Gari la Waziri lahusishwa kwenye wizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gari la Waziri lahusishwa kwenye wizi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 19, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Gari la Waziri lahusishwa kwenye wizi Tuesday, 18 January 2011 21:38

  Sadick Mtulya
  JESHI la Polisi Mkoani Morogoro, limekamata gari la Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Lucy Nkya likihusishwa kubeba tani 30 za madini ya shaba iliyoibwa mkoani Morogoro.

  Shaba hiyo yenye thamani ya zaidi ya Sh 300 milioni iliyoibwa wakati ikisafirishwa kutoka nchini Zambia kuelekea jijini Dar es Salaam. Pia, jeshi hilo limemtumia mtoto wa waziri huyo, Jonas Nkya kumtia mbaroni mmoja wa watuhumiwa ambaye alikuwa ni meneja wa hoteli inayomilikiwa na waziri Nkya.

  Gari hilo aina ya Toyota Surf lililokamatwa Jumamosi iliyopita, linashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Morogoro. Taarifa ambazo zilipatikana jana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani humo, Adolpine Chialo, zilisema gari hilo lilitumiwa na mtuhumiwa (jina linahifadhiwa) ambaye ni meneja wa hoteli moja , inayomilikiwa na Waziri Nkya.

  “Tumelikamata gari aina ya Toyota Surf inayomilikiwa na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Nkya kutokana na kuhusika kubeba madini ya wizi Januari 11 mwaka huu majira ya saa 3 usiku eneo la Madafu barabara kuu ya Morogoro – Dar es Salaam,’’ alisema Chialo.

  Akaongeza: “ Gari hili lilitumiwa na meneja wa hoteli inayomilikiwa na Dk Nkya.’’ Kamanda huyo alieleza kuwa , kabla ya tukio kufanyika, mtuhumiwa aliidanganya familia ya Nkya kuwa gari hilo lilikuwa bovu na kwamba lilitakiwa kufanyiwa matengenezo.

  “Ndipo huyu mtuhumiwa akatumia mwanya huo kubeba madini haya,’’ alisema. Hata hivyo, Kamanda huyo alisema polisi walilazimika kumtumia mtoto wa waziri, Jonas Nkya ili kufanikisha kumpata Meck kutokana na kukimbia baada ya kufanya tukio hilo.

  “Si kweli kwamba polisi inamshikilia Jonas kwa tuhuma za kuhusika katika tukio hilo ila tulimtumia kufanikisha kumpata mtuhumiwa na si vinginevyo,’’ alisema.

  Mbali na mtuhumiwa huyo,watu watatu pia wanashikiliwa kuhusiana na tukio hilo huku watuhumiwa wengine tisa wakitafutwa. Juzi Kamanda huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa shaba hiyo ilikuwa imepakiwa kwenye gari aina ya lori Scania lililokuwa likiendeshwa na mmoja kati ya watuhumiwa waliokamatwa ambaye ni mkazi wa Mafisa Manispaa ya Morogoro.

  Alisema baada ya polisi wa kikosi cha kupambana na ujambazi wa kutumia silaha kupata taarifa za kutelekezwa kwa gari hilo ambalo ni mali ya Dhandlo Road Haulage T. Limited eneo la madafu walilifuatilia na kulikuta na shaba pamoja na nyaraka za shaba hiyo na kwamba baada ya uchunguzi wa haraka alikamatwa dereva wa gari hilo jina limehifadhiwa ambaye alitoa ushirikiano kwa polisi na kufanikiwa kukamatwa kwa wenzake.

  Katika mahojiano na polisi watuhumiwa hao waliweza kuonyesha mahali ilikofichwa shaba hiyo eneo la Forest Hill na hivyo polisi kufika katika eneo hilo ndani ya nyumba ya mtu mmoja jina limehifadhiwa ambaye kwa sasa yuko masomoni mkoani Dodoma na kwa kipindi kirefu nyumba hiyo aliachiwa mmoja wa watuhumiwa hao jina limehifadhiwa ili kuishi.

  Alisema madini hayo yalikuwa yamefichwa katika nyumba hiyo kwa kufukiwa ardhini na juu kumwagwa mchanga na kwamba yaliweza kufika katika nyumba hiyo baada ya mmoja wa watuhumiwa hao jina limehifadhiwa ambaye ni dereva wa winji kuyatoa huko porini lilipoachwa gari hilo na kuyashusha katika eneo hilo.

  Kamanda Chialo alisema polisi wanaendelea na zoezi la kukagua eneo la nyumba hiyo pamoja na kuimarisha ulinzi wa saa 24 ili kubaini mali na vitu vingine ambavyo vinaweza kuwepo katika nyumba hiyo na kwamba tayari mmiliki halali wa madini hayo ameshatambulika na uchunguzi zaidi kuhusina na tukio hilo unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwatafuta wengine waliohusika katika tukio hilo kwa namna moja ama nyingine ili waweze kufikishwa mahakamani.


   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Hivi hii habari imekaaje, vile..........yaani inawezekana gari aina ya TOyota Surf kubeba tani 30 za shaba kama inavyodaiwa humu...........................
  Something is terribly amiss here..........what do you think.......................................Have your say..........................


   
 3. M

  Misterdennis JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2011
  Joined: Jun 4, 2007
  Messages: 1,521
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Mtoto wa huyo waziri anaweza kuwa behind the deal ... na meneja akawa kama alivyo .. an employee; ila baada ya dili kulipuka kageuzwa kafara.
   
Loading...