Geita: Baba ambaka mtoto wake wa miaka 4

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
GEITA JESHI la Polisi mkoani Geita linamshikilia mkazi wa Kata ya Nyankumbu, Selemani Mathis (35), kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake (jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka minne.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo, alisema mtuhumiwa huyo yuko rumande akisubiri uchunguzi tuhuma dhidi yake ukamilike ili aweze kufikishwa mahakamani.

Mtoto huyo alikuwa akiishi na baba yake baada ya mama yake kutengana na baba yake na kumwacha mtoto huyo na mdogo wake wa miaka miwili
 
Hizi habari za ubakaji watoto ni utata mtupu, mtu mzima awezaje kumuingilia mtoto wa miaka minne maungoni mwake? Kwanza maungo ya mtoto ni madogo, pili baba mtu mzima anaweza vipi kumuingilia mtoto wake wa kumzaa kama si vitendo vya imani za kishirikina?
 
Kubaka ni kumuingilia mwanamke kingono kinyume na hiyari yake mtoto wa miaka 4 hana hiyari katika jambo hilo kwa hiyo AMENAJISIWA
 
Daah! Mbaya sana hiyo.

Pia nawaza tu kwa nini huyo mama akaacha wanawe wakiwa wadogo kiasi hicho bila kuondoka nao.
 
Back
Top Bottom