Gharama za AIRTEL ni hatari

Gharama za AIRTEL ni hatari

Kimla

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2008
Posts
3,953
Reaction score
6,996
Wanabodi, Airtel, wamenila sh 45,000 ndani ya dk 10.Je hii ni haki kweli?? Nimewapigia simu custor services sijapata majibu ya maana. Ninahisi kuwa watu wanaiba kupitia mifumo wa IT au elimu ya IT waliyonayo. Mwenye experience na tukio kama hili aniambie alifanyaje?
 
ulifanya nini ndani ya hizo dakika kumi?maybe its justified
 
Piga namba hii 0784105400 utapata majibu muafaka ni ya Corporate Customer Care Service
 
Airtel ni wezi, ila Tigo wamezidi, siipendi Voda lakini sasa sina jinsi itabidi nijiunge tu na Rostam!
 
Hizo dk 10 ulipiga nchi gani? yote kwa yote tunaibiwa sana na makampuni haya ya simu
 
Mkuu ulipiga simu au ulitumia internet cause haieleweki ndani ya dk 10 ulifanya nn!
Hata kama unapiga int. Call haifiki kiwango hicho na hata kama unatumia skyper internet huwezi kuliwa 45 ndan ya dk 10, ebu angalia usije ukawa uliingiziwa 4,500 kwa makosa ww ukadhani ni 45,000
 
Mkuu, waombe wakupatie bill print uweze kuona matumizi ya hiyo 45k. Halafu jiridhishe kwamba hiyo simu unaitumia wewe peke yako. Yawezekana pia mtu wa karibu yako (spause/family member/close friend) ameitumia bila wewe kujua? Labda huna full control na simu yako?
 
Wanabodi, Airtel, wamenila sh 45,000 ndani ya dk 10.Je hii ni haki kweli?? Nimewapigia simu custor services sijapata majibu ya maana. Ninahisi kuwa watu wanaiba kupitia mifumo wa IT au elimu ya IT waliyonayo. Mwenye experience na tukio kama hili aniambie alifanyaje?
maneno hayajitoshelezi
 
Tunapiga kelele kila siku kuhusu mitandao ya simu nchini. Hatuna pa kukimbilia, tunabaki kimya na kukubali matokeo.
 
duh utakuwa umerusha tu,au kuna mtu alitumia simu yako,kiwango hicho Airtel hawana
 
hapa lengo ni kuonyesha uliweka salio la 50,000 hakuna jingine hapa
 
Back
Top Bottom