Getrude Mongella amvaa Rais Kikwete

Getrude Mongella amvaa Rais Kikwete

rosemarie

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
6,887
Reaction score
3,439
WAKATI tuzo ya kuuenzi Muungano iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa Jaji Joseph Warioba ikiibua maswali, Rais mstaafu wa Bunge la Afrika, Gertrude Mongela, amekosoa upendeleo uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete katika utoaji wa tuzo hiyo.

Mongela ambaye amepata kuwa Mbunge wa Ukerewe kwa muda mrefu, amemshangaa Rais Kikwete kuwatunukia wanaume pekee nishani ya kuuenzi Muungano na kuwaacha wanawake ambao wapo waliofanya mambo makubwa ya kuuenzi Muungano kuliko hao waliopewa.

Akizungumza katika mkutano wa pili wa masuala ya jinsia katika nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Mongela alisema ameshangaa kuona katika orodha ya waliopewa tuzo hakuna mwanamke hata mmoja wakati anawafahamu wanawake wengi waliofanya mambo makubwa katika kuuenzi Muungano.

"Wapo wanawake wengi ambao wameuenzi Muungano huu kama kina Mwanaidi Makame, mwanamke ambaye alikuwa akiimba nyimbo za kuhamasisha Muungano, kwanini mwanamke kama huyo asingepewa tuzo?" alihoji Mongela.

Mongela aliwataja wanawake wengine aliosema wangepaswa kupata tuzo hiyo kuwa ni Mama Sophia Kawawa, aliyeanzisha mapambano ya kumkomboa mwanamke wakati huo akiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), ambapo alipigania kuondoa sheria ya kuwazuia watoto wa kike kusoma moja kwa moja na badala yake waishie kidato cha sita na kupewa kazi.

"Mwanamama huyo pamoja na elimu yake ndogo ya kujua kusoma na kuandika lakini alikuwa na upeo mkubwa wa kupambanua mambo na hatimaye alifanikiwa kumshawishi Mwalimu Nyerere kuondoa sheria hiyo na kuwaruhusu watoto wa kike kusoma moja kwa moja hadi Chuo Kikuu," alisema.

Kwa mujibu wa Mongela, mwanamke mwingine aliyestahili tuzo hiyo ni Mama Maria Nyerere, aliyemtunza Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere wakati alipokuwa akipigania Muungano.

Hata hivyo Mama Maria Nyerere alipewa nishani ya Muungano ya daraja la nne.

Akizungumzia kuhusu mwenendo wa mchakato wa Katiba Mpya, Mongela alionyesha kukerwa na namna ambavyo Bunge limeendeshwa, kutokana na wajumbe wengi kutoleana lugha za matusi na kusahau kujadili masuala muhimu yaliyowaleta bungeni.

"Wajumbe walikuwa wakitumia muda mwingi kujadili muundo wa serikali wakati wanajua kabisa wingi wa serikali hauna masilahi kwa Watanzania wengi. Hadi sasa tuna serikali nyingi, kwani zipo za mitaa, vijiji na serikali kuu," alisema.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia kwa Wanawake (TGNP), Lilian Liundi, alitoa wito kwa serikali kuhakikisha wanakamilisha malengo waliyojiwekea ya kuwa na uwakilishi wa 50 kwa 50 kati ya wanaume na wanawake ifikapo mwaka 2015.

Ingawa Liundi alikiri kwamba hadi sasa Tanzania imefanikiwa kupata asilimia 30 ya uwakilishi wa wanawake katika ngazi za maamuzi, lakini alishauri nafasi hizo zisiishie eneo la siasa na badala yake ziwe pia katika sehemu nyingine, zikiwamo za kiuchumi, sayansi na teknolojia.

Liundi alifafanua kuwa suala la 50 kwa 50 linatakiwa kuanzia ngazi ya chini hadi juu na kwa kila sekta.

