Hii haina tofauti na wewe ambaye huwezi kumuachia house girl wako ATM card ila unamuachia mtoto wako wa kumzaa mchana kutwa.Wewe unanunua passo au vitz ya milion 5 mbwembwe nyingii...unaweka alarm...funguo unaficha mbalii...hutak mtu aiguse guse ...
Ila cha ajabu sasa wabongo wengi wananunua gari la milion 40 anampa teja amiliki tena muda wote hadi lizeeeke.....
Najiuliza gari ni kitu kinchosaminiwa sana na mtu yoyote akitaka kusafiri either kutoka kituo kimoja kwenda kingine au mtaa mmoja kwenda mtaa mwingine lazima utaona anaoga, anajiweka safi safi....cha ajab gari unaloenda kupanda unakuta linaendeshwa na dereva teja na konda teja...
Swali ninayojiuliza na naomba tusaidiane..
1. Je ni nn chanzo cha haya magari kuendeshwa na kusimamiwa na hawa mateja??
2. Je hakuna vijana wasafi watanashati wanaweza kurun hii huduma ya usafiri.
3. Je ni kwa nn madereva na kondakta hasa kondakta lazima afungie suruali kitambaa ama kamba ya katani na surual kuwa inalegea...
4. Kwa nn wachafuuuu na kauli zao chafu.
Nini tufanye ili hii huduma muhimu ambayo watumiaji wanajali usafi ila waliomo ndani ya gari hawajali usafi na utu.
Kama uko kwenye daladala tunaomba utupie picha ya konda alivyo vaa hapo sasa hivi
Njoo arusha uone walivyo wasafi wa lugha na mavazi huku wakimiliki smartphones
Labda ni nature tu ya huo mji, uchafu[/QUOTE
Njoo arusha uone walivyo wasafi wa lugha na mavazi huku wakimiliki smartphones
Labda ni nature tu ya huo mji, uchafu
mkuu wewe umeongea kitu muhim sana Leo yaan tunaweza kumuachia mtoto mpk jion lakin ATM card hata kwa saa tu hatuwezi kumuachiaHii haina tofauti na wewe ambaye huwezi kumuachia house girl wako ATM card ila unamuachia mtoto wako wa kumzaa mchana kutwa.
Duh inauma ila hakuna namna wakuuHii haina tofauti na wewe ambaye huwezi kumuachia house girl wako ATM card ila unamuachia mtoto wako wa kumzaa mchana kutwa.
Mkuu hii sekta nahisi bado haijarasimishwa hasa wa hawa mondakta wa daladala.
Siku zote mwenye gari anamuachia gari dereva so dereva ndiye anayetafuta kondakta ili apate hela nzuri na aweze kumdhibiti huyo msaidizi wake ndio anatafuta hao walikata tamaa ya maisha.
Ila ingekuwa ni ajira rasmi kama vile kuendesha gari za BRT sidhani kama wangekuwa wachafu hawa vijana.
Siku hizi mpaka makondakta wa uda nao wameshakuwa wachafu zile sare zao wakati zilipokuwa mpya ziliwapendeza sana ila sasa hivi zimepauka na zina viraka wengine wanazifunga na mipiria au katani kiunoni basi ili mradi shida tupu.
Uchafu nahisi kwenye hili jiji letu ni jadi wala sio kingine.
Mkuu driver wengi wa hizi daladala wanajua kwa ujazo huu sikosi hesabu fulani so kondakta hata akisema abane hela haizidi buku mbili.kazi sana yani mtu anakudai hela unatamani usimlipe vile alivyo mchafuuu na hasa ukiwa mmebanana mmesimamam anajipenyeza katikati kudai hela daah hata hajali....lakini pia umesema mkuu dereva apate hela nzuri anamtafuta teja..kwani kati yadereva na konda nani anakusanya hela, si konda dereva anajuaje trip hii imeingia kiasi kadhaa?