Mkuu nimejaribu kufuatilia miradi mingi ya NHC lakini kwa kweli huwezi kuona ni jinsi gani mwananchi wa kawaida anaweza kumudu kununua nyumba hizi. Labda tuambiwe malengo ya kuanzishwa kwa shirika hili yamebadilika? Maana hata ukiangalia hizo low-costing houses zao bei bado ziko juu sana. Je beneficiaries wa NHC wamebadilika?
Kwa mara nyingine tena Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
leo 24 Oktoba, 2012 limezindua rasmi mauzo ya nyumba katika mradi wake mpya wa Mindu, jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huu ulianza rasmi mwezi Novemba mwaka 2011, na unatarajiwa kukamilika rasmi Aprili 2013 na mteja kuweza kukabidhiwa nyumba yake
mwezi Mei 2013,
Kila nyumba itauzwa kwa bei ya TZS
272,050,673.08 bila kodi ya ongezeko la thamani (VAT ) na TZS
321,019,794.24 ikiwa na kodi ya ongezeko la thamani (VAT).
Wanabodi
kama kuna mtu au watu wanafanya uhuni ni huyu mkurungernzi wa NHC na watu wake.
1. Anaweka VaT makusudi ili tuone kwamba ni VAT, ila hiyo ni % hivyo ukiweke bei juu lazima itapanda, na bei ikiwa chini itapungua.
2. Anachukua mkopo kwa wanunuzi, bila kuwapa lipa, ona anauza Oktoba na kisha anakupa nyumba May 2013, maana yake anakaa na asilimia 80 yako kwa miezi zaidi ya minane ( kama itakamilika on time vinginevo kwa mwaka) fikiria kama mtabidi watu 60 @ akalipa 80% ya 272 m, mtakuwa mtoa mkopo wa Tsh 217.7 x 60= 13,062/m (billion 13) hazina liba kwa nusu mwaka, huu ni mkopo free100%
3. Unapo kuwa na NHC, kwa ukubwa wa mradi tunategemea gharama za ujenzi zipungue, ila NHC zinaongezeka.
4. Wastani wa mshahara Tanzania, ukiondoa (biases inaopatikana kwenye mabenki na contract za international organization) unakadiriwa ni Tsh1,500,000pm.
Mchanganuo wa jumla, kwa urahisi sana, 321, 019,700 / miezi 360= (sawa na miaka30) makato ya mwezi 891,721.50. kumbuka wastani wa mshahra kisha toa statury deduction kodi 30% na kisha ILO (sheria ya kazi) wanataka ubaki na 1/3 ya mshahara. Hivyo basi 1,500,000- 450,000(tax) - 500,000 (1/3 Labor law) baki 650,000/ kumbuka rejesho ni 900,000 ambayo ni principal amount bila riba, legal fee, loan fee, n.k
Ndugu hizo ni hesabu za harakaharaka tu, kwenye keyboard. Swali watu wangapi wana mshahara huo au juu ya huo? je watu hao walio bakiziwa 500,000 kwa mwezi wataenda kazini, watakula, watavaa, watalipa umeme na maji, matibabu na ada za watoto, kisha wajiwekee hakiba kwa tahadhari?
Mwisho, Mkurugenzi anatumia ujana na ujanja tu, kufanya maisha ya watanzania kuwa magumu, nashangaa hata wanaompa mkopo huo, kabla hata nyumba hazijaisha, na ndo wanamfanya aone mahitaji makubwa na watu wanahela, kumbe wanaweza kuwa wasomali, wahabeshi, waarabu, wahindi wararushwa, wazee wa mujuni,n.k
lpo siku tutajua ukweli NHC ipo kwa faid ya nani.
Wakatabahu