Gari la jeshi la sababisha ajali mbaya dar

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,141
Reaction score
951
[h=3]GARI LA JESHI LA SABABISHA AJALI MBAYA DAR KARIBU NA IDARA YA HABARI MAELEZO, MWANAJESHI MMOJA AJERUHIWA VIBAYA, KISA KUJAZA VIFAA KUPITA KIASI[/h]

GARI LA JESHI LA SABABISHA AJALI MBAYA DAR KARIBU NA IDARA YA HABARI MAELEZO, MWANAJESHI MMOJA AJERUHIWA VIBAYA, KISA KUJAZA VIFAA KUPITA KIASI JAMAA ALIKUWA AMENING'INIA JUU YA GARI AINA YA IVECO LILILOKUWA LIMEBEBA MIZIGO ILIYOJAA KUPITILIZA. ASKARI HUYO ALIJIGONGA JUU YA MTI NA KUDONDOKA CHINI NA KUPASUKA KICHWA. LIJA YA KUJAZA GARI HILO LILIKUWA LIMEVUNJA SHERIA KUPITA BARABARA ILIYOSTAHILI KUPITA MAENEO YA IDARA YA HABARI MAELEZO. KWA WANAOJUA BARABARA HIYO HUWA HAIRUHUSIWI KUPANDA KUTOKEA MAENEO YA CHUO CHA IFM, ASKARI HAO WALIPITA BARABARA HIYO WAKITOKEA CHINI CHUO CHA IFM NA KUPANDISHA MOJA KWA MOJA MNARA WA ASKARI. HALI HIYO ILISABABISHA MADEREVA TAIX KUMKATAA MGONJWA HUYO MPAKA ALIPOPAKIWA KWENYE BAJAJI ILI KUPELEKWA HOSPITALI.

HEKA HEKA ZIKIENDELEA.

MTI ULIOSABABISHA AJALI HIYO. PICHA NA TULLO CHAMBO, DAR ES SALAAM.
​

HABARI NA MATUKIO: GARI LA JESHI LA SABABISHA AJALI MBAYA DAR KARIBU NA IDARA YA HABARI MAELEZO, MWANAJESHI MMOJA AJERUHIWA VIBAYA, KISA KUJAZA VIFAA KUPITA KIASI

MY TAKE:

Tabia ya wanaJeshi wetu kujina wapo juu ya Sheria matokeo yake ni haya"
 
duh!! inasikitisha kwakweli, nampa pole aliyeumia lakini pia kumwomba Mungu amponye haraka kwakweli.
 
Kwanza, nampa pole nyingi mpiganaji aliyeumia. Mola amjalie apone haraka. Pili, nimepata kusema kwamba duniani kote, vyombo kama Jeshi ndivyo vinavyopaswa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia nidhamu. Bahati mbaya kwa nchi kama Tanzania, kuwa askari JWTZ, Polisi, Magereza, Usalama wa Taifa hata Mgambo, ni sifa ya kuvunja sheria. Nimepata kumsema Luteni Jenerali mmoja ambaye kazi yake ni kuendesha gari kwenye service road jijini dar es salaam. Katika ajali hii tunayoijadili, kulikuwa na sababu gani dereva mwanajeshi kuendesha gari kwa kupanda na njia ambayo kisheria imezuiwa? Kama kulikuwa na ulazima, leo Januari 12 ni Sukukuu ya Mapinduzi zanzibar. Jiji la Dar es Salaam halikuwa na magari mengi katikati ya jiji. Kama hivyo ndivyo, kulikuwa na sababu gani kuvunja sheria? Dereva alikuwa anakwepa ili awahi nini? Hapa ndipo ninapotarajia kuona Jeshi likimchukulia hatua dereva wake. Aeleze, kulikuwa na sababu gani kupita njia isiyoruhusiwa wakati barabara ikiwa wazi? Aeleze, kama dereva aliyefuzu, anawezaje kukubali abiria wakajaa hadi pomoni na kukaa juu ya mabomba ya gari? Haya maswali lazima msuhusika ayajibu na ikibidi awajibishwe.