Akizungumzia changamoto zilizopo kwa wanawake, alisema ni pamoja na kuongezeka kwa vitendo vya kikatili, wanawake wengi kutomiliki mali, hali inayowafanya kutokopesheka huku watoto wa kike wakikosa elimu kwa usawa.

Mbali na Jaji Warioba, wengine waliopewa nishani katika daraja hilo ni Aboud Jumbe Mwinyi, aliyekuwa Rais wa Pili wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, John Malecela, Cleopa Msuya na Dk. Salmin Amour Juma.

Wamo pia Dk. Omar Ali Juma na Idriss Abdul Wakil, ambao sasa ni marehemu.

Walioanza kupata tuzo na nishani hizo ni waasisi wa Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Aman Karume (wote ni marehemu) na kufuatiwa na Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.

Wengine ni pamoja na viongozi wa majeshi ya ulinzi na usalama, akiwamo Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jenerali Davis Mwamunyange na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu.

Wakuu wa JWTZ wastaafu pia walikumbukwa, akiwamo, Jenerali Mirisho Sarakikya na Jenerali David Musuguri.

Waliotunukiwa nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Nne, walikuwa ni Mama Maria Nyerere na Mama Fatma Karume; Bendi ya Msondo Ngoma pia ilipewa tuzo kwa kuuenzi Muungano.

Naye Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi, alipewa tuzo maalumu akiwa raia wa Tanzania aliyetoa mchango muhimu katika huduma za jamii.

Source: Tanzania Daima
 
huyu amepigwa chini ubunge na machemli wa chadema.

kuna watu wanakera sana ningekuwa mimi ndio kikwete ningemshauri atulie tuzo za kili award zinakuja huenda akapata tuzo na yeye.
 
Hakika namuunga mkono maana hata Bibi Titi Mohamed. Sina uhakika kuhusu Kawawa Mwennyewe kama alikumbukwa. Kitenngoo kilichoshughulikia tuzo alipewa kusimamia mtu asiye na uzoefu au aasiyejua historia, lakini je hata katika siku nyeti kama hii. Kingunge sijawaona Chief Adam Sapi Mkwawa, Wakuu wastaafu Usalama wa Taifa eeee jamani hawa watu hawalali kunusa habari za uhalifu dhidi ya Muungano lakkini..............
Tupo wengi tumeachhwa. Kama kapata Warioba pamoja na kuibua hii motion ya Serikali tatu kwanini Josseph Butikuu asipate?
Kama Aboud Jumbe Mwinyi alipewaa tuzo ya kuuenzi muungano basi Maalim Seif Sharif Hamad alistahili kupewa tena hata kuliko Jumbe, maana ndiye aliyefichua njama za Jumbe kuuvunja muungano kifupi mantiki ya tuzo haina 'mashiko''
 
huyu amepigwa chini ubunge na machemli wa chadema.

kuna watu wanakera sana ningekuwa mimi ndio kikwete ningemshauri atulie tuzo za kili award zinakuja huenda akapata tuzo na yeye.

Nimecheka sana...

Halafu kulikua na haja gani ya kumsifia mama Kawawa huku akimfanya Nyerere aonekane pamoja na exposure yote aliyokuwa nayo na elimu kubwa kuwa alikua kikwazo kwa wanawake kusoma hadi aliposhawishiwa na Mama Kawawa na kuondoa kikwazo(sheria) hicho? Anataka kusema nini?
 
Kumbe nyerere alikuwa kikwazo kwa wanawake kusoma ! anasingizia kutosoma kwake kuwa kulisababishwa na Nyerere, mfa maji aachi kutapatapa
 
Huyu mama sasahivi hata hana sauti, tangu aharibu kwenye uspika Bunge la Africa Mashariki sina hamu naye. Atulie tu, system waliyoilea ndiyo tayari ishamtupa hivyo.
 
