Gazeti la CCM Uhuru Heading: Siri maandamano Chadema yafichuka; Yajipanga kutumia Munguki

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
* Yajipanga kutumia Mungiki kuvuruga amani

NA MWANDISHI WETU
Gazeti la Uhuru


WAKATI CHADEMA ikitangaza kuanza maandamano ya nchi nzima kupinga muswada wa kuruhusu kuundwa tume ya kupokea maoni kuhusu katiba mpya, kuna taarifa kuwa chama hicho kimepanga kutumia wafuasi wa kikundi cha Mungiki kutoka Kenya kuhamasisha vurugu nchini.

CHADEMA pia inadaiwa kuandaa vijana wa Kitanzania 60,000 watakaoshirikiana na kikundi hicho kuwajenga kisaikolojia kushiriki kwa nguvu katika maandamano hayo.

Mkakati huo upo kwenye waraka (Uhuru ina nakala yake) uliosambazwa na uongozi wa juu wa chama hicho kwenda kwa makatibu wakuu wa CHADEMA katika mikoa ya Tanzania Bara.

Taarifa za kuaminika kutoka makao makuu ya chama hicho zilidai mpango huo utawapa ujasiri vijana kupitia wanaharakati hao kutoka Kenya.

"Tunapaswa kuwajengea uwezo wa kujiamini na kutosikiliza vitisho vinavyotolewa na serikali ili wawe tayari kushiriki kwenye maandamano,'' ilisema sehemu ya waraka huo kwenda kwa makatibu wakuu.

Waraka huo pia uliwataka makatibu wakuu kuhakikisha wanapata fedha za kutosha na kuziwasilisha makao makuu ili zitumike kuwalipa wanaharakati hao.

Alipoulizwa kuhusu habari hizo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema amepokea jalada la CHADEMA kuhusu maandamano lakini hajalisoma na kwamba leo atalitolea ufafanuzi.


"Jalada limefika mezani kwangu ila bado sijalisoma. Nitatoa ufafanuzi kuhusu maandamano hayo, hilo la Mungiki tutalifuatilia na tulitolea taarifa,'' alisema. Kwa upande wake, Mkuu wa Operesheni wa chama hicho, Benson Singo, alikana madai ya kushirikiana na kikundi cha Mungiki. Hata hivyo, alikiri kuwepo maandamano hayo, yatakayoanza Jumamosi katika mikoa 10.


"Kweli tuna maandamano yatakayohusisha viongozi wote wa kitaifa katika mikoa 10, lengo ni kupinga muswada wa maboresho ya katiba,'' alisema. Alisema maandamano hayo yatafanyika Arusha, Mbeya, Kigoma, Kilimanjaro, Ruvuma, Dodoma, Pwani, Mtwara, Tabora na Morogoro.

Katika hatua nyingine, Taasisi ya Demokrasia na Utawala Bora Tanzania (CEGODETA), imelaani tabia ya baadhi ya vyama vya siasa kupeleka vijana wahuni wa vijiweni kwenye midahalo ya katiba.


Inadaiwa vijana hao hupelekwa kwenye midahalo hiyo ili wakawazomee na kufanya fujo wakati wachangiaji wa vyama vingine wanapozungumza.


Mkurugenzi wa CEGODETA Thomas Ngawaiya alisema: "Tabia hiyo si ya kistaarabu na inaonyesha kuna baadhi ya vyama ambavyo viongozi wake bado hawajakomaa kisiasa, na wala hawakustahili kupewa nyadhifa walizonazo ndani ya vyama vyao."


Ngawaiya alisema endapo baadhi ya vyama vinaona utaratibu uliopendekezwa kupata katiba mpya haufai, ni vyema vipeleke maoni na malalamiko kwenye mamlaka husika au kupitia mikutano ya kujadili katiba badala ya kufanya fujo, kuzomea au maandamano.

