Geita: Wananchi waliteketeza Lori baada ya dereva kumgonga na kufa papo hapo muuguzi wa zahanati ya Kaseme

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
FB_IMG_1520928285068.jpeg
FB_IMG_1520928273236.jpeg
FB_IMG_1520928278615.jpeg


Wananchi wenye hasira kali wamejichukulia sheria mkononi kwa kulichoma gari aina ya Lori baada ya dereva wake kumgonga na kufa papo hapo muuguzi wa zahanati ya Kaseme wilayani Geita.

Tukio hilo limetokea jana usiku katika Kijiji cha Kaseme wakati marehemu huyo akiwa katika bodaboda pamoja na watoto wake wawili, mmoja amefahamika kwa jina la Paulo Talafa mwenye miaka 3 na mwingine mchanga wa miezi miwili ambao wao wamenusurika na kifo hicho.

Mashuhuda wa tukio hilo wanasema Lori hilo lilikuwa kwenye mwendo mkali na walipojaribu kupishana na gari lingine ndipo likawagonga na mama huyo kuumia kuanzia sehemu ya kiuno hadi miguuni na kusababisha utumbo kutoka nje.

Wamesema sababu kubwa iliyochangia watoto hao kutopatwa na madhara kama mama yao ni kuwa alikuwa amewapakata kifuani ambako hawakuguswa na gari hilo.

Marehemu amefahamika kwa jina la Martha Paulo mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha maiti kwenye hospitali ya rufaa mkoani Geita.

Chanzo: Azam Tv
 
Inasikitisha sana kifo chake aisee. Apumzike kwa amani
 
Hapana mkuu ,wananchi hapo wangefanyaje???
mtu anaendesha kwa Kasi hovyo tu, na huyo dereva ni lazima atakuwa mwana ccm tu, maana hao ndo wanatembea na damu za watu
Yote kwa yote lakini wananchi hapo wamekosea aisee. Ni masikitiko kwa kifo chake. Lakini hii dhana ya kutofuata sheria mpaka unaona hata kwenye ngazi ya juu inavyotugharimu, hii mbaya sana.
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Wananchi inabidi waelimishwe kuhusu kuchukua sheria mikononi mwao,Hii ni hatari.Apumzike kwa amani marehemu.
 
Wananchi inabidi waelimishwe kuhusu kuchukua sheria mikononi mwao,Hii ni hatari.Apumzike kwa amani marehemu.
Hii ni mbaya sana ikiota mizizi. Naona hata ambaye anagongwa kwa kutokuwa makini mwenyewe kwenye kuvuka barabara hali itakuwa hivyo. Apumzike kwa amani
 
Ila akina mama bodaboda na uko na watoto mmmh ni hatari sana. Ijapokuwa madereva wa maroli wako speed lakini hili ni lakuwa na tahadhari nalo
 
Hapana mkuu ,wananchi hapo wangefanyaje???
mtu anaendesha kwa Kasi hovyo tu, na huyo dereva ni lazima atakuwa mwana ccm tu, maana hao ndo wanatembea na damu za watu
Roli halina kosa mwenye kosa ni dereva itakuwa haina maana kulichoma kisha kumwacha dereva. Kama halina Bima na ni Mkopo imekula kwake.
 
Back
Top Bottom