Huyu mama baada ya kutimuliwa bunge la Afrika kwa ubaguzi wa kikabila amefilisika kisiasa kabisa, sasa anatafuta sehemu ya kutokea. Hiyo 50/50 kwenye kazi za professional inawezekanaje? Je kuwe na Madereva wa viti maalumu ili idadi ya madereva daladala, bodaboda, malorry nk wawe idadi sawa na wanaume? Shule zote za mjini ukiingia staff ni perfume na mapouda tu, karibu 80% t0 90% ni wanawake, je wanaume tuandamane?

Mawazo muflisi haya. Akae alee wajukuu aachane na siasa kwani anakoelekea siko.
 
hizi kelele nishazichoka,wakiwa kwenye system kimya,wakitoka ndo makalele kibao,mmmanina...wakafie mbele huko
 
alipokuwa kwenye system alifanya nn?
Tena huyu mama Mongela ndo asiseme maana katutia aibu kubwa kwa kuiba samani za nyumba alipokuwa huko Afrika Kusini kama mwenyekiti wa bunge la Afrika.
 
  • Thanks
Reactions: jme
WAKATI tuzo ya kuuenzi Muungano iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa Jaji Joseph Warioba ikiibua maswali, Rais mstaafu wa Bunge la Afrika, Gertrude Mongela, amekosoa upendeleo uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete katika utoaji wa tuzo hiyo.

Mongela ambaye amepata kuwa Mbunge wa Ukerewe kwa muda mrefu, amemshangaa Rais Kikwete kuwatunukia wanaume pekee nishani ya kuuenzi Muungano na kuwaacha wanawake ambao wapo waliofanya mambo makubwa ya kuuenzi Muungano kuliko hao waliopewa.

Akizungumza katika mkutano wa pili wa masuala ya jinsia katika nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Mongela alisema ameshangaa kuona katika orodha ya waliopewa tuzo hakuna mwanamke hata mmoja wakati anawafahamu wanawake wengi waliofanya mambo makubwa katika kuuenzi Muungano.

"Wapo wanawake wengi ambao wameuenzi Muungano huu kama kina Mwanaidi Makame, mwanamke ambaye alikuwa akiimba nyimbo za kuhamasisha Muungano, kwanini mwanamke kama huyo asingepewa tuzo?" alihoji Mongela.

Mongela aliwataja wanawake wengine aliosema wangepaswa kupata tuzo hiyo kuwa ni Mama Sophia Kawawa, aliyeanzisha mapambano ya kumkomboa mwanamke wakati huo akiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), ambapo alipigania kuondoa sheria ya kuwazuia watoto wa kike kusoma moja kwa moja na badala yake waishie kidato cha sita na kupewa kazi.

"Mwanamama huyo pamoja na elimu yake ndogo ya kujua kusoma na kuandika lakini alikuwa na upeo mkubwa wa kupambanua mambo na hatimaye alifanikiwa kumshawishi Mwalimu Nyerere kuondoa sheria hiyo na kuwaruhusu watoto wa kike kusoma moja kwa moja hadi Chuo Kikuu," alisema.

Kwa mujibu wa Mongela, mwanamke mwingine aliyestahili tuzo hiyo ni Mama Maria Nyerere, aliyemtunza Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere wakati alipokuwa akipigania Muungano.

Hata hivyo Mama Maria Nyerere alipewa nishani ya Muungano ya daraja la nne.

Akizungumzia kuhusu mwenendo wa mchakato wa Katiba Mpya, Mongela alionyesha kukerwa na namna ambavyo Bunge limeendeshwa, kutokana na wajumbe wengi kutoleana lugha za matusi na kusahau kujadili masuala muhimu yaliyowaleta bungeni.

