Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 61,371
- 100,422
Nimesikitishwa sana na taarifa ya gazeti la Majira, na Lengo la kuandika hapa ni ili wajisahihishe .
Kilichoniuma ni kuona habari ya Mapokezi ya JK nchini CHINA kupewa kipaumbele as if ni kitu ambacho kitaisaidia Jamii ya Watanzania kuondokana na umaskini au kupata hata madawa kwenye hospital ambazo kumeripotiwa kuwa na uhaba mkubwa sana wa Dawa.
Kwa namna nyingine ni kumdhalilisha Rais yaani as if kilichompelekea China ni kwenda kuvunja historia ya mapokezi na sio kusaini mikatabam pengine majira hawakupendezewa na hio Mikataba (hata mimi sikuipenda) lakini wangeweza at least ku-highlight na issue ya mapokezi ikafuata chini yake (sub titles) yaani ingekuwa kama hivi;
KIKWETE ASAINI MIKATABA (MKATABA) YA MAENDELEO (?)
At least ingeleta maana kidogo.....
Magazeti mengi pia yameandika mapokezi hayo lakini haikua habari ya Kipaumbele, kwa mtu mwenye kufikiria pasipo kutumika, tena kutumika kijinga, huwezi kuacha habari nyingine muhimu ambazo zimetokea siku ya jana zikkiwemo hizo za hospital kuishiwa madawa, Mikataba ya TPDC kukataliwa, Jinsi ya Kujikinga na Ebola na mambo ya kiuchumi na katiba kwa ujumla halafu uje utuambie issue ya Mapokezi. Kweli? Kweli kabisa mtu unaweza kuandika vitu kama hivi?
Naiombeni mjirekebishe aisee, na tena naomba nieleweke vizuri kuwa sina Ugomvi kwa Profesa Kikwete kupokelewa kwa mbwembwe nyingi lakini haikua habari muhimu kwa Taifa ambayo ingestahili kuwekwe ukurusa wa mbele.
NB: SIZUNGUMZII SAFARI ZA JK NAZUNGUMZIA UZITO WA HABARI NA GAZETI LA MAJIRA

- NI YA ujenzi wa bandari
- utafutaji wa gesi (!!)
- Avunja rekodi ya mapokezi......
At least ingeleta maana kidogo.....
Magazeti mengi pia yameandika mapokezi hayo lakini haikua habari ya Kipaumbele, kwa mtu mwenye kufikiria pasipo kutumika, tena kutumika kijinga, huwezi kuacha habari nyingine muhimu ambazo zimetokea siku ya jana zikkiwemo hizo za hospital kuishiwa madawa, Mikataba ya TPDC kukataliwa, Jinsi ya Kujikinga na Ebola na mambo ya kiuchumi na katiba kwa ujumla halafu uje utuambie issue ya Mapokezi. Kweli? Kweli kabisa mtu unaweza kuandika vitu kama hivi?
Naiombeni mjirekebishe aisee, na tena naomba nieleweke vizuri kuwa sina Ugomvi kwa Profesa Kikwete kupokelewa kwa mbwembwe nyingi lakini haikua habari muhimu kwa Taifa ambayo ingestahili kuwekwe ukurusa wa mbele.
NB: SIZUNGUMZII SAFARI ZA JK NAZUNGUMZIA UZITO WA HABARI NA GAZETI LA MAJIRA
wewe kweli unashangaza. chuki zingine ni za kustaajabisha. hapo tanzania ndio imepata mapokezi makubwa wewe umekazania tu jk. ishara ya kufanikiwa ziara ni mapokezi. majira hawajakosea kitu.
Sikiliza Sumu, anachosema Elli ni kuwa kwa vile Official visit ya Rais wetu kule China inapaswa iwe wazi kwetu sisi Watanzania habari ya mapokezi yake haikizi haja ya kufahamu nini kimejiri kule China kwa sababu apokewe kifalme au kama mjakazi kwetu sio issue bali issue ni kazi iliyompeleka imefanikiwa kwa kiwango gani na ni nini hasa kimefanyika na kina manufaa gani kwetu. Huwezi kuweka mapokezi kama habari kuu huku ukiacha yaliyofanyika huko kama msingi mkuu wa ziara yake, hivi akirudi TZ na habari tunayoijua pekee ni mapokezi yake wewe utaona ni sawa?
Madhara ya kuandika kwa msingi wa kufurahishana ndio tatizo la vyombo vyetu vingi vya habari na sisi kama wananchi tunabaki weupe vichwani bila kujua nini kinaendelea nchini wakati transparency inatakiwa katika day to day Government activities sio mapokezi.
cc Elli