Gerson Msigwa amechemsha tena katika Mahojiano Medani za Siasa "Royal Tour" Star Television

Mkuu umewasilisha na kuchambua vyema sana,hakika hili ni aina ya maandiko JF Yanatakiwa andikwa.
Level za uwajibikaji umeshuka sana,watu wanafanya kazi kwa biznes as usual,SASHA kwenye usimamizi anafeli na si ajabu kuna watu na ajenda zao wanampa ushauri usio sahihi kwa maslahi yao.
Tunapay the price of putting ahead siasa badala ya maslahi ya nchi.
Kwanza ahsante mkuu VERDAD

Niendelee kwa kusema kwamba nchi hii tumegawanyika kwa matabaka mawili makubwa yaani wavuja jasho na unyonge wao dhidi ya walamba Asali na wapiga debe wao ambao ni wanufaika kwa mlango wa pili.

Sasa humo kuna wanasisas toka milengo yote miwili na pia kutoka pande zote mbili.

Milengo...wavuja jasho na watetezi wao dhidi ya walamba Asali na wapambe wao.

Pande mbili...Chama tawala na vyama pinzani.

Kote huko kuna wajasiliamali wa kisiasa kwa manufaa yao binafsi.
 
Naafiki hii

Tunahitaji bunge lenye nguvu ya kuhoji haya mambo, tutaingizwa mkenge na foreigners wakatuachia kesho mbovu kama kwenye gas
Kweli kabisa...hata huko kwenye ziara kuna mikataba ya gesi imesainiwa...kwa mujibu wa maelezo ya Gerson Msigwa wakati akijibu mojawapo ya maswali ya Odemba.
 
Kwanza ahsante mkuu VERDAD

Niendelee kwa kusema kwamba nchi hii tumegawanyika kwa matabaka mawili makubwa yaani wavuja jasho na unyonge wao dhidi ya walamba Asali na wapiga debe wao ambao ni wanufaika kwa mlango wa pili.

Sasa humo kuna wanasisas toka milengo yote miwili na pia kutoka pande zote mbili.

Milengo...wavuja jasho na watetezi wao dhidi ya walamba Asali na wapambe wao.

Pande mbili...Chama tawala na vyama pinzani.

Kote huko kuna wajasiliamali wa kisiasa kwa manufaa yao binafsi.
👍 Well said mkuu,ndio maana maisha yangu sitaki sikia ushabiki wa vyama na itatokea hivyo ikiwa tuu ugali wangu utatoka huko maana hakuna mwenye nia ya kutukomboa ss walala hoi ama wavuja jasho kama usemavyo
 
Watutajie basi ili nasi tuwashukuru kwa misaada waliotoa ili kufanikisha jambo hili kwani kuna ubaya gani?
Hata sinema za Hollywood zote huwa zinatoa orodha ya wawezeshaji na wote waliowezesha sinema kutengenezwa bila kificho.
 
Ukweli wa wadau waliochangia Loyo tua mtawajua bila kificho mara tu Hangaya akiwa nje Taasisi,kwasasa thubutu.
 
Usiri wa serikali kuhusu wafadhili wa "Royal Tour" na gharama halisi zilizotumika.
Pamoja na ukubwa wa msafara wa uzinduzi.

Kipindi ni Medani za siasa kwenye Luninga ya Star TV.jioni hii 30/04/2025.

Muendesha kipindi ni Mtangazaji star tv.
Chief Odemba.

Mgeni mualikwa ni Msemaji mkuu wa serikali.
Gerson Msigwa.

Odemba.... kabla ya yote amemkumbusha Msigwa kwamba....

"Katika kipindi cha kwanza tulichokifanya hapa star tv,kuhusu filamu hii.
Msigwa uliahidi kutaja gharama zote za filamu baada ya kuwa imekamilika na kuzinduliwa."

Na leo tuko hapa tena.....

"Je unaweza sasa kuwaambia Watanzania kuhusu kiwango halisi cha gharama zilizotumika za utengenezaji wa filamu hii ambayo ni makala ya utalii maarufu kama Tanzania Royal Tour.
Pamoja na wafadhili walioko nyuma ya ufadhili huo?"

Msigwa amejibu kwamba...."serikali ilikwishatoa majibu kuhusiana na hilo ambapo
Filamu hiyo imegharimu 7bilioni shilingi za kitanzania.
Ambazo zimechangwa na wadau binafsi pamoja na taasisi mbalimbali nchini.

Mwendesha kipindi akamwambia.......

"Watanzania wanataka kuwajua wafadhili rasmi wa gharama za filamu hiyo na kwa nini inakuwa siri?"

Msigwa amehamaki na kuonekana kutokuwa tayari kuwataja wahusika na badala yake akasema ni....

"Taasisi na watu binafsi waliojitolea na hii ni baada ya serikali kuunda tume ya kuratibu upatikanaji wa pesa za hiyo project."

Na kuitangaza huko Dodoma.
Chini ya Dk Hassan Abbas ambaye ni katibu mkuu wizara ya habari.

Huku akionekana mwenye hasira Msigwa akatamka...

"Watanzania waache kuhoji gharama na ufadhili wa filamu hii,badala yake waangalie matokeo yake."

Akaendelea kusema.....
"Hata hao kina Greenbarg huwa hawataki kutumia hela za serikali!"

Kisha Odemba akamuuliza Msigwa....
"kama wao hawataki kutumia hela za serikali mbona Dk Abbas ni mtumishi wa serikali na unasema serikali iliratibu ukunyasanyaji fedha hizo?"

Msigwa akajibu..."Odemba nenda pale hazina kama utaona kuna bajeti ya Royal Tour!"