Taasisi hiyo imetoa wito kwa vyama vyote vya siasa na wananchi kuwa watulivu katika kipindi cha kukusanya maoni. Pia wameiomba serikali kuongeza muda wa ukusanyaji maoni.
 
wabunge na viongozi wa cdm sisi vijana wa udom tumesikia kuwa mswada umeondolewa sasa tunauliza maandamano yapo au vipi kama yapo tujipange vya kutosha dada regia au yoyote tupeni tarifa ili tujue siku hio tuiweke kwa ajili ya kutetea watanzania
 
Kwanini Chama Tawala always gossiping about Chadema?

Na Polisi wanatumiwa kama Commando ya Chama Tawala; Mauaji ya wananchi yalitokea hivi karibuni hawakuweza kupatikana lakini Maandamano ya Chadema wameisha jipanga vilivyo
 
inaonekana hii ndio CCM yenye gamba jipya!!!! tehetehetehete!!! keep it up chadema...ishu hapa ni KUBADILIKA NA KUWA KIUMBE KISICHODHURU NA KULETA SHIDA KWA BINADAMU NA SIO KUBAKIA NYOKA!!!
 
Nilisahaacha kusoma gazeti hilo kitambo sana. Kwa hiyo hata kama siku ya kiama ikitangazwa humo nafikiri sitaweza kujua.
 
Nilisahaacha kusoma gazeti hilo kitambo sana. Kwa hiyo hata kama siku ya kiama ikitangazwa humo nafikiri sitaweza kujua.

Yeah same here lakini kama CCM ikitoka Madarakani 2015 Uhuru na ndugu zake yatakufa kama KANU iliposhindwa KENYA TIMES pia iliaga na maisha kukatika.
 
MUNGIKA, KAMA WALIVYOKUA AL-SHAABAB, LAZIMA NI WAGENI WENU CCM WALA MSICHANGANYA MADA HAPA!!!

Maandamno ya CHADEMA nchi nzima iko pale pale kwa kuwa kuna mengi sana kubadilishana na Nguvu ya Umma hasa kuhusu hali ya siasa na madai ya kuundwa kwa Katiba Mpya nchini.

Hivyo kma kuna madai ya Mungiki basi ni wa kwao Kikwete na Kalonzo Musyoka wa Kenya ndio waliowapeleka kule Libya kumsaidia swahiba; na Gaddafi hakufanya ajizi na hiyo rasilmali watu hata akwapeleka mtari wa mbele vitani na Mungiki wakachinjwa zaidi ya nzige kila mahali huko ugenini.

Nadhani Mhariri huyu wa CCM alichanganya kidooogo amechanganya mada hapa tofauti na maelekezo halisia. Kwanza Watanzania hawhitaji maelekezo ya Gazeti la CCM kujua maandamano ya CHADEMA yameandaliwa vipi.

Huu ni ulofa na kufilisika kwa CCM; tangu maandamano yooote ya CDM hakujawahi kwepo na matukio ya aina hiyo zaidi tu ya NGUVU YA HOJA masikioni.

Hata hivyo kwa kuwa hapa katikati CCM walidiriki kukodisha Al-Shaabab toka Somalia ili kutekeleza machafu yao nchini wala haitoshangaza hku ku-panic kwao wakamuomba Mzee Moi hao ma-Mungiki kuja nchini.
 
Ujumbe kwa Chadema;

Chama hiki kipenzi cha wananchi wajiangalie sana katika maandamano yao wikiendi hii. Kuna tetesi kwamba CCm wamepanga kupandikiza "Mungiki" wa kufanya fujo katika hayo maandamano kuonyesha kwamba CDM ni chama cha vurugu kinachotaka kuvunja amani.

Chadema wawe makini -- kwani kutokana na yaliyozuka huko Dom, CCM iko katika its lowest ebb na nyota ya CDM inang'ara sana. Ufisadi wote uliotikisa CCM ulitokana na juhudi za CDM kwa hivyo CCM wana kila sababu kutaka kukipaka matope chama hicho.

Be careful CDM!
 
