Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 4,102
- 3,436
Kuna taarifa na picha ya gari hilo la rangi ya kijani likiwa limeegeshwa katika nyumba moja huko Tabata maeneo ya Jiandae. Taarifa zaidi hapo baadaye.
Nami nimewaza kama wewe Gembe,iweje huyu jamaa atenganishwe kichwa chake na kiwiliwili,alafu mazingira aliyookotwa ni njia panda ili wapita njia wamwone watoe taarifa kituo cha polisi.
Hawa mabedui walipanga kabisa kumwondoa roho na ili wasifuatiliwe kwa karibu kabla ya kutimiza azima yao wakawa wametuma SMS kwa mamsapu ili ajue tu jamaa katumwa na mheshimiwa.Tibagaina tupe ripoti na hao wauaji watiwe nguvuni haraka.
Bila shaka tusubiri uchunguzi wa Polisi maana ni mapema mno kuharakisha kupata taarifa zao, ila nakumbuka gari hili lilitiwa dawa maalum kabla halijaondolewa pale tabata Kimanga na kukawa na alama za vidole nyingi tu ambapo Polisi wa IB walichukua picha kwa ajili ya kufanyia kazi. Nadhani pia kuna haja ya kutumia utaalamu wa DNA kupata wahusika halisi wa tukio hili.