Geita hatuna mbunge

Geita hatuna mbunge

Kifai

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
816
Reaction score
174
Toka kachaguliwa huyu bwana Donald Max ambaye ni mbunge wa Geita mjini is equal 0....!

Kana kwamba hatuna mbunge, hajawahi kuweka mkutano na wananchi wake na kuwaeleza mipango na mikakati katika jimbo kuhusu maendeleo, zaidi kikubwa amekuwa akionekana sehemu mbalimbali za kujirusha na vimwana mbalimbali.

Nashukuru kura yangu ilipotelea upinzani, naitamani sana 2015 sababu wana Geita washajifunza kitu.
 
Unashangaa nini Mbona Nchi haina Rais!!!Magamba lengo lao ni kuwatumia kama kondomu wakishapata walichikihitaji wanawatupilia mbaliii subirini 2015 mumuadhibu
 
Muanzishieni M4C huko huko. Mumfundishe adabu.
nijuavyo mimi mkoa mzima wa Geita hauna Mbunge. Hata pale Chato kuna usanii tu na maigizo!
mkijipanga vizuri mtawaondolea mbali hao!
 
Tatizo ni kwamba watz wanashawishika na vitu vidogo sana kabla ya kutoa kura zao. Max alipanda majani Geita mjini karibu na ofisi za ccm na kuanzisha vijiwe viwili vya kahawa kimoja karibu na soko kuu na kingine general tyre na kuwevikea tv, hapo watu wa Geita wakamuona huyu ndiye anaefaa kuwa mbunge. Wacha sasa wajute na kutafuna hayo majani aliyowapandia kama rushwa ya kutafuta ubunge.
 
Toka kachaguliwa huyu bwana max ambae ni mbunge wa geita mjini is equal 0....! kana kwamba hatuna mbunge, hajawai kuweka mkutano na wananchi wake na kuwaeleza mipango na mikakati katika jimbo kuhusu maendeleo, zaidi kikubwa amekuwa akionekana sehemu mbalimbali za kujirusha na vimwana mbalimbali, nashukuru kura yangu ilipotelea upinzani, naitamani sana 2015 cause wana geita washajifunza kitu

Wacha muipate kisawasawa na sasa mtambue sio kila king'aacho ni dhahabu, na pia tambua majuto ni mjukuu.
 
Tatizo ni kwamba watz wanashawishika na vitu vidogo sana kabla ya kutoa kura zao. Max alipanda majani Geita mjini karibu na ofisi za ccm na kuanzisha vijiwe viwili vya kahawa kimoja karibu na soko kuu na kingine general tyre na kuwevikea tv, hapo watu wa Geita wakamuona huyu ndiye anaefaa kuwa mbunge. Wacha sasa wajute na kutafuna hayo majani aliyowapandia kama rushwa ya kutafuta ubunge.

Kwani tumekuwa ng'ombe au mbuzi hadi tule majani? Acha kututukana bhana?! Kutenda kosa sio kosa bali kurudia kosa, tumejifunza 2015 hatutafanya makosa.
 
Muanzishieni M4C huko huko. Mumfundishe adabu.
nijuavyo mimi mkoa mzima wa Geita hauna Mbunge. Hata pale Chato kuna usanii tu na maigizo!
mkijipanga vizuri mtawaondolea mbali hao!

Kaka liko jembe moja katika mkoa huu mpya linaitwa KULIKOYELA KANALWANDA KAHIGI!
 
Hakuna maji, umeme kwa cku unapatikana masaa 2 masaa mengine 10 umeme umekatika, kweli hii ndo geita ya wawekezaji wa kikaburu
 
Kaka liko jembe moja katika mkoa huu mpya linaitwa KULIKOYELA KANALWANDA KAHIGI!

Prof huyo naye anadaiwa hajafanya chochote kwa wanaBukombe, wamekata naye tamaa....siasa mchezo mgumu sana
 
Matatizo ya kupokea Kanga na Kofia hadi wanaume wanashonewa Makoti.
 