Odemba amemuuliza pia kuhusu idadi kubwa ya watu waliokwenda Marekani kwenye uzinduzi na gharama zilizotumika?

Msigwa akajibu...
"Ukiondoa Rais na msafara wake,hao wengine kila mmoja amekwenda kwa gharama zake binafsi au taasisi yake"

Odemba pia amemuuliza Msigwa....
Je ilikuwa ni vema Mheshimiwa Rais kwenda kuongelea nje ya nchi kuhusu mahusiano yake au tofauti zake yeye na mtangulizi wake JPM?

Msigwa akajibu.......

"Odemba...mimi nilikuwepo siku hiyo,ila tusiyakuze saana haya mambo maana mimi niliyachukulia kama mazungumzo baada ya habari."

Kwa ujumla Msemaji wa serikali amejichanganya sana kwenye mambo mengi aliyoulizwa,tukiachana hata na haya ya Royal Tour.

Kulikuwa na maswali mengi zaidi kuhusiana na sekta mbalimbali ikiwemo madini na nishati pamoja na Uchumi na uwekezaji.

Unaweza kuyapata mahojiano haya kupitia.
Facebook na Instagram@chiefodemba.tz

Imeonekana Msigwa hakujiandaa kwenda kukutana na maswali aliyokutana nayo pale Star Television.
Bali alitarajia kukutana na maswali waliyozowea kuulizwa na wanahabari wetu huko TBC na kwingineko huku neno Mheshimiwa likitawala mahojiano.

Msemaji makini wa serikali,walau angebeba baadhi ya dondoo za takwimu toka kwenye makabrasha yake,(kama anayo).
Pengine ingemsaidia kuweza kujibu maswali kwa ufasaha.Badala ya kwenda bila hata Ipad mkononi ili imsaidie baadhi ya kumbukumbu kulingana na interview ile.

●Tahadhari yangu kama raia na mpenda maendeleo ya nchi yetu Tanzania.

Ninapenda wahusika wa upande wa serikali, kuhusiana na filamu hii muhimu ya makala ya utalii kwa nchi yetu.....waelewe kwamba......

Kitendo cha kuficha gharama halisi,ufadhili pamoja na uwazi kwenye umiliki rasmi wa hii Documentary.

Ni suala ambalo linaweza kuja kuzalisha kashfa mbaya huko mbeleni.
Endapo itagundulika matumizi mabaya ya fedha za Umma kwa kificho au kufadhiliwa na watu ambao walikuwa na ajenda zao bila Mheshimiwa Rais kujuwa.

Na kama hapo baadae itakuja kuibuliwa kashfa yoyote katika moja ya mikataba tunayoambiwa wameisaini huko Marekani.
Kwenye ziara ambayo wamemhusisha na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ni kitendo ambacho kitaiponza na kitaiharibia jina na soko.
Sio tu filamu hiyo na Rais wetu.
Bali taifa na sekta ya utalii kwa ujumla.

Wazungu huwa hawana urafiki na kashfa ya aina zozote hasa zinazoihusha serikali dhidi ya raia wake.

Huwa hawapendi kuhusishwa nazo na pia hupenda kujitenga nazo kwa kutotaka kulipia chochote kilichotokana na jasho lao kwenda kwenye serikali zenye kashfa.
View attachment 2206994View attachment 2206995
Huyyu Gresin Msigwa anamajivuno Sana. Anajisikia Sana kumbe kichwani ni Kama Mimi.

Anaonekana ni mkesha miziki huyu hiyo nafasi haimfai. Happy Kuna maswali ambayo hata Mimi ningeyajibu na watu wakaridhika.
 
Rais anakubali kulipiwa gharama yeye na delegation yake kwa wiki mbili Marekani ili iweje yaani.

Kwa makubaliano yapi??

Je unaweza mdai kodi mtu aliyekulipia tripu ya wiki mbili marekani??

Kwanini Rostam Aziz hakosekani kwenye msafara wa Rais??

Kwani ni yeye tu ni mfanyabishara mzalendo anayehitaji support ya Rais??
 
Kweli kabisa...hata huko kwenye ziara kuna mikataba ya gesi imesainiwa...kwa mujibu wa maelezo ya Gerson Msigwa wakati akijibu mojawapo ya maswali ya Odemba.
Mungu wetu atatuchoka very soon
 
Rais anakubali kulipiwa gharama yeye na delegation yake kwa wiki mbili Marekani ili iweje yaani.

Kwa makubaliano yapi??

Je unaweza mdai kodi mtu aliyekulipia tripu ya wiki mbili marekani??

Kwanini Rostam Aziz hakosekani kwenye msafara wa Rais??

Kwani ni yeye tu ni mfanyabishara mzalendo anayehitaji support ya Rais??
Brooo kinachofuata ni kulipa fadhila tunakuwa na viongozi wenye uwezo mdogo, wenye mahasira mwisho tunaanza kutekana na kufanyiana unyama.

Majina yameshafika Ikulu yako mezani subirini fadhila.
 
Brooo kinachofuata ni kulipa fadhila tunakuwa na viongozi wenye uwezo mdogo, wenye mahasira mwisho tunaanza kutekana na kufanyiana unyama.

Majina yameshafika Ikulu yako mezani subirini fadhila.
Yale mambo ya kutekana yatarejea upya na kwa kasi kubwa maana kadri kelele zitakapokua zinazidi ndivyo nao watakuwa wanatumia mbinu mbali mbali kuzizima.

Ukiuliza sana unajitia hatarini maana unakua unashtua watu na kuwaharibia kula yao.

We better be very careful.
 
Back
Top Bottom