Hadrianus
JF-Expert Member
- Feb 19, 2020
- 2,112
- 5,208
Ukizoea vya kunyonga...
Baada ya kusota kwa muda mrefu wakiwa Ligi daraja la kwanza hatimaye wakapanda Ligi kuu Tanzania bara maarufu kama NBC PREMIER LEAGUE (Ligi yetu kivyetu vyetu).
Misimu waliyocheza Ligi daraja la kwanza Geita Gold FC walitumia viwanja viwili, kimoja ni cha Shule ya wavulana WAJA na cha pili ni kiwanja cha shule ya sekondari ya wasichana Nyankumbu iliyojengwa kwa udhamini mnono wa GGML (ila upigaji ukawa mkubwa shule ikajengwa tofauti na matarajio si unajua wabongo tena).
Geita Gold FC wakiwa wanatumia uwanja wa shule ya wasichana Nyankumbu, hawakuwahi kupoteza mechi yoyote pale hivyo kupelekea kupaita "Machinjioni".
Kama unakumbuka lile sakata la Geita Gold, Jkt Kanembwa, Polisi Tabora & Jkt Oljoro kushushwa daraja kwa kosa la upangaji matokeo, leo nataka nikupe kisa kwanini wanahangaika kupata matokeo ya ushindi katika michezo ya Ligi kuu hadi kupelekea kumtimua mapema kabisa Ettiene Ndayiragije.
Hawa wakauitwa Geita Gold FC mwanzo walikua wanadhaminiwa vizuri na mgodi wa GGML, jamaa walimwaga pesa za kutosha ili timu isajili, inunue usafiri wake, ilipe vizuri wachezaji hatimaye ipande Ligi kuu.
Kama unavowajua wabongo zile "noti" zikatumiwa vibaya, wakanunua usafiri wa bei rahisi ili wapate pa kupiga, kwa kifupi pesa hazikutumika ipasavyo mbaya zaidi walianza kununua mechi na marefarii.
Geita Gold kila walipokua wanacheza mechi pale Nyankumbu, wanahonga waamuzi ili kuwaminya wapinzani ili mradi wao washinde mechi, mfano unakuta mshambuliaji wa timu pinzani kila akipigiwa pasi, mwamuzi wa pembeni ananyoosha kibendera kwamba ni offside hata kama hajaotea.
Baada ya kashfa hizo za upangaji matokeo na hatimae kushushwa Daraja, GGML walijiondoa kuidhamini timu hiyo na Halmashauri ikaichukua na kukomaa nayo hatimaye ikapanda Ligi Kuu (Ligi daraja la kwanza mipango ni mingi kuliko mpira).
Mashabiki wa Geita Gold FC kumbukeni kwamba mnapolalamika kua timu yenu haipati matokeo mazuri nyumbani ni kwasababu zamani mlikua mnabebwa kwa nguvu, mnashinda kwa ubabe, mfano mechi ile ya JKT Oljoro mchezaji anashika mpira nje ya 18 refa anatenga tuta, mchezaji anapiga penat, kipa anatoa refa anasema penati irudiwe, pakazuka ugomvi mkubwa sana na refa akapigwa ngumi za kutosha.
Nasikitika Wallace Karia ulipoenda kuomba "indosimenti" mkoani Geita viongozi wakakupa masharti kuwa uwanja wa Nyankumbu utumike kuchezewa michezo ya Ligi Kuu ili hali uwanja haukidhi vigezo hata nusu (pichi yake nyasi ni ngumu sana), viongozi wakaomba mechi zao dhidi ya timu kubwa za Dar es Salaam zipangwe mzunguko wa pili na kweli imekua hivyo.
Geita Gold mliuza wafungaji kidogo walikua wanajitahidi mkaenda kusajili wachezaji wabovu kama GEORGE MPOLE na DANY LYANGA mkitegemea mtabaki Ligi kuu? (Hapana lazima mshuke daraja).
Mkamleta Ettiene Ndayiragije ndani ya mechi 4 mmefukuza, mlitegemea awafunge Namungo, Yanga, Mtibwa & Mbeya City? (Lazima mrudi mlikotoka).
Huku Ligi Kuu vyakunyonga havipo, huku kuna kunyongwa tu.
Hali kama yenu ndiyo aliyopitia Gwambina, alinunua mechi, akawa anatembea na marefa kila mechi ni hao hao tu hawabadiliki leo hii Gwambina wako wapi?
Mtarudi mlikotokaaa.
Mlizoea vya kunyonga.
NB: Ligi yetu inatimu nyingi nzuri zinacheza mpira mzuri sana, ila tatizo ni viwanja vingi.
havifai kuchezewa mechi.