People in Geita...actually at one time I was a resident in that place na nilimshuhudia huyu Mbunge wa sasa akishindwa kura za maoni mwaka 2010 na watu wa Geita mjini walikuwa wakimtaka sana kisa kawajengea Public Toilet na Kijigarden cha ovyo ovyo.Its time to pay a price coz mlinunuliwa kwa vitu cheap sasa mnalipa Gharama kubwa na nasikia jamaa anajitapa kuwa ni pesa zake ndizo zilimpa Ubunge na kutukana wa tu wanaomfuata kuongelea maendeleo ya Jimbo
 
Siku moja tulikua tunakunywa nae pale Kisabo Hotel, alisikika hivi, "Kijana kama wewe nikikuona unapenda ccm nakushangaa sana, nakuona kama huna akili, hivi sisi wabunge wa ccm hua hatuoni hata tukiwa Bungeni, hatujadiri mambo ya maendeleo, sisi ni chama tu!" Siku nyingine tena aliwahi kusema hivi, "Mimi mwaka 2015 sitagombea tena Ubunge, umri wangu umeisha enda, lakini nyie wana Geita mnadai eti siwatetei, siku ninaapishwa niliambiwa nifunge mdomo wangu Geita ni shamba la Ikulu, sasa niwatete nini" Sijawahi kurudi tena huko Geita, nilikwenda kikazi na nikakutana na Classmate wangu then akanipeleka hapo hotelini kupata moja baridi moja moto, ila hayo ndio niliyasikia toka kwake, mara nyingi mtu akilewa hua anasema kitu ambacho hawezi kusema akiwa mzima, ila huyo ndio Maximilian Donald, mbunge wa Geita, kazi ni kwenu wazee wa madini!
 
Hayo matatizo kama ya Ubungo kiongozi
Hakuna maji, umeme kwa cku unapatikana masaa 2 masaa mengine 10 umeme umekatika, kweli hii ndo geita ya wawekezaji wa kikaburu
 
People in Geita...actually at one time I was a resident in that place na nilimshuhudia huyu Mbunge wa sasa akishindwa kura za maoni mwaka 2010 na watu wa Geita mjini walikuwa wakimtaka sana kisa kawajengea Public Toilet na Kijigarden cha ovyo ovyo.Its time to pay a price coz mlinunuliwa kwa vitu cheap sasa mnalipa Gharama kubwa na nasikia jamaa anajitapa kuwa ni pesa zake ndizo zilimpa Ubunge na kutukana wa tu wanaomfuata kuongelea maendeleo ya Jimbo

Mkuu Mutasingwa Wayne, hili ndilo tatizo la watu kutegemea mbunge alete maendeleo kwa kutumia pesa yake ya mfukoni badala ya kuibana Serikali ilete maendeleo. Kama katumia pesa yake kuleta maendeleo, ina maana amewekeza, akipata ubunge itabidi arudishe pesa yake.
 
Last edited by a moderator:
Atafanya nini iwapo aliambiwa na Magamba afunge domo lake kwa 7bu Geita ina "Machimbo ya Chama"!
 
Mkuu Mutasingwa Wayne, hili ndilo tatizo la watu kutegemea mbunge alete maendeleo kwa kutumia pesa yake ya mfukoni badala ya kuibana Serikali ilete maendeleo. Kama katumia pesa yake kuleta maendeleo, ina maana amewekeza, akipata ubunge itabidi arudishe pesa yake.

Mkuu Sawabho hili ndio tatizo linalifanya Bunge letu liwe la kibiashara zaidi zaidi ya hoja..yaani mwenye pes ndiye anayestahili ubunge.Kuna rafiki yangu msomi mzuri na msomi mwenye track record nzuri ya utumishi wa umma amekwenda kutangaza nia kipindi hiki cha Krismas iliyopita akaulizwa ana milioni 200?Amerudi amekata tamaa anasema hataki tena mambo haya.
 
Back
Top Bottom