Gari la msafara wa IGP Sirro laua Morogoro

Gari la msafara wa IGP Sirro laua Morogoro

Besta Mlagila

Senior Member
Joined
May 29, 2018
Posts
101
Reaction score
191
Jackline Samwel (9), amefariki dunia leo Alhamisi Desemba 12, 2019 baada ya kugongwa na gari lililokuwa katika msafara wa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro mkoani Morogoro.

Akizungumza na Mwananchi leo kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Mugabo Wekwe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, “ni kweli ajali imetokea leo saa 4 asubuhi eneo la Kwa Makunganya.” Amesema Jackline ni mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya Msingi Mbwanga mkoani Dodoma, kwamba amegongwa na gari la msafara huo wakati akivuka barabara eneo la Kwa Makunganya manispaa ya Morogoro.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema mwanafunzi huyo aligongwa na gari wakati akivuka barabara baada ya kutoka kununua maji akiwa na mama yake mdogo na ndugu zake wengine watatu.

Wanaeleza kuwa baada ya wenzake kuvuka kurejea katika basi la kampuni ya ABC walilokuwa wakisafiria kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam, yeye alikuwa wa mwisho kuvuka ndipo alipogongwa na gari hilo na kufariki dunia.

Kaimu kamanda huyo amesema mwili wa mwanafunzi huyo umehifadhiwa Hospitali ya rufaa Mkoa wa Morogoro.
 
Morogoro. Jackline Samwel (9), amefariki dunia leo Alhamisi Desemba 12, 2019 baada ya kugongwa na gari lililokuwa katika msafara wa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro mkoani Morogoro.

Akizungumza na Mwananchi leo kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Mugabo Wekwe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, “ni kweli ajali imetokea leo saa 4 asubuhi eneo la Kwa Makunganya.”

Amesema Jackline ni mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya Msingi Mbwanga mkoani Dodoma, kwamba amegongwa na gari la msafara huo wakati akivuka barabara eneo la Kwa Makunganya manispaa ya Morogoro.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema mwanafunzi huyo aligongwa na gari wakati akivuka barabara baada ya kutoka kununua maji akiwa na mama yake mdogo na ndugu zake wengine watatu.

Wanaeleza kuwa baada ya wenzake kuvuka kurejea katika basi la kampuni ya ABC walilokuwa wakisafiria kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam, yeye alikuwa wa mwisho kuvuka ndipo alipogongwa na gari hilo na kufariki dunia.

Kaimu kamanda huyo amesema mwili wa mwanafunzi huyo umehifadhiwa Hospitali ya rufaa Mkoa wa Morogoro.

Chanzo: Mwananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani kwa maelezo hayo huyo mama mdogo atakuwa jinga kabisa......
alimuachaje mtoto nyuma badala ya kuvuka wote!!!?
Wanawake bana...... Siku moja Arusha pale posta Mama anavuka anamwacha mtoto wa 4yrs nyuma....... Alitukanwa Sana maana boda boda ilikuwa apite naye...

Mtu mzima inatakiwa uwe nyuma watoto mbele..... Na happy uwe umeshapiga macho Kama kamera za traffic
 
Ajali inatokea kwa mtu yoyote, tusiweke siasa, poleni wafiwa, pole sana IGP
 
Igp ashtakiwe kwa kusababisha ajali. Kwani hakuwaelekeza madereva wa msafara wake waendeshe kwa kuzingatia alama za barabarani? Awajibike!
 
Igp ashtakiwe kwa kusababisha ajali. Kwani hakuwaelekeza madereva wa msafara wake waendeshe kwa kuzingatia alama za barabarani? Awajibike!
Ukizingatia eneo husika hurusiwi kuendesha kwa speed zaidi ya 60kmp
 
Inauma sana. Tena mtoto na mama yake walikuwa safarini kwenda Dar. RIP.
 
Back
Top Bottom