Mkuu kutoka na habari zilizo andikwa kwenye gazeti hilo siyo rahisi kulipata ukissubiri ifike saa saba soma online lakini lilikuwepo...Gazeti letu maarufu la Tanzania daima sijaliona kwa muda wa siku mbili yaani jana na leo. Jana sikulipata mitaa niliyotembelea,mbezi,ubungo,posta na mwenge. Leo pia sijalipata mitaani mbezi,ubungo,kariakoo na ubungo. Kuna nini kimelisibu hili gazeti maarufu hapa nchini?. Lisipokuwepo gazeti la magamba a.k.a uhuru litatamalaki kwa propaganda zake bila kujibiwa. Je vipi huko mtaani kwako umeliona tanzania daima? Tupeane taarifa!
Mimi nalipata mtandaoni. Nadhani labda linauzika sana kiasi ambacho halibaki, au kuna watu wanayanunua yote ili yasisomwe.
Tanzania Daima - Sauti ya Watu
Habari zinazo andikwa nyingi huwa mwiba kwa serikali na viongozi wake, hivi karibu habari za mtekaji wa Ulimboka zilivyo fululiza, na hii ya Jk kukaliwa kushatkiwa kwa umoja wa mataifa nazo sio habari nzuri sana kwa magamba!