Genge la vibaka kunduchi mtongani

dj-sulleh

Member
Jul 17, 2015
75
22
Ndugu zangu leo nimevamiwa na vibaka ofisini kwangu wakafanikiwa kumwibia mteja simu, begi na hela. Nilichofanya nimeripoti polisi kisha wakati tunarudi tukakutana na wale vibaka nikawaambia tafadhali rudisheni begi letu kusikia hivyo wakatoa mapanga na visu mimi nikatoa panga langu pia kukabiliana nalo kisha nikamwambia dogo akawaite polisi kwani kituo hakiko mbali huku mimi nikipiga kelele za wezi lakini hakutokea mtu na polisi wakamjibu dogo tutawakamata kesho.

Imagine niko mwenyewe nakabiliana na vibaka watano halafu polisi wanajibu tutawakamata kesho ilihali wako na vitu vyetu na bado wanakabiliana na mimi.

Jamani nimeshindwa hata kuelewa msaada wangu uko wapi kama polisi wananiachia soo mwenyewe na vibaka wakatokomea na begi simu na hela.
 
Ah..baadhi ya polisi michosho ndg yng ishawahi nikuta hyo hadi unahisi lao moja nn?
 
Ndugu zangu leo nimevamiwa na vibaka ofisini kwangu wakafanikiwa kumwibia mteja sim begi na hela nilichofanya nimeripoti polisi kisha wakati tunarudi tukakutana na wale vibaka nikawaambia tafadhali rudisheni begi letu kuskia hivyo wakatoa mapanga na visu mimi nakatoa panga langu pia kukabiliana nalo kisha nikammwambia dogo akawaite polisi kwani kituo hakiko mbali huku mm nikipiga kelele za wezi lakini hakutokea mtu na polisi wakamjib dogo tutawakamata kesho imagine niko mwenyewe nakabiliana na vibaka watano af polisi wanajib tutawakamata kesho ilihali wako na vitu vyetu na bado wanakabiliana na mimi
....jaman nimeshindwa hata kuelewa msaada wangu uko wapi kama polisi wananiachia soo mwenyewe na vibaka wakatokomea na begi sim na hela
Pole sana. Vibaka wanakera kweli. Ndo mtu akikuta kibaka amevishwa tairi unasaidia kukusanya kuni
 
Ndugu zangu leo nimevamiwa na vibaka ofisini kwangu wakafanikiwa kumwibia mteja sim begi na hela nilichofanya nimeripoti polisi kisha wakati tunarudi tukakutana na wale vibaka nikawaambia tafadhali rudisheni begi letu kuskia hivyo wakatoa mapanga na visu mimi nakatoa panga langu pia kukabiliana nalo kisha nikammwambia dogo akawaite polisi kwani kituo hakiko mbali huku mm nikipiga kelele za wezi lakini hakutokea mtu na polisi wakamjib dogo tutawakamata kesho imagine niko mwenyewe nakabiliana na vibaka watano af polisi wanajib tutawakamata kesho ilihali wako na vitu vyetu na bado wanakabiliana na mimi
....jaman nimeshindwa hata kuelewa msaada wangu uko wapi kama polisi wananiachia soo mwenyewe na vibaka wakatokomea na begi sim na hela
Ungemwambia dogo awaambie polisi kuwa “kuna brother wangu kada wa ccm anakabwa na vibaka” wangekuja fasta tu
Tatizo haujajiongeza
 
Dogo angesema polisi mwenzao anauawa na Vibaka huko, Ungeona kama wasingetoka kituo kizima wale waowao kwa wao wanbebana hawez kusikia mwenzao anafanyiwa tukio akapotezea au akakausha..
 
Siku hizi kuwaita polisi ni kutumia mbinu ;
1. Polisi mwenzenu anapigwa
2. Kuna mkutano wa Chadema
3. Kuna gari la magendo limeanguka
4. Kuna begi la pesa limeokotwa na kuna watu wanataka kutokomea nalo n.k.

Pole sana aisee
 
Ndugu zangu leo nimevamiwa na vibaka ofisini kwangu wakafanikiwa kumwibia mteja sim begi na hela nilichofanya nimeripoti polisi kisha wakati tunarudi tukakutana na wale vibaka nikawaambia tafadhali rudisheni begi letu kuskia hivyo wakatoa mapanga na visu mimi nakatoa panga langu pia kukabiliana nalo kisha nikammwambia dogo akawaite polisi kwani kituo hakiko mbali huku mm nikipiga kelele za wezi lakini hakutokea mtu na polisi wakamjib dogo tutawakamata kesho imagine niko mwenyewe nakabiliana na vibaka watano af polisi wanajib tutawakamata kesho ilihali wako na vitu vyetu na bado wanakabiliana na mimi
....jaman nimeshindwa hata kuelewa msaada wangu uko wapi kama polisi wananiachia soo mwenyewe na vibaka wakatokomea na begi sim na hela
Haaaaaa haaaaaaa nyie so ndiyo wale mlichoma moto kituo cha polisi enzi zile mkasema hamhitaji polisi tena mkajiona wajanja kweli .Sasa dhambi inawatafuna hasa maana hata mkiitaji hao polisi wanakuja kesho maana kituokituo kipo mbali magari yapo machache mmeletewa huduma karibu mkadharau .Haaaaa Mlifikiri mnazaa mitume manabii na malaika . Sasa shahawa zenu na maamuzi yenu yanawatesa.Naikumbuka ile siku nilikuwa Tarime naangalia ITV habari eti hawa watoto wa mamwinyi wa kizaramo na kindengereko wamechoma kituo cha polisi .Yaani huku kwetu ubabe ubabeni mguu wa shingo mguu wa roho kata shingo kata miguu bado hatuchomi kituo cha polisi Eti nyie mnaasira Kali .Hiyo dhambi itawatafuna sana Kugola Atakapowakumbuka.
 
Hatari sana... pole sana...

Polisi wa hicho kituo inaonekana wanapenda mambo ya theory (Uchunguzi)...

kwenye practical (Tukio halisi) wananywea...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom