Gari la serikali linapotengenezwa na kampuni ya uwindaji nini fadhila ya serikali kwao? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gari la serikali linapotengenezwa na kampuni ya uwindaji nini fadhila ya serikali kwao?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mkute, Jul 21, 2012.

 1. mkute

  mkute Member

  #1
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  DSC03279.JPG DSC03276.JPG DSC03277.JPG Jamani naomba ufafanuzi kama sheria inaruhusu gari la serikali kama linavyooneka katika picha kutengenezwa pindi linapoharibika katika karakana ya moja ya wawekezaji wakubwa katika sekta ya uwindaji nchini,ambayo hivi karibuni iliwahi kuhusishwa na tuhuma za kuhonga gari kwa Dc mmoja wa wilaya iliyopo kanda ya ziwa na kupelekea wananchi kuchomewa nyumba zao na polisi eti kuwalazimisha kuhama katika maeneo ambayo inadaiwa kuwa ni sehemu ya hifadhi,jambo lilopelekea mbunge wa wananchi hao kulisemea bungeni mwaka huu na kutakiwa kupeleka ushahidi na mh. spika.Gari hili ambalo inasemekana lipo ndani ya garage ya kampuni hiyo inasemekana limetoka wilaya husika, swali langu ni je hizi ndio fadhila za wawekezaji kwa serikali? kama sivyo inamaana serikali haina pesa za kukarabati hata magari yake kiasi cha kuishiwa hata matairi kama inavyoonyesha katika gari hili ikitegemea wawekezaji? Tunakwenda wapi kwa mtindo huu kweli serikali yetu itakuwa na sauti ya kutetea wananchi wake au itatetea wawekezaji wanaoifadhili namna hii?,naomba kutoa hoja!
   
 2. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Red: nakuonyesha kwamba unaficha vitu vingi, inashangaza kama umeweza kuipiga picha sehemu ambayo gari lipo nini kinakufanya kuanzisha taarifa ya kificho hapa. Kama umeweza kuleta hadi namba za gari ni kwa nini unajiumauma sana kusema wazi kwenye red humo???
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Hilo ni kosa huna haja ya kuficha kama ukweli unao,
   
 4. mkute

  mkute Member

  #4
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Mkuu sio kwamba nafichaficha au kujiumauma mambo hayo mbona yako wazi kama wewe ni mfatiliaji wa mambo mzuri labda kama leo ndio umejiunga humu JF.
   
 5. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  weka wazi washughulikiwe kijana
   
Loading...