Gari la waziri mkuu mstaafu yapigwa mawe

Gari la waziri mkuu mstaafu yapigwa mawe

Joined
Sep 18, 2013
Posts
40
Reaction score
5
Katika kile kilichoelezwa kuwa na mwendelezo wa uhasama wa kisiasa, Gari la aliyekuwa waziri mkuu wa JMT mh. Sumaye limepigwa mawe na kundi LA watu wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa mbunge wa wilaya ya Hanang mama Mary Nagu.
Sumaye ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa wilaya ya Hanang mkoani manyara amekutwa na mkasa huo baada ya kumalizika Kwa mkutano wake wa hadhara aliyoifanya hapo Jana mjini katesh.

Hata hivyo hakuna madhara makubwa yaliyoripotiwa kutokana na shambulio Hilo.

Ikumbukwe kuwa waziri mkuu huyo aliyehudumu katika serikali ya awamu ya mkapa amekuwa akitajwa katika harakati za kuusaka urais October.

My take: Watanzania bado hatujafahamu namna tulivu ya kuwakataa tusiowapenda kisiasa badala yake tunakuwa harsh kwa mahasimu wetu wa kisiasa.

More to follow......
 
Hapendwi hadi jimboni kwake? Si bora awe tu mzee wa kabisa atulizane
 
kwani sumaye na nagu wana uhasama hadi wafuasi wa nagu wamshambulie?
 
Hapendwi hadi jimboni kwake? Si bora awe tu mzee wa kabisa atulizane

Huo ni mkono wa Mama Nagu kibaraka wa Lowasa. Ni vurugu za kutengeneza. Mama Nagu anagawa matrekta kama baiskeli vile sijui ana biashara gani. Jeuri ya fedha kamconfuse mme wake Prof.
 
mwaka 2015 ni mwaka mgumu kisiasa tusipokua watu wa kuvumiliana yaliotokea Kenya yanaweza kujirudia TZ.
 
Ni heri sumaye kuliko nagu huyu mama anqroho mbaya sana.
 
Hivi mtu ukishakuwa waziri mkuu unataka nini tena???!!!
Acha yawakute. . . .
 
Mama Nagu mume wake ni Prof. Wa wapi???ndio kwanza nasikia kiongozi wa kike ana mume.Nilidhani wamejitolea kulitumikia taifa kama watumishi wakikatoliki.
 
Back
Top Bottom