"Nilikwenda kumsikiliza (Dr slaa) pale Mwembetogwa na muda wote aliohutubia nilizingatia sana dakika alizotumia. Alizungumza kwa dakika 50 ambazo hata hivyo alitumia zaidi dakika 40 kuwashambulia watu akiwemo Rais kikwete, mkewe mama salma, mtoto wao Ridhiwani Kikwete, Mnadhimu mkuu wa jeshi la wananchi, polisi pamoja na idara ya usalama wa Taifa. Dakika nyingine kama tatu au nne alizitumia kumtambulisha mchumba wake, Josephine na kisha aliongelea sera kwa takribani dakika tatu akaanza kuwatambulisha wagombea wa viti vya udiwani wa chama chake na mgombea ubunge".