Gazeti: 'CHADEMA yanuka damu'

Gazeti: 'CHADEMA yanuka damu'

Laiti Chadema, CCM ama chama chochote cha siasa na hata serikali ingelazimika kujibu kila linaloandikwa kwenye kila gazeti na hasa magazeti yenyewe yakionyesha wazi mwelekeo wa "kuganga njaa" nadhani hivyo vyama ama serikali basi vitakuwa havina kazi nyingine zaidi ya kujibu tuhuma ambazo magazeti hayo kila siku yatatuhumu. Imethibitika yapo magazeti au sahihi tuseme vipo vigazeti ambavyo watu hukaa na kutunga "habari" yeyote na kuitoa ili mradi ivutie watu na ama gazeti liuzike au kwa malengo mengine ya kisiasa. Aghalabu sasa hivi imekuwa kitu cha kawaida kuona kichwa cha habari cha gazeti kikiwa tofauti kabisa na maelezo ya habari yenyewe.

Ipo haja ya marekebisho ya dhati ya Sheria ya Vyombo vya Habari na wasimamizi wake wawe waadilifu wasiokinzana na msemo wa "sheria ni msumeno hukata kotekote". Naamini, kwa mwenendo tulioanza kuushuhudia badala ya "Chadema yanuka damu" kichwa cha habari kingekuwa "CCM yanuka damu" si ajabu hicho kigazeti kingekuwa mashakani kufungiwa kwa kuandika habari za uzushi, habari zisizofuata maadili ya uandishi n.k
 
Wapo wasomaji wake kwani huwajui wamiliki wao!
Wasomaji wa gazeti hili jata awe msomi vipi lakini atasimamia hata upuuzi kutokana na imani yake !

...nakusoma mkuu ndo maana wanalishwa matango pori kirahisi sana...
 
Back
Top Bottom