Gbagbo awataka askari wa UN waondoke Ivory Coast

Gbagbo awataka askari wa UN waondoke Ivory Coast

KAMA Gbagbo hakuwa tayari kuondoka madarakani, kwa nini aliruhusu kura ipigwa? Haya ndo tunayaona hapa Tz wakati wa uchaguzi uliopita na sasa kwenye mchakato wa Mameya! Hiyana hiaya hiaya! Watu wengine hudhani watatawala milele, wamezaliwa kutawala daima! What a shame

Shame on You Gbagbo na wanaokuhusudu wote ndani na nje ya Ivory Coast

Wa-Tz wenzango, nina amini kuwa swala la Ivory Coast hatulijui vizuri. Tunaweza kueleza kwa uzuri tatizo la Tz na pengine Kenya zaidi kuliko nchi ya Ivory Coast, a francophone country in west Africa. lakini wengi tunaojitokeza kulisemea tunakuwa kama tunapoteza tu muda wetu.

Mimi ninaye jamaa hapa anatoa maelezo hadi machozi yanamtoka jinsi wa-France wailivyoikalia kooni nchi hiyo kwa miaka mingi. Shida ya wa-Faransa ni kuwa kumbe Ivory Coast ni shamba lao linalotegemeza uchumi wa nchi ya France kwa miaka mingi. Kosa la Gbagbo ni kukataa %-ge ya mauzo ya cocoa kwenda France kama mkataba wao ulivyo. Nasikia karibu nchi zote zilizokuwa chini ya koloni la ki-Faransa walikuwa na mkataba wa jinsi hiyo. Hilo pia ndio chanzo cha Rwanda kufarakana na colonial master wake few years ago.

Huyo Quattara ni pandikizi tu, na tena si raia wa Ivory Coast. Katiba ilipobadilishwa kuzuia mtu asiye raia kugombea uongozi ndio vurugu zilizotokea (kama tunakumbuka). Rais wa Africa Kusini Mr Thabo Mbeki ndiye aliyekwenda kupendekeza kuwa ili kupunguza mgogoro wa uasi amruhusu Quattara, japo kinyume cha sheria, awe miongoni mwa wagombea wa urais. Na hivyo ndivyo ilivyofanyika, lakini Gbagbo ni maarufu, isingewezekana kuanguka kwa kura, hivyo mkakati wa kumteka Mwenyekiti wa Electoral Commission na kumshinikiza kutangaza kuwa Quattara ndiye mshindi. Lakini ukweli ni kuwa Quattara si mshindi na hata hakukaribia kushinda.

Kwa kifupi tu ni kwamba wale ambao mko interested kujua ukweli wa swala hilo fanyeni uchunguzi kwanza ndio muweze kutoa maoni yenu. Wakati mwingine inachosha kusoma maelezo ya mtu mwenye hisia kali lakini hana ukweli wowote juu ya tatizo.

Hao UN ambao kimsingi ni wa-Faransa chini ya kivuli cha UN ndio wanasababisha matatizo na kwahiyo uamuzi wa kuwafukuza ni kutafuta amani ya nchi hiyo na sio kung'ang'ania madarakani. Sasa UN wamekataa kuondoka, maana yake Ivory Coast haiko huru.
 
Mnaonaje JK akimuunga mkono Gbagbo, si mnajua Tanzania lazima iwe upande wa Africa kujiamria mambo yake. Msisaau wosia tuliopewa na Mwongozo unaosemekana uliandikwa na Ngombale Mwiru, wakati uliposemakuwa; " kitendo chochote kinachompa mtu kuamua mambo yake ni kitendo cha maendeleo hata kama akitoi shibe".
 
Back
Top Bottom