Gharama ya kubadili ownership Gari

Kremme

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
471
495
Habari za asubuh wakuu,
Naomba nijue taratibu na gharama za kubadili ownership ya gari TRA.
je pia gharama inategemea pesa mliyouziana?
natanguliza shukurani za pekee; Gari ina cc 1980 na kwa matumizi binafsi.
150251_large.jpg
 
Nenda na mkataba wa mauziano,card original na document zote halali za gari. Watakuchaji 1 au 3% (nimesahau)ya bei mliouziana.

Wajanja huwa wanaandika mikataba miwili kupunguza gharama.

Kama gari haijalipiwa ushuru utapigiwa hesabu ulipe.
 
Nenda ofisi za TRA zilizo karibu yako ukiwa na mkataba wa mauziano watakupa gharama au ingia website ya TRA
 
Nenda na mkataba wa mauziano,card original na document zote halali za gari. Watakuchaji 1 au 3% (nimesahau)ya bei mliouziana.

Wajanja huwa wanaandika mikataba miwili kupunguza gharama.
Nilikuwa nasubiri poa kufahamu
 
Utalipa transfer fee ya 1% ya gharama ya kununua gari( mkataba wa mauziano utaonesha), plus stamp duty Tshs.10,000 na kuna shs. 60,000 nyingine (sikumbuki inaitwaje) so simply Tshs.70,000 plus 1% ya gharama ya kununua gari.
 
Wao watakuwa na uhakika vipi juu ya gharama halisi eg mfano mmeuziana tu kishkaji na mkamtafuta lawyer aka set mambo? Nauliza tu
 
Wao watakuwa na uhakika vipi juu ya gharama halisi eg mfano mmeuziana tu kishkaji na mkamtafuta lawyer aka set mambo? Nauliza tu
Mara nyingi wanatumia kilichoandikwa kwenye mkataba. Ila kama hakina uhalisia Afisa wa TRA anaweza kukadiria thamani upya.
 
Utalipa transfer fee ya 1% ya gharama ya kununua gari( mkataba wa mauziano utaonesha), plus stamp duty Tshs.10,000 na kuna shs. 60,000 nyingine (sikumbuki inaitwaje) so simply Tshs.70,000 plus 1% ya gharama ya kununua gari.
gharama uhakika ni Tshs, 60000 (hapo 50000 kwa ajili ya kubadilisha umiliki, 10000 kwa ajili ya kuprint card mpya) na 1% ya bei ya mauziano. ninavyojua kama bei itakuwa inaonekana kwa namna yeyote ile sio halisi bas officer wa TRA atafanya tathmin kwa kuangalia market price(bei ya soko). Kumbuka mauziano yeyote ya kishkaji hayakubaliki. Hivyo kama unataka kupunguza bei inawezekana lakn n kwa kiasi ambacho labda mtu hawezi kunotc(inmaterial). hata hivyo one percent naona n ndogo sana hizo gharama za kuandaa mikataba miwil na wanasheria mara mbili gharama itakuwa ile ile.
Ni mawazo yangu....kwa gharama nina uhakika nazo 100%.
 
vitu ambavyo huwa huhitajika ni kama wadau walivyosema hapo juu, lakin pia kitambulisho chako, kadi OG ya gari, kitambulisho cha anaeuza gari. Pia kama hauna TIN itabid uende na barua kutoka serikali za mitaa na passport size mbili. ndo hivyo ninavyovikumbuka kwa experience.
 
Habari za asubuh wakuu,
Naomba nijue taratibu na gharama za kubadili ownership ya gari TRA.
je pia gharama inategemea pesa mliyouziana?
natanguliza shukurani za pekee; Gari ina cc 1980 na kwa matumizi binafsi.
View attachment 492647
Ila kwanza hakikisha gari yako haina deni nikimaanisha MVL na RL maana hayo ndiyo yanayo acha deni na penalty juu kama hayajalipiiwa mda mrefu then utalipa 50,000/ gharama ya transfer halafu 10,000/ gharama ya kadi na 1% ya gharama ya gari hapo utakuwa umemamaliza mkuu

NB: hayo ni pale tu kama una tin namba na tin namba yako haidaiwi chochote maana yake miradi yako yote uliyo isajili kwa tin namba yako imelipiwa yote na haina deni ,kinyume na hapo jiandae kwa gharama za kufukia mashimo ya zamani kabla ya kuchimba shimo jipya.
 
Uende na tin number,mkataba uliosainiwa na hakimu,kadi original, fedha tasilimu si chini ya laki moja kutegemeana na fefha uli;nunulia gari yako(iliopo kwenye mkataba).
 
Back
Top Bottom