Prince si wa kwanza kunena ufujaji wa Fedha M4C wapo pia Kama Nyimbo aliyekipa mgongo Chama hiki hivi karibuni. WanaJF tafadhari tajeni na wengine. Ila mimi naamini siku si Nyingi watashikana Mashati kugombea ulaji wa Fedha na hapo ndo Siri zaidi zitakapofumka. CDM ndo inakwenda hivyo ifikapo 2014 itakuwa hoi bini taabaniGazeti la RAI limeshambulia vikali chama cha CDM kwa kile lilichodai kufuja pesa ovyo kwa operesheni M4C huku chama hicho kikishindwa vibaya kwenye uchaguzi wa madiwani.
Gazeti hilo limedai matokeo hayo ya Chadema hayaridhishi kabisa wananchi ikilinganishwa na nguvu kubwa iliyotumiwa na chama hicho.
Matokeo ya udiwani yanaonyesha mgawanyo wa viti ulikuwa CCM 22 CDM 5 TLP 1 CUF 1.Hata hivyo CDM ikifanikiwa kurejesha viti vyake 2 huku ikiinyanganya CCM viti 3.
My Take:
Gazeti la RAI miezi iliyopita lilikuwa limeanza kurudu katika ramani yake kwa kutoa habari bila upendeleo lakini tangu Prince Bagenda aajiriwe kama Mhariri Mkuu amekuwa na chuki kubwa dhidi ya chama cha CDM na habari za gazeti hilo kila wiki zimekuwa zikikishambulia vikali chama hicho.Pia tangu Bagenda aajiriwe kumekuwa na makala maalum kila wiki za kushambulia viongozi wa chama hicho hasa Mkiti Freeman Mbowe n Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa.Hata hivyo soko la gazeti hilo kwa sasa tangu aajiriwe Bagenda limeporomoka vibaya sana.
Huyu jamaa alikuwa na jenerali ulimwengu ,salva rweyemamu, Padri privatus karugendo ,muhingo na wengine tu enzi za gazeti la rai .
Baada ya kuuzwa wananunuzi wakafikri na waandishi akili zao pia wamezinunua ,jamaa wakaachia gazeti wakaanzisha raia mwema vichwa vyote vikahama.
Isipokuwa Prince Bagenda aliyepewa jukumu la kuandika makombora enzi za mh.Kikwete baada ya ushindi Salva Rweyemam akapewa mwandishi wa rais,Bagenda ama misimamo yake ama hulka yake akaachwa,wenzie wote wakahamia gazeti la raia mwema.
Bagenda nampenda namheshimu ila ana udhaifu wake anatumiwa ana misimamo mikali akishika kalamu akakaa chini kama uko ofisini utatafuta pa kutokea ,kumbukeni enzi za gazeti la rai kipindi cha mkapa ,ila cha muhimu shujaa mmoja akipotea huzaliwa wengine .mwanahalisi ikazaliwa.
fmpiganaji, hili gazeti haliwezi hata siku moja kuiandika vizuri CDM kwa sababu ndio waliomfanya bosi wao ajiuzuru ubunge wa Igunga. Lakini pia 'Profesa' J. aliimba "ili nifanikiwe ninahitaji marafiki, ili nifanikiwe zaidi nahitaji maadui. Maadui wa CDM wamekuwa wakitoa mchango mkubwa sana (japo bila kulitambua hilo). M4C inatesa watu wengi sana, kwa kuona haraka unaweza kuona kuwa haijafanya kitu, ila kiukweli kuna kitu kikubwa sana kimefanyika, Vijana ambao bado wamenyimwa haki yao ya kupiga kura ni wangapi katika hizo kata, uandikishaji ulifanyika 2010. Siumizwi na wakala wa NYINYIEM (RAI) ila ni kuongeza umakini ktk M4C inayofuata.
Mungu wangu kweli dunia haina haki hivi kweli kwenyeuteuzi wa wakuu wa mkoa amekusahahu,wa wilaya pia?jitahidi mwanangu akina nepi wanakusoma wanaweza wakakupendekezaNimelinunua gazeti la Rai, na nimelisoma lote lakini sijaona sehemu yoyote limeishambulia Chadema. Rai limeandika Chadema wamepata viti 5 vya Udiwani, CCM wamepata viti 22 vya Udiwani...sasa hapo kuna kosa gani.
Kweli upenzi unawasumbua na utakiangamiza chama chenu huku mnakiona! Badala ya kujadili hoja mnajadili mtu. Hivi ni watu gani nyie ambao mnaamini kwamba mko perfect? There is only one perfect being.
Nimelinunua gazeti la Rai, na nimelisoma lote lakini sijaona sehemu yoyote limeishambulia Chadema. Rai limeandika Chadema wamepata viti 5 vya Udiwani, CCM wamepata viti 22 vya Udiwani...sasa hapo kuna kosa gani.
CCM Kata 22=kura 29 000
CHADEMA Kata 5=kura 28 800