Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Baada ya mdau kuweka uzi hapa jukwaani, akihoji ukimya wa TFS na Jeshi la Polisi juu ya mauaji yaliyofanywa na askari hao kwenye pori la uhifadhi (Kwa maelezo ya tukio hilo ingia hapa: DOKEZO - GEITA: Kuna Kijana ameuawa kwa kupigwa risasi na Askari wa Hifadhi ya Pori la Kigosi, TFS na Jeshi la Polisi mbona mpo kimya?), Jeshi la Polisi limetoa ufafanuzi juu ya hatua iliyochokuliwa kwenye tukio hilo:
=====
TAARIFA KWA UMMA
ASKARI WANNE WA JESHI LA UHIFADHI (JESHI USU) WASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI
Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linawashikilia Askari wanne wa Jeshi la Uhifadhi (JESHI USU) kwa tuhuma za mauaji ya Eziboni Fikiri (20), Mkulima, Mkazi wa Kijiji cha Msonga, Wilaya ya Bukombe.
Tukio hili la mauaji limetokea Agosti 13, 2025 majira ya saa 12:00 asubuhi katika eneo la Pori la Hifadhi ya Kigosi, Wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita wakati Askari hao wakitekeleza jukumu la ukamataji watu waliokuwa wameingia hifadhini na kukata miti kinyume cha sheria.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Bukombe kwa ajili ya uchunguzi wa kitaalamu. Watuhumiwa wanahojiwa na uchunguzi utakapokamilika watafikishwa Mahakamani.
Jeshi la Polisi linawaomba wananchi kuwa watulivu wakati uchunguzi wa tukio hili unaoendelea kufanyika ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria.
Imetolewa na:
Kaimu Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Geita