Kama ni kweli ndio maana CCM nchi inawashinda baada ya kufikiria jinsi gani wataondoa kero zinazowakabili wananchi wao wanafikiria jinsi ya kuichafua chadema. Pole zao
 
Mungiki yahusishwa na CDM mnh!Naona sasa ccm wameamua kuja na singo mpya kujaribu tena soko baada ya zile za awali kutokufanya vizuri...teh teh teh lol...!Wamefulia.
 
hilo linajulikana ila nacho mshukuru Mungu ni juu ya watanzania kujua kila kitu na wamekuwa na upeo mkubwa sana wa kuchambua mambo kwa hyo naimani watanzania watajua yote hayo na kuwapuuza
 
wabunge na viongozi wa cdm sisi vijana wa udom tumesikia kuwa mswada umeondolewa sasa tunauliza maandamano yapo au vipi kama yapo tujipange vya kutosha dada regia au yoyote tupeni tarifa ili tujue siku hio tuiweke kwa ajili ya kutetea watanzania

unapoongelea umma fulani wakati si waliokutuma kusema maneno hayo unakuwa unakosea bwana mdogo, mimi mwenyewe nipo hata UDOM, Na sijapata taarifa yoyote uliyoiwasilisha hapo juu kwamba "SISI UDOM TUMEJIPANGA" uwe unazingatia itifaki, kama unataka taarifa juu ya maandamano hayo, mtafute "ALEX MUSHI" kwenye facebook atakupa ratiba. Dont use generalization again, that is fallacial.
 
hilo linajulikana ila nacho mshukuru Mungu ni juu ya watanzania kujua kila kitu na wamekuwa na upeo mkubwa sana wa kuchambua mambo kwa hyo naimani watanzania watajua yote hayo na kuwapuuza

Pamoja na hayo ni lazima viongozi wa CDM wawe makini. habari kutoka Mby zasema kuwa yule Kitambara anapanga vijana wa CCM wasio na kazi kufanya vurugu katika mkutano wa chama.
 
Ujumbe kwa Chadema;

Chama hiki kipenzi cha wananchi wajiangalie sana katika maandamano yao wikiendi hii. Kuna tetesi kwamba CCm wamepanga kupandikiza "Mungiki" wa kufanya fujo katika hayo maandamano kuonyesha kwamba CDM ni chama cha vurugu kinachotaka kuvunja amani.

Chadema wawe makini -- kwani kutokana na yaliyozuka huko Dom, CCM iko katika its lowest ebb na nyota ya CDM inang'ara sana. Ufisadi wote uliotikisa CCM ulitokana na juhudi za CDM kwa hivyo CCM wana kila sababu kutaka kukipaka matope chama hicho.

Be careful CDM!


Ni kweli usemayo mkuu. CCM imefika chini sana katika popularity yake in over 50 yrs. Inaweza kutaka kuiharibia CDM ili kionekane chama cha vurugu tu katika jamii.
 
Ccm siku zote kazi yao ni kutetea serikali ili iendelee kuwa madarakani na sio kuwatetea wananchi ili waje kuwachagua tena hawa wayaondoka kwa nguvu za watu zitokanazo na mungu...
 
CCM wanataka kupoteza lengo. Agenda hapa ni wao kujidai kuvua gamba sio CDM. Wasafishane tu waache kutusema. That is gossiping na ni dhambi, Si tukisema kitu ni cha kweli na watudhihirishia kuwa we were right all along. Na bado tuhuma zote tulizotoa zitathibitishwa kuwa ni kweli.
 
Si walisema chadema ni cha wachaga, cha kikanda, cha kikristo na sasa hivi ni cha munguki au al shababu, mwishowe kitaitwa chama cha kigaidi
 
Huo ndio wendawazimu, hao vijana kutoka Kenya wataingiaje nchini bila kuwa na hati za kusafiria, au ndio hakuna mipaka tena? Je, ni CDM waliokubali muafaka wa EAC? Je serikali iliyopo madarakani kwa nini isiwashike hao Mungiki Brothers mapema na kuwachukulia hatua za kisheria? Je, huu ndio utawala bora wa sheria ambao wanahubiri kila kukicha lakini wanashindwa kuwachukulia hatua mafisadi ndani ya chama chao?
 
Back
Top Bottom