utazipata tu. Labda mahari ndio itapungua kidogo
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Dec 2, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mengi uliyotaja sio ya lazima bali ni mambo ya kutafuta sifa.Kama huna pesa sifa ya nini? Sifa gharamia mwenyewe bwana sio kwa mifuko ya wengine.
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  kuna waumini wa dini moja,yote hayo ni optional....
  mnaweza waambia watu kuwa kesho mnafunga ndoa
  likapikwa pilau ,jungu moja kuubwa,shehe akaitwa kutia ubani...
  gharama hata laki mbili haifiki....huyo unachukua mke......lol......
   
 6. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #6
  Dec 2, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Tobaaaa.....Yeleuwiiii kama hali ndio hii nimeamua kuwa MSEJA sioi tena ng'ooooooo
   
 7. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #7
  Dec 2, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ....hahaha, e bana ee? aheri yetu tuliojiolea enzi zileeeeeeeeee..... sasa tunasubiri wajukuu tu!
  Kwani ni lazima kujfaharisha ee? Poleni.
   
 8. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #8
  Dec 2, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mengine ni ya kujitakia,.kutafuta sifa zisizokuwa na maana... Sio lazima kwa dini yoyote...mnaeza enda kanisani kimya kimya na kufunga ndoa bila mbwembwe zote hizo.
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Dec 2, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Na siku zote mwanamke ukisha mpiga mimba thamani yake ukweni inashuka drastically hivyo unajibebea kama unalia.
   
 10. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #10
  Dec 2, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ....lol....

  umenikumbusha, kuna zile za kuoa alfajr alfajr baada ya "salaa...!" - kahawa, chai na maandazi
  kwa muozeshaji na mashahidi na waliopo nyumbani inatosha, si sadaka tu bana?
  haina majotroo...
   
 11. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #11
  Dec 2, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Na hizo sifa zitakufikisha pabaya
   
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  Dec 2, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mseja na kapera ni neno moja au????
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Dec 2, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hii ya kimya kimya ndo nitakayo fanya mimi kikubwa ni cheti cha ndoa.
  Sasa gharama za posa nauli ukweni n.k nikifikiria hivyo nasikia uchungu bora niendelee kunywa bia.
   
 14. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #14
  Dec 2, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Swahiba mimi nimeamua kuwa MSEJA banaa....swahiba niende huko ukweni kwenu waje waanze sijui khanga ya dada, blanketi la bibi, shuka la mmoja, mto wa shangazi, sijui nilete sharubu za babu, mbuzi mwekundu sijui wa wajomba mimi nitatoa wapi hayo jamani.....
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Dec 2, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Piga mimba unabeba AD kilainiiiiiiiiii kwanza wanamsusa anahamia kwako kisha ww unamtuma Asprin akaonekane ukweni anaenda na Tsh.15000/= tu biashara imekwisha ndoa mtafunga uzeeni
   
 16. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #16
  Dec 2, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  No MSEJA mara nyingi inatumika kwa MAPADRI.....KAPERA nafikiri ni yule ambaye hajaoa bado
   
 17. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #17
  Dec 2, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mimi naipenda ya usiku baada ya sala....
  watu wameshashiba makwao,we unawapa chai tu biskuti,unachukua mke lol
   
 18. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #18
  Dec 2, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Usiogope swahiba we tangaza nia mie ntajitolea ubani, lizzy mkeka, the boss mchele kg10, klorokwini nyama kg3, uporoto matango na nyanya, asprin ataleta maji kwenye madumu...king'asti atamfunda mwali na kumchora hina, bht atamwazima mwali dera, gaijin atatuletea radio na cd zote za taarab.... Ndoa tayari...kaizer atawapeleka nyumbani na kimkweche chake.
   
 19. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #19
  Dec 2, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mpwa unauliza majibu wakati tayari huu ni mwezi wa nne sasa subiri katoto ka ukweli...
   
 20. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #20
  Dec 2, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  watakusema mtaani wanakudavid
   
Loading...