Gas Mtwara-naomba tutizame haya

Gas Mtwara-naomba tutizame haya

MIGNON

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2009
Posts
4,120
Reaction score
5,119
Mod naomba isiunganishwe ili tupate mchepuo mwingine wa majadiliano.
Nimemsikia Rais JK akihutubia taifa na kueleza kwa ufasaha kuhusu suala la gas Mtwara pamoja na yaliyojiri.
Binafsi nimeridhika sana na maelezo ya Rais hasa ufafanuzi aliutoa kuhusu processing ya gas,usafirishaji na viwanda vitakavyojengwa Mtwara na kwa maelezo ya Rais na uelewa wangu ni kuwa hapakuwa na sababu ya vurugu wala majibishano kwani kila kitu kipo in black and white!!!!!.Maswali kidogo,ikiwa hivyo ndivyo,
  1. Kwa nini PM alikwenda Mtwara wakti mambo yote yako wazi kiasi hicho?
  2. Kwa nini PM alitumia muda kusikiliza hoja za wadau mbalimbali wakati kila kitu kilikuwa wazi?
  3. Kwa nini Katibu Mkuu wa CCM aseme wana Mtwara wana hoja na inabidi wasikilizwe?
  4. Kwa nini Zitto,mwanasiasa anayeonekana kuwa na mawzo huru nae alidai kuwa wananchi wana hoja?
  5. Kwa nini washiriki wa baraza la mawaziri kama Mkuchika na Ghasia washindwe kui contain hoja ya wana Mtwara wakati mambo yako wazi?
  6. Je kuna uwezekano wa kuwa wana Mtwara walielezwa yote hayo kabla (kuhusu kiasi cha gas itakayobaki,viwanda n.k) lakini wakafanya waliyofanya kwa ubishi tu?
Nahisi kuna jambo ambalo haliko wazi au kuna kutokuwajibika au kuna hujuma ya maksudi kwa JK toka kwa wateule wake.
Hebu tujadiliane kidogo.
 
6.Je kuna uwezekano wa kuwa wana Mtwara walielezwa yote hayo kabla (kuhusu kiasi cha gas itakayobaki,viwanda n.k) lakini wakafanya waliyofanya kwa ubishi tu?
Nahisi kuna jambo ambalo haliko wazi au kuna kutokuwajibika au kuna hujuma ya maksudi kwa JK toka kwa wateule wake.
Hebu tujadiliane kidogo.
Wananchi hawakuelezwa haya yote kabla!, ushirikishwaji wa wananchi ulikuwa mdago hivyo kutoa mwanya wa upotoshwaji!. Kati ya yote rais aliyoongea, mengi yanawahusu wanaMtwara, litakapokuja suala la mkataba wa ujenzi wa bomba la mafuta, hili sasa sio la Wanamtwara!, hili ni letu sote!.
Pasco.
 
Ni kweli lakini tatizo la serikal ye2 imezoea kuziba pancha badala ya kununua tairi jipya, Kama hii mikakati ilikuwepo kabla kwa nini wananchi hawakuathe mbiwa mapema mpaka ikangoja maafa ndo wakaambiwa ukweli huu na kama sio uwongo. Kwanini maamuzi ya kujenga kinu yamekuja baada ya maandamano, hili ujue jinsi gani yetu isivyoenda bila maandamano. Hapa KUNA BEHINDE THE SCENE nachowaasa Wanamtwara wawe waangalifu kwa hili wakifumba macho imekula kwetu. sikatai mengi yamefanyika kuendeleza mladi huu wa gesi, lakini kwa nini kimya kimya mpaka yatokee huu NI URASIMU TUPU HAKUNA CHOCHOTE, hebu ona na ujiulize kwanini MP alikimbia MASWALI? na kusingizia anawahi ndege wakati aliruhusu maswali yataulizwa baada ya kikao akasingizia ndege itamuacha....mmmmh! kuna nini hapa hi ndo nchi yetu tusubiri WAMAKONDE TUIBIWE
 
Wanadai gesi inapelekwa dar kwa maendeleo ya nchi, Hivi mtwara cio tanzaia, Gesi ikiprossesiwa kule na kusafirisha umeme uliotayari kwa nguzo to DAR hautatumika?, au mji wa Mtwara ukiendelezwa, Bandari ipo tena asilia, Uwanja upo ni marekebisho tu, Barabara ndo hiyo isiyoisha, mmmmh mambo mengine haya hayahitaji hata Mchumi Lipumba aje afanye tasmini ni plann tu na mikakati na sio kutanguliza urasimu mbele. Hili mbona linawezekana na sio kurundika Dar, serikari haijui ina karibisha umaskin siku Dar ikivamiwa na kulipuliwa Tanzania ndo basi tena tunapoteza kila kitu....Tulifikirie hili kwa MAENDELEO ENDELEVU (SUSTAINABLE DEVELOPMENT)
 
Wananchi hawakuelezwa haya yote kabla!, ushirikishwaji wa wananchi ulikuwa mdago hivyo kutoa mwanya wa upotoshwaji!. Kati ya yote rais aliyoongea, mengi yanawahusu wanaMtwara, litakapokuja suala la mkataba wa ujenzi wa bomba la mafuta, hili sasa sio la Wanamtwara!, hili ni letu sote!.
Pasco.
Pasco,nashukuru kwa mchango wako.
Nashindwa kuamini yaliyotokea na nina hamu sana kuona michango mingi zaidi ili tujue wa kumlaumu katika hili na ambaye atabeba dhamana ya hasara iliyotokea.
Ngoja tusubiri wadau naona wengi leo wanaangali Nigeria vs Ivory coast!!!
 
Ukweli ni kwamba hapo awali jitihada za kuwapotosha wananchi zilikuwa kubwa kuliko jitihada za kuwapa wananchi taarifa sahihi.

Hapa tunajifunza kuwa iwapo wapinzani wataendelea kufanya siasa chafu za upotoshaji, gharama ya mawasiliano kati ya serikali na wananchi inaongezeka mara dufu.

Chama tawala kinapaswa kutekeleza wajibu wake na wapinzani wanapaswa kuwa na siasa safi za kizalendo. Bila hivyo maendeleo tutayachelewesha mno...
 
Back
Top Bottom