Humu ndani suala la emulator ya android kwenye pc sio geni watu wengi wanaulizia jinsi ya kueka whatsapp kwenye pc na vitu kama hivi. kuna kipindi kuna game la android nilitaka kulicheza kwenye pc nikadownload emulator zaidi ya 5 za android bila mafanikio mwisho nikaja kufanikiwa kwa kutumia hii genymotion. emulator hii ni unique na pia inahitaji utaalam kidogo ila kwa muongozo mzuri ukifanikiwa kuieka utaelewa kwa nini hii ni bora.
suala la ram
Moja ya kitu nilichopenda kwenye hii emulator ni kwamba unajikuna unapojifikia, kwanini nasema hivi?
Genymotion inakuruhusu kudownload virtual device zenye resolution tofauti na ram tofauti, kuna virtual device kama galaxy s3, s4, nexus zote, xperia nk inamaana unachagua simu halafu ndio inakuwa emulator.
Mimi pc yangu ina ram 3gb hivyo nikadownload virtual device ya galaxy s3 yenye ram 1gb inamaana emulator yangu itachukua 1gb of ram na kuniachia 2gb kwa ajili ya apps nyengine,
Mfano wewe pc yako ina 1gb of ram hivyo unaweza download simu ya zamani kama htc nexus one yenye 512mb of ram ili kuweza kuirun emulator vizuri.
Nafikiri nitakuwa nimeeleweka nikisema suala la ram unajikuna unapojifikia, wale wenye pc za zamani mnaweza kuidownload.
android version
tofauti na emulator nyengine genymotion unachagua version ya android unayotaka, kuanzia android za zamani kama 2.3 hadi android mpya kama 4.4.4 kitkat
kuflash mafile
emulator hii inakuja na rom ya aosp bila service za google, ila inaruhusu kuflash mafile just download mafile yako ya kuflash then drag&drop kwenye genymotion yatajiflash. niliflash google apps na arm libraly kwenye hii emulator bila shida.
root
usijali hii emulator tayari wameshairoot hivyo apps zako zote zinazohitaji root access zitafanya kazi.
user interface
muonekano wa genymotion ni kama wa simu tu, kila kitu kinafanana hivyo hutapata shida kuizoea.
pia upande wa kulia kuna navigation keys kama back, home, menu, battery icon, rotate screen na gps.
jinsi ya kuidownload
hakikisha una mb za kutosha kama unaieka hii emulator minimum mb300 ila zinaweza kuzidi pia.
-nenda website hii katengeneze account kisha download genymotion.
Genymotion
kuna vifurushi vitatu chagua kifurushi cha bure.
yenyewe ina around mb 120 utainstall genymotion pamoja na virtual box na driver zake, process yote hii ni automatic just fata maelekezo itakayokupa.
-open genymotion then utaona kuna option ya start na add, kwa kuwa hatuna virtual device click add halafu utaeka account yako uliotengeneza hapo juu zitakuja simu mbalimbali chagua simu kutokana na uwezo wa pc yako. ukichagua s4 wakati pc ni kimeo ujue haitakubali.
ukishachagua simu itadownload then utaweza kuplay virtual device yako.
kuieka genymotion kama simu
genymotion yenyewe ni aosp kuibadili iwe kama oha inabidi uflash google apps na ueke arm libraly hivi vitu utavipata hapa.
-google apps
https://goo.im/gapps
-arm libraly
Genymotion-ARM-Translation_v1.1.zip (8.96 MB) free instant download - FileTrip
jinsi ya kuflash just drag and drop kwenye emulator itakuuliza kama unataka kuflash then bonyeza yes.
pia hizo google apps zipo nyingi chagua inayoendana na version ya virtual device yako. mfano ulidownload s3 yenye jelly bean 4.1 basi google apps tafuta package ya jelly bean 4.1
i hope utaenjoy hii emulator kama una swali niulize.