Geita kimenuka: Pinda asusiwa kikao!

Geita kimenuka: Pinda asusiwa kikao!

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Posts
4,225
Reaction score
869
Wakuu habarini za Usiku.

Taarifa rasmi zilizonifikia kutoka Mkoani Geita zinaeleza kuwa Waziri Mkuu amekumbana na kasheshe baada ya Waislamu kumsusia kikao na kuondoka,baada ya kukataa kutoa amri ya kuwaachia Waislamu sita wanaoshikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji ya Mchungaji.

Hata hivyo Waziri mkuu Mizengo Pinda amewaambia kwamba siku wakijisikia wako tayari kzungumza naye wamwambie atakwenda kuwasikiliza na kuzungmza nao kisha atatoa maelekezo ya nini kifanyike,kutokana na hali hiyo Waziri Mkuu amesema hawezi kutoa tamko lolote juu baada ya kuzungumza na upande mmoja wa Wakristo ambao walikubali kuzungumza nae.

Hata hivyo habari zilizopatikana kutoka ndani ya kikao hicho zimedai kuwa Lawama nyingi amesukumiwa Mkuu wa wilaya hiyo Omar Manzie Mangochie kwamba ndiye chanzo cha vurugu zilizotokea kutokana na yeye kuegemea upande mmoja wa waislamu.Hata hivyo tayari jana Waziri mkuu alitamka wazi jijini mwanza kwamba hakuna mwenye haki ya kuchinja kwa mujibu wa sheria za nchi isipokuwa ni suala la imani ya mtu.

Haya karibuni tujadili kwa pamoja hili.

UPDATE:
Feb 18, 2013
na Victor Eliud, Geita

JUHUDI za Waziri Mkuu za kutaka kutanzua mgogoro wa kidini wilayani Geita mkoani Geita kati ya Waislamu na Wakristo, zimegonga mwamba baada ya Waislamu kugoma kuendelea na kikao wakitaka wenzao waliokamatwa na kushtakiwa waachiwe.

Pinda aliwasili mkoani hapa ili kumaliza mgogoro huo ambao uliibuka wiki iliyopita na kusababisha kifo cha Mchungaji Mathayo Kachila (45) wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God katika eneo la Buseresere.

Mapema Mkuu wa Mkoa wa Geita, Said Magalula alimtambulisha Pinda na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye alikuwa akimwakilisha waziri wake, Dk. Emmanuel Nchimbi aliyelazimika kwenda Zanzibar kushughulikia tukio la kifo cha Padri Evarist Mushi.

Akizungumza kabla ya waandishi wa habari kutolewa nje ya kikao hicho, Pinda alisema kuwa tukio la Zanzibar linafanana na lile lililotokea Geita, na kwamba alikuwa hapo kutafuta suluhu.

Habari za ndani zilisema kuwa, wakati kikao hicho kikiendelea kati ya Pinda na viongozi hao wa dini zote mbili, mwakilishi kutoka upande wa Waislamu, Hamza Omar alisimama na kumweleza waziri mkuu kuwa yafaa wenzao waliokamatwa waachiwe kwanza, ili wawepo kwenye mazungumzo hayo. Hata hivyo, Pinda hakukubaliana na wazo hilo kwa ufafanuzi kuwa suala hilo kwa vile liko kisheria, aliomba mahakama iachiwe ifanye kazi yake.

Waziri Mkuu alifafanua kuwa bado watuhumiwa hao hawajatiwa hatiani kwa vile bado uchunguzi unaendelea, hivyo si utaratibu kuingilia uhuru wa mahakama. Msimamo huo ulipingwa vikali na wawakilishi wa Waislamu waliokuwa kikaoni hapo, na hivyo kunyanyuka na kuondoka ukumbini, hatua iliyomlazimu Pinda kuahirisha kikao hicho. "Utaratibu unabaki ule ule wa kuchinja, mazungumzo yameshindikana hadi siku nyingine baada ya Waislamu kugomea mazungumzo mpaka wenzao waliokamatwa Buseresere waachiwe," alisema Pinda.

Kabla ya Waislamu kutoka nje, Pinda alikuwa amekabirisha maoni kutoka pande zote mbili akianza na Wakristo, ambapo Askofu Musa Magwesela wa AICT alisimama na kumwomba kiongozi huyo atoe tamko kuhusu kuchinja.

"Sisi hapa hatuko tayari kula nyama iliyochinjwa na Waislamu kwa vile utaratibu huo hauko kisheria bali ni mazoea, hivyo tunakuomba Waziri Mkuu utoe tamko," alisema askofu huyo.

