Nampenda na yeye ananipenda. Kinachoniumiza kuna watu wanaonifahamu wanamfeed mambo yangu ambayo hayamvutii. Kuna wengine wanamtajia wasichana niliowahi kuwa nao. Mwingine alifika mbali zaidi na kumwambia mimi nimeoa na kuacha mke. Huwa ananiulizia majina ya hao wasichana na tulikuwa na uhusiano gani! Nilishamwambia kuwa nilikuwa na mahusiano huko nyuma na nimeacha lakini sikumtajia majina yao. Hivi haniamini? Nifanyeje? Naona kama itavunja uhusiano, maana kuna muda huwa nakasirika ila najishusha.
Kama unampenda kwa dhati then umwambie vitu vinavyokuhusu ambavyo unahisi akiambiwa na mtu mwingine itakuwa disaster....ni bora asikie kutoka kwako kuliko kutoka mdomoni mwa mwingine..niamini mimi,lazima uaminifu upungue especially wakati akikuuliza unaanza kubabaika...ndo kabisa atakuona una vitu vyako vya kijinga unavificha...Funguka bro!!
Na si unajua mdomo haulipiwi kodi...mtu akiamua kuliongelea lako likitiwa chumvi hilo...haliliki hata kwa ndimu lazima GF wako akasirike,so kama una vijimambo vyako bora umwambie..
kwa nini usimwambie past yako yote huyo mdada?
hehehehe hapo chacha kuna watu wana msururu wa totoz kiasi akianza kutoa historia huyo demu mwenyewe anaweza kuanza kuwazia kusepa .