hah, bila kusahau kuwashia moto asubui....na tukiochukua tunapeleka gereji kubandika kwenye gari wakati tinapulizia rangi maana ni pana...
Mtachonga wee. Tanzania Daima litakufa kama Mfanyakazi na Shaba. Udaku haudumu
Mara nyingi huwa nanunua magazeti asubuhi na ninanunua mwananchi, Tanzania Daima na mara chache Nipashe na Mtanzania...Sasa Leo nilichelewa sana kununua magazeti kwani nilichelewa kutoka kanisani na nikapitia kwenye majukumu mengine....
Nilipofika kwa muuza magazeti (around saa 9 alasiri) nikakuta kuna copy moja tu ya Tanzania Daima nikaimalizia....Muuza magazeti akaniambia alikuwa na copies 100 na nililochukua copy ya mwisho ila kwa upande wa gazeti la Mzalendo alikuwa na copies 5 tu lakini mpaka wakati huo zilikuwa zimenunuliwa copies tatu tu !
Watu wanaomini propaganda za CCM kupitia magazeti yao ni wachache sana.......Watu wengi, wanacheza tune ya mabadiliko !
Jamaa yangu alikua na pc 100 za mzalendo kazimaliza zote!
Labda kama alichambia
Utafiti mwananchi na Tanzania daima ndio magazeti yanayonunuliwa kwa wingi sana kila siku
....na tukiochukua tunapeleka gereji kubandika kwenye gari wakati tinapulizia rangi maana ni pana...
Mtachonga wee. Tanzania Daima litakufa kama Mfanyakazi na Shaba. Udaku haudumu
yes mkuu....saa 7 hukuti mwananchi Na tz daima
Mwananchi walitaka kujichanganya kipindi cha nyuma kwa kuandika habari za kuifagilia ccm gazeti lao likaanza kudoda,walikula hasara sana wakaona isiwe tabu waendane na mabadiliko wanayotaka wananchi ndo sasa wanauza sana gazeti lao na wamekoma kabisa kuandika propaganda za ccm maana ilibaki kidogo tu mwananchi litoweke mitaani,amini usiamini,magazeti ya serikali yote yana survive tu kwa kuwa yana ruzuku kubwa sana lakini ingekuwa yanajiendesha menyewe kwa kutegemea mauzo yangekuwa yameshatoweka yote,serikali imeamua kuyachapisha kwa gharama zake japokuwa inakula hasara ili kuepuka fedheha kubwa,huwa hayanunuliki hata wana ccm wenyewe wananunua magazeti ya mabadiliko.
Mimi nanunua sana gazeti la mzalendo kwa ajili ya ufugaji wavifaranga. Hilo gazeti huwa natumia kulazia kuku na watoto wake.
Hahahaha!