Katika vurugu hizo, mali za wananchi ziliharibiwa vibaya, huku baadhi ya maduka na bidhaa zikiteketezwa kwa moto. Miongoni mwa wananchi walioharibiwa mali zao ni pamoja na Mwenyekiti wa Bakwata Wilaya ya Chato na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Buseresere, Yusuf Idd Banana ambaye amezitaja mali zake zilizoharibiwa kuwa na thamani ya sh milioni 10.


Source: Tanzania Daima
 
Huko tunapoelekea inabidi kujenga mageraza za kutosha ili kuwaweka ndani wote wanouvunja sheria na kutishia amani.., Inabidi tuelewe kwamba imani na sheria ni vitu viwili tofauti.., na nchi inaendeshwa kwa sheria na sio imani.., Amini kivyako lakini usivunje sheria. Hii imesababishwa na serikali kuchekeana na wavunja sheria
 
Waislam walishawahi mwaka juzi kushinikiza muhalifu atolewa mahabusu bila masharti yeyote na akatolewa. Mpaka leo yuko huru.
Si ajabu na hao wauaji wakatolewa bila masharti.
 
Hivi nani alijua kwamba Geita ingekuwa kwenye front pages na mtafaruku wa kidini? Kuna sehemu zilizozoeleka kama Mwembechai, lakini Geita? Na hii inaonesha ni jinsi gani udini umesambaa. CCM mmetufikikisha pabaya sana.
 
Kama dini ni kukosa fikra bora nisiwe na dini. Sasa mtu ameua halafu mnashinikiza waachiwe. Childish

Mkuu hata usipokuwa nayo siku likinuka hata wewe utakuwepo tu,dawa hapa ni kuendelea kuomba sana kwa mungu ili aepushe aina yoyote ile ya chokochoko.
 
Kinuke tu...haya mashetani yatataka kutushika ------ baadae!
 
Kama Uislam ndo huo basi wataishia kupataja mbinguni, si hukumu ila ni mtazamo wangu tu! na naamini uvunjifu wa sheria kwa makusudi si mafundisho halisi ya KOROAN TUKUFU na wanaoendesha vitendo hivyo ni mbumbumbu wa kufikiri.
 
Watanzania mjilaumu wenyewe kwa matukio mabaya yanayoendelea nchini kwa sasa!! Serikali ya ccm haikuingia mstuni na kutwaa madaraka bali mliipa kura kwa ushabiki wenu wenyewe!!! Hiyo ndiyo kasi mpya... na ndiyo madhara ya kupiga kura kama vipofu!!
 
viongozi wa serekali waaangalie upya migogoro ya kidini na kubuni njia muwafaka ya kukabiliana nayo na kuwadhibiti wahalifu na wavunjaji amani na utulivu wa nchi,kuchelewa kutoa tamko katika baadhi ya matukio au kutumia nguvu ya dola kupita kiasi(nguvu haizalishi ila nguvu)itatupeleka kubaya
 
Nchi yetu ni ya kipekee saana, mtu katoa kauli ya kipuuzi na kwa kauli yake kaweka Amani ya nchi Rehani alafu mtu huyo bado yupo offisini bila wasi wasi! Uwajibikaji 0!
 
lakini tulisha ahidiwa nchi haitatawalika.. ndio hayo sasa.
 
Kumbe mkuu wa wilaya ni Mangochie? Huyu jamaa toka Mafia.
Mheshimiwa Rais tafadhali sana kuwa makini unapopeleka watu mikoani.
Wasukuma walikuwa si watu wa kujali nani mchinjaji.
 
Kumbe mkuu wa wilaya ni Mangochie? Huyu jamaa toka Mafia.
Mheshimiwa Rais tafadhali sana kuwa makini unapopeleka watu mikoani.
Wasukuma walikuwa si watu wa kujali nani mchinjaji.

Hii ni kwa Tanzania tu! Tuna kawaida ya kuangalia tulipoangukia na si tulipojikwaa.

Wale walikuwa wanapambana hivyo ilibidi tuangalie chanzo cha kufikia mapambano hayo, na nani mwanzilishi.
 
bado kuna haja kuwa makin ktk kuchagua viongoz wenye hekima japo naamini jamii huchagua kiongoz stahik kwa hekima zao. naamin hapa ange chinjwa shehe wangehitaji paka afufuliwe ndo wakae pa1. ningewashaul wakae mezan watoe tofaut na wazuie jambo hili lisijirudie. cku moja inaweza kutokea hata kwa kumpoteza mwanae kwa sababu zinazoweza kuzuirika
 
Back
Top Bottom