Ghafla Liverpool imegeuka kuwa binti maringo?

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,438
GORDON Brown, Waziri Mkuu wa zamani wa England aliwahi kuulizwa ni kitu gani kizuri Waingereza wanazalisha kwa sasa na dunia nyingine inaweza kujivunia. Alijibu kwa maringo yaliyopitiliza. Alijibu kwa kifupi. “Ligi Kuu ya England”.

Unaweza kumkatalia? Hapana. Kuanzia Malaysia, Newala kule Mtwara, New Delhi India, Miami Marekani, Buenos Aires pale Argentina na hata Melbourne pale Australia. Wote tunasubiri Ligi Kuu ya England.

Mwamuzi wa pambano la Fulham na Arsenal, Chris Kavanagh atakapopuliza filimbi kuanzisha pambano la kwanza la Ligi Kuu ya England pale Craven Cottage tutakuwa tunakaribishwa katika ligi maarufu zaidi duniani. Tunasubiri kuona nini msimu huu? Liverpool atatetea taji? Man City atapora taji? Manchester United ataingia Top Four au kuwania ubingwa? Arsenal ataingia Top Four? Chelsea yupo katika anga za ubingwa? Wote tunatazama kule juu.

Wakati tukitazama juu tunamkuta mtu ambaye watu watakuwa na hasira naye zaidi. Liverpool. Ndiye namba moja mpaka sasa. Kuwa namba moja ni rahisi, kuendelea kuwa namba moja ni kitu kigumu zaidi katika maisha ya soka.

Liverpool kuna mawingu kidogo. Anatazamiwa kutetea taji lakini wako wapi wachezaji wapya? Nahisi kuna kiburi kinaendelea pale Anfield. Kama sio kocha basi matajiri wanaringia kikosi chao. Kiburi hiki kinatoka wapi?

Tulidhani wangeingia sokoni kwa nguvu kuimarisha kikosi chao. Wamemchukua beki Mgiriki, Kostas Tsimikas katika upande wa kushoto ambaye tunajua anakwenda kuwekwa benchi na Andy Robertson. Sioni akichukua namba pale. Robertson amefiti vema katika mfumo wa Jurgen Klopp.

Kabla ya hapo Januari alitua mchezaji anayeitwa Takumi Minamino ambaye mpaka sasa ameshindwa kujihakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza. Alikuwa mchezaji mzuri, lakini nadhani Klopp alitaka kutuonyesha uwezo wake wa kufanya maajabu ya kumgeuza mchezaji wa kawaida kuwa wa ajabu kama alivyofanya kwa Mane. Liverpool ilipaswa kuingiza kikosini wachezaji ambao wana ubora wa kupora nafasi za waliopo hasa katika eneo la kiungo na ushambuliaji. Inaonekana kama vile Klopp anawalinda Mo Salah, Sadio Mane na Roberto Firmino. Tulidhani angemchukua Timo Werner akamuacha aende Chelsea.

Tulidhani eneo hilo Klopp angepambana kumnasa mchezaji wa daraja la juu ambaye angeidai nafasi yake kutoka kwa Mane au Salah au Firmino. Hata hivyo mwamuzi wa pambano la Liverpool na Leeds akikaribia kuanzisha kipute pale Anfield bado hawa watatu hawajapewa mpinzani. Kwa sasa anahusishwa Thiago Alcantara. Inawezekana akamchukua. Huyu ndiye mchezaji tuliyemtarajia. Huyu ni aina ya mchezaji ambaye anaingia katika timu huku akiidai nafasi yake na si kusubiri kucheza mechi za Carabao au FA kama ninavyotazamia kwa Kostas Tsimikas.

Inawezekana Klopp anakwenda katika msimu mwingine wa nne wa timu iliyokamilika akiwa na matumaini yale yale. Kuna ule msimu aliukimbiza ubingwa wa Ulaya, lakini akapigwa fainali na Real Madrid pale Ukraine.

Kuna msimu mwingine ulikuja mbele yao ambapo waliukimbiza ubingwa wa Ulaya na kufanikiwa kuupata pale Madrid baada ya kuichapa Tottenham. Ndani ya msimu huo huo waliachwa pointi moja na Manchester City katika mbio za ubingwa.

Msimu uliofuata wametwaa ubingwa wa England. Namaanisha msimu uliopita. Yote haya yanafanyika huku Liverpool ikiwa na utatu mtakatifu pale mbele. Mane, Salah na Firmino. Wataendeleza mwendo mdundo mpaka lini? Ni swali la kujiuliza kwa umakini.

