Gharama ya Usafiri Ubungo kwenda Changanyikeni yapaa

spyboss

Member
Nov 30, 2015
45
69
Habari za mchana. Gharama ya Usafiri kwa wakaazi wa Changanyikeni kupitia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) imenda kutoka Tsh 500/- na kuwa Tsh 1000/- kwa usafiri wa kutumia bajaji bado sijapata bei ya pikipiki. Ikumbukwe pia kwamba hakuna daladala zinazotoa huduma kwenda changanyikeni hivyo usafiri pekee kwa wakazi hawa ni boda boda na Bajaji

Nawasilisha
 
bajaji sio usafiri wa umma, hata wakichaji buku mbili ni poa tu
Watu hulalama bila kujua anacholalamikia ni nini inawezekana analalama tatizo yeye. Jibu sahihi kabisa umempatia.

Alitakiwa alalamike kuhusu kukosekana kwa usafir wa daladala katika eneo hilo aombe Sumatra waanzishe hiyo ruti
 
Bajaj ni usafiri wa umma mzee,
Ndio maana leo hii ukinunua bajaj kwenye usajili kama ni ya biashara lazma upate kibali kutoka sumatra,na kinaeleza ni kwa ajili ya ruti ipi
Hapo sasa, kuna commuter (public) na taxi au teksi, hire au private hire.

Kwahiyo bajaji hazijasajiliwa kwa kazi ya commuter bali na hire kwa hiyo wanaweza panga bei kulingana na gharama za uendeshaji hautaki unachapa mwendo kwa mguu
 
Watu hulalama bila kujua anacholalamikia ni nini inawezekana analalama tatizo yeye. Jibu sahihi kabisa umempatia.

Alitakiwa alalamike kuhusu kukosekana kwa usafir wa daladala katika eneo hilo aombe Sumatra waanzishe hiyo ruti
Kipindi cha nyuma kulikuwa na hiyo ruti, sijui kilitokea nini ikasitishwa. Ni sawa na ruti ya Kawe Posta au Masaki Posta, hazipo tena
 
bajaji sio usafiri wa umma, hata wakichaji buku mbili ni poa tu
Bajaj ni usafiri wa umma mzee,
Ndio maana leo hii ukinunua bajaj kwenye usajili kama ni ya biashara lazma upate kibali kutoka sumatra,na kinaeleza ni kwa ajili ya ruti ipi

Mtu hajui lakini mbaya zaidi pia hajui kuwa HAJUI lakini yumo tu,

Kwakujiamini kabisa;
"Et,i Bajaji sio usafiri wa umma"

Sinahakika iwapo tatizo ni Lugha au kuna changamoto nyingine zaidi.

Mkuu #Prince Jr umemjibu vizuri sana.
 
Back
Top Bottom