Gazeti RAI laishambulia CHADEMA

Udaku gani Rai wameandika? Hivi kuandika Chadema wamepata viti 5 ndio udaku?

Hawa jamaa vichekesho kweli. Eti tusubiri 2015! Sasa dalili ya vua si ni mawingu? Kama kwenye viti 29 wanapata 17% ilikuwa wakae chini wajiulize. Au watatoa wapiga kura Kenya?!
 
Serikali tunaomba mtupatie haki yetu ya kupata habari,lifungulieni Mwanahalisi) kwa nini mnatuonea?
 
M4C nimeiona inavyofanya kazi mikoani mpaka ulaya matunda yake tumeyaona imezaa kata 3.

Kumbe unakiri...imezaa kata 3 ...au kwa lugha nyingine CCM imenyanganywa kata 3.Kalaghabaho.
 
Siku zote ukikubali kusifiwa basi ukubali pia na kukashifiwa. Zote ni sehemu ya maisha.

lakin kwa upande wa habari, unapewa nafasi kujibu hoja hizo na kutolewa kwa wananchi kujua ukweli upo wapi na si kujificha chooni na kulalama.
 
Kada Maarufu Wa CCM Prince Bagenda ameanza Rasimi Kazi ya Kuua chadema na kumujenga Lowasa.
Waandishi wote Wenye mwelekeo wa Kuunga mkono Mageuzi wameminywa na amewaleta Waandishi wa zamani kutoka gazeti la Taifa Tanzania lilikuwa linamlinda Nazir Karamagi.

Mpango huu una andaliwa kutumia gazt La TAZAMA , Sauti Huru kwa malengo ya kulinda Mtandao Wa Lowasa

Waandishi walipangwa kwenye mkakati huo ni pamoja na

1.Brayceson Kayungilo aliyekuwa Taifa Tanzania
2.Julius Mapunda Kutoka TAZAMA
3.Esbon Kagya Kutoka Taifa Tanzania


Ukiangalia gazeti la RAI leo mtandao huo umeonyesha Uandishi wa Chuki na Ushabiki wa Kisiasa wenye lengo la kupotosha umma na Kumulinda Lowassa
 
-Hao jamaa huwa wanafanya propaganda za kizamani sana
Naamini turnover ya kampuni ni negative kwa kufanya kazi kwa hasara

Siku hizi wameshajua CHADEMA ndiyo habari ya mjini ni lazima watumie siku nzima kutafuta headline inayogusa chadema.Ni turn over boosting strategy
 
CDM WALIKUWA wanajitangaza kwa ajili ya kukijenga chama kwa ajili ya 2015.pia gazeti lingebainisha ni shilingi ngapi kila chama kimetumia.huwezi ukasema wapinzani wanapoteza pesa bure kwenye kampen kama za udiwan.wao ndiyo shughuli yao kuu,kujinadi.wanaopoteza pesa bure ni chama tawala ambao walitakiwa kutumia pesa hiyo kutekeleza ilani yao ya uchaguzi
 
Nimelinunua gazeti la Rai, na nimelisoma lote lakini sijaona sehemu yoyote limeishambulia Chadema. Rai limeandika Chadema wamepata viti 5 vya Udiwani, CCM wamepata viti 22 vya Udiwani...sasa hapo kuna kosa gani.

hehehe.. mkuu pro cdm hawataki kusikia habari yoyote mbaya kuhusu CDM hata kama ni ukweli..
 

Kuchukua viti 3 vya CCm ni mafanikio tosha kabisa.

Hapo wakusikitika ni CCM ambao wamenyanganywa viti 3. Na endapo wakiendelea hivi CDM mwaka 2015 watapata viti vingi sana.



MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 

Dawa ndogo tu; kutolinunua. MIMI NILISHALIGUNDUA NA SITAMANI HATA KULISOMA, KAMA NILIVYOISUSIA TBC
 
Kwani tatizo liko wapi ..si limeandikwa ukweli mtupu... Jinsi cdm inavyojinadi na ilivyofanya kampeni chini ya mbowe na babu slaa haikustahili matokeo hayo... Ni jibu jepesi tu kuwa cdm bado hakikubaliki katika tz kipo moshi arusha na mwanza kidogo... Na ukweli kuwa cdm inawafuasi wa mikutano haina wapiga kura
 

heri yako umekuwa makini na wa unesha umma we umekomaa kifikira si mtu wa kukurupuka na kuropoka big up. Tunaiangalia input na out put kaka umeeleweka. Walopokaji achanana nao
 
Hivi kumbe bado linauzwa,Ndio kwanza na jua leo.I think limejifia.
 
Hata kama ukitumia HCL ACID & NITRIC ACID huwezi kumtakatisha huyu, anamagamba magamba magumu sana.
 

Akili kubwa sana hizi,naunga mkono hoja mia kwa mia...huwezi kuwa na shilingi mia ukaporwa thelathini halafu ukaenda mtaani ukipiga kelele kwa majigambo kama zuzu lazima utakuwa mwehu tu....M4C ni kiboko yao na bado itawanyuka sana.
 
Rai,Mwananchi,Jamhuri yote hayana hoja hayana tofauti na kiu na sani na ijumaa udaku mtupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…