Wataendelea kupewa changamoto na Divork Origi mpaka lini? Labda angeingia Timo Werner angewapa changamoto zaidi. Timu lazima ichangamshwe mara kwa mara. Sir Alex Ferguson alikuwa ana uwezo wa kufanya hivyo.

Katika soka kuna kitu kinaitwa ‘Second Season syndrome’. Huu ni uchovu wa msimu wa pili baada ya kufanya vema katika msimu uliopita. Baada ya ubingwa wa England ambao waliusaka kwa miaka 30 hatuwezi kujua wachezaji wataamka msimu huu wakiwa na uchovu upi. Ni katika nyakati kama hizi, Sir Alex alikuwa anajua namna ya kukichangamsha kikosi chake.

Oktoba 5 dirisha la uhamisho litafungwa. Sio mbali sana katika masuala ya uhamisho kwa sababu kunakuwa na mchakato mrefu linapokuja suala la uhamisho wa mchezaji. Siamini kama Liverpool itakuwa na maajabu sana.

Majuzi nilimuona Jurgen Klopp akiwa na sura nyekundu alipoulizwa kusuasua kwa Liverpool katika uhamisho wa wachezaji. Akatoa jibu la kukejeli Chelsea na Manchester City kwamba zina pesa nyingi kutoka kwa matajiri wa mafuta. Ukweli ni kwamba tangu 2016 Liverpool ilipotinga fainali za Europa na kuanza kupata mafanikio mengi katika kipindi hiki ni wazi pia wameingiza pesa nyingi. Mafanikio hayaji bure. Yanaambatana na pesa.

Liverpool imevuna pesa nyingi kwa kutwaa ubingwa wa Ulaya na pia kufika fainali waliyochapwa msimu mmoja kabla.
Klopp asitake kuniambia Liverpool ni masikini. Ubahili wa sasa inawezekana unatokana na matajiri wa Kimarekani kuanza kuwa na mkono wa birika au yeye mwenyewe kuamua kuanza kufuata nyendo za Arsene Wenger. Sina ndoto nzuri kuhusu Liverpool ya msimu huu. Nina ndoto mbaya. Napata usingizi wa mang’amung’amu kidogo.

Edo Kumwembe
 
Kama ni Edo kumwembe achana naye..
hajawahi kutabiri ukweli juu ya Liverpool

Wakati liver inamchukua Alison aliponda sana, akasema pale hamna kitu.. baada ya kutua liver..amekua kipa bora duniani

mwaka jana wakati ligi inaanza alisema liver haitafanya vizuri kwa sababu hyo ya uchovu, kwamba wachezaji wa liver wamechoka baada ya kukimbizana na Manc city kwenye ubingwa na uefa.. kwa hiyo hawataweza si tu kuchukua ubingwa bali kuwa hata mshindani.
liver mwaka jana kachukua ubingwa kwa tofauti ya point nyingi tu

mwambie achambue team nyingine lakini sio Liverpool
 
Arsenal hii hii? Mechi mbili za mwisho ikiwemo Ngao ya hisani...Zote mbili amepigwa Huyo Liverpool...uwe unaweka na record as an evidence Ku support maneno yako na si kupuyanga tu.
kombe la mbuzi hilo
 
Ambacho huyu mwandishi akielewi usajili wa karne pale anfield ni klop. Huyu jamaa ni mastar plan anajua anachokitafuta na kwa jicho la nje huwez ona mpango mkakati wa klop msimu uliopita liver ilianza goigoi hivi hivi wakatokea wachambuzi uchwara kibao kila mtu akasema lake mwishowe tukanyanyua ligi.

Kuchukua ligi ni strategy haijalishi unachezaje ila point 3 ni muhimu ni nukuu kauli ya klop msimu uliopita " kila game ni fainali tunahitaji kupambana hata tukishinda kwa taabu lakini cha msingi tujihakikishie point 3" na kwny mahojiano yake mara nyingi awapi pressure wachezaji huwa anawaambia nyie ni binadamu makosa ni part ya ubinadamu cha msingi ni point 3 haijalishi. Tumechezaje lkn point 3 tumeziweka kibindoni mark my words
Msimu huu competitor pekee wa liver ni man city tu tena ubingwa unaweza amuliwa na upatikanaji wa ushindi baina ya liver na man city
 
Ameongea ukweli mtupu ila Kops walio wengi hawataki kusikia hayo maneno
 
Kwa maana hiyo una uhakika wa kuchukua points 6 au 4 katika hizi mechi;

