Gari zinazotumia Gongo?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gari zinazotumia Gongo??

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by redSilverDog, Mar 7, 2011.

 1. redSilverDog

  redSilverDog JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 486
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwavile tunagombana na wapika gongo, kwanini tusinufaike nao ili na sisi wote pia tunafaike.

  Ni hivi, iwapo mabasi au daladala zote zitatumia gongo ama kiutaalam zaidi ETHANOL gharama za usafiri zitapungua au sio? Pia, tutahifadhi mazingira na akina mama wapika gongo watapata ajira!! Na ile miwa ya moro si itatumika kisawa sawa au?

  Pia 2tapigiwa mfano katika nchi zinazohifadhi mazingira!!

  Najua najua najua!!! matajiri wauza mafuta watakula wapi?? Sasa hapa si ndo 2fanye maamuzi magumu au?

  Lakini ndo hivyo bwana!!
   
 2. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Yaaani its need decsionmakers wenye kutaka kufanya

  • maamuzi ya kibunifu
  • Kujaribu mambo mapya
  Our leader wamekariri mapaka USA UK wafanye nawao ndo wanafanya.

  Sio tu kutumia gongo kwenye gari binafsi sioni sababu ya kupiga gongo marufuku wakati kuna kiwanda cha konyagi. Kwa nn wasiunde chombo maalum cha kuwa kinahakikina kuweka standadr na kuwapa vibali hawa local manafucturer. Yes watapata mapato kiasi.

  Hata scotch whisky huko ulaya kuna watu wanatengeza majumbani mwao.

  We have set ourselves to be just consumers na tunajiwekea vikwazo wenyewe pale watu wanapotakakuwa wazalishaji.

  Ni aibu Hakuna hata mbunge au waziri mwenye ujasiri wa kuongelea gongo. wakati wako tayari kuongelea kodi za Whisky.

  Watu wanakunywa whisky zinaitwa malibu hawajui ni modified version ya gongo ya Nazi. Sasa kwa nn isiwepo accepted gongo version ya ndizi, miwa , etc.

  Kuna waziri alikuwa anaitwa Kinyondo RIP yule jamaa alishawai kusema haya watu wakawa wanamuona hafai.

  teh teh.
   
 3. Mwelewa

  Mwelewa JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 2,238
  Likes Received: 2,349
  Trophy Points: 280
  Kweli, hii di aidea nzuri sana na pia inamaslahi kwa hawa wakinamama na kwa nchi, ila si unajua mawazo ya viongozi wetu au hujui?
  Watu wanajitahidi kuwa wabunifu lakini hakuna msaada wowote, nadhani ingekuwa poa kama serikali ingeangalia hili swala kwa kina na kufanya maamuzi yatakayotoa fursa za ajira.
  Vipi kuhusu magari mengi yaliyopo hapa nchini yatafaa kutumia gongo(ethanol)? Ok, hii inawezekana kama kutakuwa na wataalam wa kubadilisha mfumo wa engine au sio?
  Lakini je, vipi kuhusu upatikanaji wa hizi malighafi kwa ajili ya production ya hii gongo kuweza hudumia magari je zinatosha? Labda iwe inatengenezwa kwa kutumia miwa au hizo ndizi vipi hapa au ndo itakuwa aidea ya muda tu na baadae kushindikana kwa kukosekana kwa malighafi? Vipi haita leta usumbufu wa chakula kwa wale ndugu zetu wanaotumia ndizi kama chakula? Vipi kuhusu miwa, kama wazalishaji watakuwa wanauza sana kwa hawa watengenezaji wa hii ethanol kwa ajili matumizi ya magari kama nishati mbadala, si ndio tutakuwa na upungufu wa sukari? Ok nilisahau labda sio ishu sana kama tutokuwa hatunywi chai,, anyways tunaweza import ila daah hii si ndio ile inaitwa (inelastic good) sasa hapo vipi si ndio tatizo juu ya tatizo maana inelastic goods huhitajika hata kama ni bei gani,, nadhani hapa mshahara wa kabwela ndio utafika kikomo na kusababisha madeni juu ya madeni!
   
Loading...