GE2025 Geho: ADA TADEA hawana fedha za kuanza kampeni

GE2025 Geho: ADA TADEA hawana fedha za kuanza kampeni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Ikiwa ni takribani siku nane tangu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ifungue rasmi dirisha la kampeni za Udiwani, Ubunge na Urais, Chama cha ADA TADEA mkoani Ruvuma bado hakijaanza rasmi kampeni zake kutokana na hali ngumu ya ukata wa fedha.

Akizungumza na TVE Habari, Katibu wa ADA TADEA Jimbo la Songea Mjini, Paulo Geho, amesema chama hicho kimefanikiwa kusimamisha wagombea katika kata 4 kati ya 21 pamoja na mgombea wa nafasi ya Ubunge, lakini uhaba wa rasilimali umekuwa changamoto kubwa.

Geho ameongeza kuwa ukosefu wa fedha unakwamisha ushindani wa haki kisiasa, na hivyo ametoa wito kwa Bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuangalia upya sheria ya ruzuku kwa vyama vya siasa, ili kuimarisha usawa wa kisiasa na demokrasia shirikishi.

Kwa upande wake, Anna Kapinga, mgombea wa Ubunge kupitia ADA TADEA katika Jimbo la Songea Mjini, amesema licha ya changamoto hizo, bado wamejipanga kwa bidii kuhakikisha wanawafikia wananchi wote kwa njia mbalimbali.
 
Back
Top Bottom