Man. United
Chelsea
Man. City
Arsenal
Spurs
Everton
 
Kama ni Edo kumwembe achana naye..
hajawahi kutabiri ukweli juu ya Liverpool

Wakati liver inamchukua Alison aliponda sana, akasema pale hamna kitu.. baada ya kutua liver..amekua kipa bora duniani

mwaka jana wakati ligi inaanza alisema liver haitafanya vizuri kwa sababu hyo ya uchovu, kwamba wachezaji wa liver wamechoka baada ya kukimbizana na Manc city kwenye ubingwa na uefa.. kwa hiyo hawataweza si tu kuchukua ubingwa bali kuwa hata mshindani.
liver mwaka jana kachukua ubingwa kwa tofauti ya point nyingi tu

mwambie achambue team nyingine lakini sio Liverpool
ukileta ushahidi aliposema Allison hamna kitu nipigwe ban.
 
GORDON Brown, Waziri Mkuu wa zamani wa England aliwahi kuulizwa ni kitu gani kizuri Waingereza wanazalisha kwa sasa na dunia nyingine inaweza kujivunia. Alijibu kwa maringo yaliyopitiliza. Alijibu kwa kifupi. “Ligi Kuu ya England”.

Unaweza kumkatalia? Hapana. Kuanzia Malaysia, Newala kule Mtwara, New Delhi India, Miami Marekani, Buenos Aires pale Argentina na hata Melbourne pale Australia. Wote tunasubiri Ligi Kuu ya England.

Mwamuzi wa pambano la Fulham na Arsenal, Chris Kavanagh atakapopuliza filimbi kuanzisha pambano la kwanza la Ligi Kuu ya England pale Craven Cottage tutakuwa tunakaribishwa katika ligi maarufu zaidi duniani. Tunasubiri kuona nini msimu huu? Liverpool atatetea taji? Man City atapora taji? Manchester United ataingia Top Four au kuwania ubingwa? Arsenal ataingia Top Four? Chelsea yupo katika anga za ubingwa? Wote tunatazama kule juu.

Wakati tukitazama juu tunamkuta mtu ambaye watu watakuwa na hasira naye zaidi. Liverpool. Ndiye namba moja mpaka sasa. Kuwa namba moja ni rahisi, kuendelea kuwa namba moja ni kitu kigumu zaidi katika maisha ya soka.

Liverpool kuna mawingu kidogo. Anatazamiwa kutetea taji lakini wako wapi wachezaji wapya? Nahisi kuna kiburi kinaendelea pale Anfield. Kama sio kocha basi matajiri wanaringia kikosi chao. Kiburi hiki kinatoka wapi?

Tulidhani wangeingia sokoni kwa nguvu kuimarisha kikosi chao. Wamemchukua beki Mgiriki, Kostas Tsimikas katika upande wa kushoto ambaye tunajua anakwenda kuwekwa benchi na Andy Robertson. Sioni akichukua namba pale. Robertson amefiti vema katika mfumo wa Jurgen Klopp.

Kabla ya hapo Januari alitua mchezaji anayeitwa Takumi Minamino ambaye mpaka sasa ameshindwa kujihakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza. Alikuwa mchezaji mzuri, lakini nadhani Klopp alitaka kutuonyesha uwezo wake wa kufanya maajabu ya kumgeuza mchezaji wa kawaida kuwa wa ajabu kama alivyofanya kwa Mane. Liverpool ilipaswa kuingiza kikosini wachezaji ambao wana ubora wa kupora nafasi za waliopo hasa katika eneo la kiungo na ushambuliaji. Inaonekana kama vile Klopp anawalinda Mo Salah, Sadio Mane na Roberto Firmino. Tulidhani angemchukua Timo Werner akamuacha aende Chelsea.

Tulidhani eneo hilo Klopp angepambana kumnasa mchezaji wa daraja la juu ambaye angeidai nafasi yake kutoka kwa Mane au Salah au Firmino. Hata hivyo mwamuzi wa pambano la Liverpool na Leeds akikaribia kuanzisha kipute pale Anfield bado hawa watatu hawajapewa mpinzani. Kwa sasa anahusishwa Thiago Alcantara. Inawezekana akamchukua. Huyu ndiye mchezaji tuliyemtarajia. Huyu ni aina ya mchezaji ambaye anaingia katika timu huku akiidai nafasi yake na si kusubiri kucheza mechi za Carabao au FA kama ninavyotazamia kwa Kostas Tsimikas.

