beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Raia wa Ghana, leo wanasherehekea miaka 63 ya uhuru wa Taifa hilo.
Ghana itawaliwa na Uingereza na kupata uhuru wake Machi Sita mwaka 1957, chini ya Mwanasiasa mashuhuri na mwanamapinduzi wa Taifa hilo Kwame Nkurumah.
Nkurumah ndiye alikua Waziri Mkuu wa kwanza wa Ghana baada ya uhuru na baadaye Rais wa Taifa hilo ambalo hapo awali lilijulikana kama Gold Coast.
Ghana ilikuwa ni nchi ya kwanza Kusini mwa Jangwa la Sahara kupata uhuru wake na baada ya hapo chini ya Mwanasiasa huyo mashuhuri Nkurumah, ilijitahidi kuhakikisha nchi nyingine za Afrika ikiwemo Tanzania zinapata uhuru wake.
Shamrashamra za kuadhimisha siku ya uhuru wa Ghana zinaendelea hivi sasa katika uwanja wa michezo wa Baba Yara uliopo kwenye mji wa Kumasi, ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika katika mji huo.
Kwa kawaida siku hiyo ya uhuru huwa ikisherehekewa na raia wa Ghana waliopo nchini humo na wale waliopo nje ya nchi, ambao wamekua wakifanya shughuli mbalimbali ili kuienzi siku hiyo.
Siku ya uhuru Ghana ni ya mapumziko ambapo wafanyakazi wa umma na wale wa sekta binafsi nao wanakua mapumziko ili kusherehekea siku hiyo ambayo wanaiona muhimu katika Taifa hilo ambalo lilikua likifahamika sana kwa utajiri wa dhahabu pamoja na pembe za ndovu.