Nimepitia vichwa vya habari vya magazeti yote asubuhi hii, yakiandika kuhusu alichosema Kardinali Pengo kule Mwanza wakati wa mazishi ya Askofu Mkuu Anthony Mayalla. Wakati magazeti mengi yakiandika kuhusu jinsi Pengo alivyowashukia mafisadi, Mtanzania limesema: 'Pengo aumbua makamanda wa ufisadi'. ukiisoma habari ya gazeti hili unaweza kudhani Pengo naye ni mmoja wa watu wasiotaka vita dhidi ya ufisadi. kwani kwake wanaopinga ufisadi ni wale ambao wamekosa 'opportunity' ya kuwa mafisadi na sasa wanawaonea wivu mafisadi. Kwa bahati mbaya sikumsikiliza Pengo alipokuwa akiongea jana. Nitaamini ninachosoma tu kwenye magazeti. Lakini kauli hii (kama kweli aliitoa) naona ni muhimu ianzishe mjadala.
Mimi nilifanikiwa kuangalia shughuli yote kupitia Star TV jana na sijaona sehemu Mtanzania walipokosea, lakini hebu tuangalie magazeti mengine
1. NIPASHE: PENGO ATEMA MOTO MAZISHI YA ASKOFU
- Ahoji kulikoni ufisadi kila kona
- Auliza wapiganaji ni wakweli?
- Aitaka Serikali isiwazonge maaskofu
2. HABARILEO: WARAKA NI NENO LA MUNGU - PENGO
- Asema si lazima Serikali ibariki nyaraka za kanisa
- Asisistiza kelele za 'ufisadi' zitajenga chuki
- Ataka wanaozipiga wajitazame
3. TANZANIADAIMA: PENGO ACHARUKA
- Sasa awageukia wapiganaji wa vita vya ufisadi
- Apasha wasio na dhamira ya kweli wanyamaze
- Aeleza sababu ya ufisadi kutomalizika nchini
- Amshambulia Kingunge kupinga waraka wao
4. MWANANCHI: PENGO AIPINGA CCM
- Ataka Maaskofu wasifundishwe kazi na wanasiasa
Sijui ni magazeti gani hayo unayoyasema yaliyoripoti Pengo kuwashukia mafisadi? Magazeti yote yameripoti alivyohoji dhamira ya hao wanaoshabikia vita ya ufisadi, na ndivyo walivofanya gazeti la Mtanzania, sioni walipokosea, labda kama unataka kuhoji hiyo kauli ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.