Inawezekana Klopp anakwenda katika msimu mwingine wa nne wa timu iliyokamilika akiwa na matumaini yale yale. Kuna ule msimu aliukimbiza ubingwa wa Ulaya, lakini akapigwa fainali na Real Madrid pale Ukraine.

Kuna msimu mwingine ulikuja mbele yao ambapo waliukimbiza ubingwa wa Ulaya na kufanikiwa kuupata pale Madrid baada ya kuichapa Tottenham. Ndani ya msimu huo huo waliachwa pointi moja na Manchester City katika mbio za ubingwa.

Msimu uliofuata wametwaa ubingwa wa England. Namaanisha msimu uliopita. Yote haya yanafanyika huku Liverpool ikiwa na utatu mtakatifu pale mbele. Mane, Salah na Firmino. Wataendeleza mwendo mdundo mpaka lini? Ni swali la kujiuliza kwa umakini.

Wataendelea kupewa changamoto na Divork Origi mpaka lini? Labda angeingia Timo Werner angewapa changamoto zaidi. Timu lazima ichangamshwe mara kwa mara. Sir Alex Ferguson alikuwa ana uwezo wa kufanya hivyo.

Katika soka kuna kitu kinaitwa ‘Second Season syndrome’. Huu ni uchovu wa msimu wa pili baada ya kufanya vema katika msimu uliopita. Baada ya ubingwa wa England ambao waliusaka kwa miaka 30 hatuwezi kujua wachezaji wataamka msimu huu wakiwa na uchovu upi. Ni katika nyakati kama hizi, Sir Alex alikuwa anajua namna ya kukichangamsha kikosi chake.

Oktoba 5 dirisha la uhamisho litafungwa. Sio mbali sana katika masuala ya uhamisho kwa sababu kunakuwa na mchakato mrefu linapokuja suala la uhamisho wa mchezaji. Siamini kama Liverpool itakuwa na maajabu sana.

Majuzi nilimuona Jurgen Klopp akiwa na sura nyekundu alipoulizwa kusuasua kwa Liverpool katika uhamisho wa wachezaji. Akatoa jibu la kukejeli Chelsea na Manchester City kwamba zina pesa nyingi kutoka kwa matajiri wa mafuta. Ukweli ni kwamba tangu 2016 Liverpool ilipotinga fainali za Europa na kuanza kupata mafanikio mengi katika kipindi hiki ni wazi pia wameingiza pesa nyingi. Mafanikio hayaji bure. Yanaambatana na pesa.

Liverpool imevuna pesa nyingi kwa kutwaa ubingwa wa Ulaya na pia kufika fainali waliyochapwa msimu mmoja kabla.
Klopp asitake kuniambia Liverpool ni masikini. Ubahili wa sasa inawezekana unatokana na matajiri wa Kimarekani kuanza kuwa na mkono wa birika au yeye mwenyewe kuamua kuanza kufuata nyendo za Arsene Wenger. Sina ndoto nzuri kuhusu Liverpool ya msimu huu. Nina ndoto mbaya. Napata usingizi wa mang’amung’amu kidogo.

Edo Kumwembe
😂😂😂😂😆😆😆😆😆 TUMEONGOZA KUPATA MAJERUHI WENGI SANA CHANGANYA NA AKINA DALA NA MANE KUPATA CORONA NA TULIFUNGWA NA ASTON VILLA 7-1 LAKINI MPAKA SASA TUNAONGOZA LIGI NA TUNA GD 17 NYINGI ZAIDI YA TIMU ZOTE...WHAT A TEAM LAZIMA MTESEKE SANA NI.BACK TO BACK.....💥💥💥💥
 
TUMEONGOZA KUPATA MAJERUHI WENGI SANA CHANGANYA NA AKINA DALA NA MANE KUPATA CORONA NA TULIFUNGWA NA ASTON VILLA 7-1 LAKINI MPAKA SASA TUNAONGOZA LIGI NA TUNA GD 17 NYINGI ZAIDI YA TIMU ZOTE...WHAT A TEAM LAZIMA MTESEKE SANA NI.BACK TO BACK.....
Kwa mbinde
 
Arsenal hii hii? Mechi mbili za mwisho ikiwemo Ngao ya hisani...Zote mbili amepigwa Huyo Liverpool...uwe unaweka na record as an evidence Ku support maneno yako na si kupuyanga tu.
Bado huamini kuwa aseno ni mbovu?
 
Back
Top Bottom