"Wajumbe walikuwa wakitumia muda mwingi kujadili muundo wa serikali wakati wanajua kabisa wingi wa serikali hauna masilahi kwa Watanzania wengi. Hadi sasa tuna serikali nyingi, kwani zipo za mitaa, vijiji na serikali kuu," alisema.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia kwa Wanawake (TGNP), Lilian Liundi, alitoa wito kwa serikali kuhakikisha wanakamilisha malengo waliyojiwekea ya kuwa na uwakilishi wa 50 kwa 50 kati ya wanaume na wanawake ifikapo mwaka 2015.

Ingawa Liundi alikiri kwamba hadi sasa Tanzania imefanikiwa kupata asilimia 30 ya uwakilishi wa wanawake katika ngazi za maamuzi, lakini alishauri nafasi hizo zisiishie eneo la siasa na badala yake ziwe pia katika sehemu nyingine, zikiwamo za kiuchumi, sayansi na teknolojia.

Liundi alifafanua kuwa suala la 50 kwa 50 linatakiwa kuanzia ngazi ya chini hadi juu na kwa kila sekta.

Akizungumzia changamoto zilizopo kwa wanawake, alisema ni pamoja na kuongezeka kwa vitendo vya kikatili, wanawake wengi kutomiliki mali, hali inayowafanya kutokopesheka huku watoto wa kike wakikosa elimu kwa usawa.

Mbali na Jaji Warioba, wengine waliopewa nishani katika daraja hilo ni Aboud Jumbe Mwinyi, aliyekuwa Rais wa Pili wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, John Malecela, Cleopa Msuya na Dk. Salmin Amour Juma.

Wamo pia Dk. Omar Ali Juma na Idriss Abdul Wakil, ambao sasa ni marehemu.

Walioanza kupata tuzo na nishani hizo ni waasisi wa Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Aman Karume (wote ni marehemu) na kufuatiwa na Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.

Wengine ni pamoja na viongozi wa majeshi ya ulinzi na usalama, akiwamo Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jenerali Davis Mwamunyange na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu.

Wakuu wa JWTZ wastaafu pia walikumbukwa, akiwamo, Jenerali Mirisho Sarakikya na Jenerali David Musuguri.

Waliotunukiwa nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Nne, walikuwa ni Mama Maria Nyerere na Mama Fatma Karume; Bendi ya Msondo Ngoma pia ilipewa tuzo kwa kuuenzi Muungano.

Naye Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi, alipewa tuzo maalumu akiwa raia wa Tanzania aliyetoa mchango muhimu katika huduma za jamii.

Source: Tanzania Daima

labda ingewekwa orodha wa wote waliotunukiwa nishani hiyo Desemba 25,2014 kwani inadaiwa ni watu hamsini
 
Anaongea nini huyu mama, wakati hamthamini mumewe hata kidogo?! Arudishe samani za watu alizokwiba huko SA ndio amuhoji rais
 
"Wajumbe walikuwa wakitumia muda mwingi kujadili muundo wa serikali wakati wanajua kabisa wingi wa serikali hauna masilahi kwa Watanzania wengi.
Hadi sasa tunaserikali nyingi, kwani zipo za mitaa, vijiji na serikali kuu," alisema.

Source: Tanzania Daima

Huwa likija suala la muundo wa muungano huwa wanajitoa akili ya kawaida na kuja full nonsense... Why???
 
mbona mwanae John Mongella alipopewa U DC hakulalamika na watoto wa walalahoi wapewe hizo nafasi, yeye atulie zama zake zishapita
 
Anaongea nini huyu mama, wakati hamthamini mumewe hata kidogo?! Arudishe samani za watu alizokwiba huko SA ndio amuhoji rais

Kweli hamthamini mumewe!!, iweje sasa yeye anataka athaminiwe? anu ndo mazoea ya vyeo vya kupewa.. anataka favor kila kona. mumewe yuko wapi?
 
mkiwa wakame bila vyeo mnakuwa na kelele mkiwa madarakani mnakuwa wakimya na wapole.hama chama cha intalahamwe ccm kama unautaka ubunge.shida yake mama g. ni ubunge
 
Back
Top Bottom