Gharama ya miwani ya kusomea

asante mkuu
Liko shirika moja pale Kisutu sokoni, ukienda na cheti cha macho unapewa miwani ya bure kabisa.
Hata kama utaandikiwa ya kusomea na ya kutembelea unapata zote mbili bure.
Ukiulizia pale Kisutu watakuonesha ofisi zao zilipo, tatizo huwa wanahamahama ofisi lakini wapo maeneo hayo hayo.
Jaribu kwenda kuulizia, mimi nilishapeza miwani za kitembelea mara mbili bure kabisa.
Uwahi tu asubuhi na unajiandikisha, saa tatu ofisi inafungulia na kuanza kugawa miwani hizo. Kwa siku moja wanatoa miwani mia mbili hadi tatu kulingana na watu walioenda.
Hao jamaa wana miwani myingi mno.

Nenda kaulizie sasa.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…