Mwisho, nitoe rai kwa askari wote. Kuwa askari haina maana uwe juu ya sheria. Nchi hii kila kwenye ka-cheo akiamua kuonyesha makeke, nani atasalimika? JWTZ lazima wawe mfano wa kuigwa. Wasishiriki uhuni wa aina yoyote.

Manyerere Jackton
Dar es Salaam
 
ni jana niliongozana na rolly la jeshi likiwa harina indiketa, taa taa ya breki wala taa ya pakingi yaani lipo kama limepigwa bomu huki likiwa limepakia mizigo mpaka juu likitembea mwendo wa konokono na kuleta msongamano. hawa jamaa sio kabisa
 
jeshin hakuna starehe usiogope hayo nikawaida njoo ngerengere mpendwa
 
Kwanza, nampa pole nyingi mpiganaji aliyeumia. Mola amjalie apone haraka. Pili, nimepata kusema kwamba duniani kote, vyombo kama Jeshi ndivyo vinavyopaswa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia nidhamu. Bahati mbaya kwa nchi kama Tanzania, kuwa askari JWTZ, Polisi, Magereza, Usalama wa Taifa hata Mgambo, ni sifa ya kuvunja sheria. Nimepata kumsema Luteni Jenerali mmoja ambaye kazi yake ni kuendesha gari kwenye service road jijini dar es salaam. Katika ajali hii tunayoijadili, kulikuwa na sababu gani dereva mwanajeshi kuendesha gari kwa kupanda na njia ambayo kisheria imezuiwa? Kama kulikuwa na ulazima, leo Januari 12 ni Sukukuu ya Mapinduzi zanzibar. Jiji la Dar es Salaam halikuwa na magari mengi katikati ya jiji. Kama hivyo ndivyo, kulikuwa na sababu gani kuvunja sheria? Dereva alikuwa anakwepa ili awahi nini? Hapa ndipo ninapotarajia kuona Jeshi likimchukulia hatua dereva wake. Aeleze, kulikuwa na sababu gani kupita njia isiyoruhusiwa wakati barabara ikiwa wazi? Aeleze, kama dereva aliyefuzu, anawezaje kukubali abiria wakajaa hadi pomoni na kukaa juu ya mabomba ya gari? Haya maswali lazima msuhusika ayajibu na ikibidi awajibishwe.

Mwisho, nitoe rai kwa askari wote. Kuwa askari haina maana uwe juu ya sheria. Nchi hii kila kwenye ka-cheo akiamua kuonyesha makeke, nani atasalimika? JWTZ lazima wawe mfano wa kuigwa. Wasishiriki uhuni wa aina yoyote.

Manyerere Jackton
Dar es Salaam

Ndio Jeshi letu hilo. Kule polisi wanajichukulia sheria mikononi wanaua kabisa raia
 
Ushasema jeshi wako wengi

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Tatizo kubwa la askari wetu wanaona kuwa wao wako juu ya sheria. Pole sana majeruhi, twaomba apone haraka.
 
Ni fundisho tosha kwa wanajeshi mambulula. hawa jamaa uwa wanavunja sheria sana za barabarani
 
Dah, jamaa amepiga mti hadi umechubuka? Pole yake.
Ni kweli wamezidi hao wanajeshi. Na ukiwapigia horn wanajidai kupandisha. Yule askari wa ajali ya mikocheni sijui kama alishatoka icu maskini, manake alikaa moi for more than a month akiwa hana fahamu.
 
Tatizo kubwa la askari wetu wanaona kuwa wao wako juu ya sheria. Pole sana majeruhi, twaomba apone haraka.

Ni uelewa mdogo tu kwa baadhi ya hawa askari, askari wote wanafundishwa kuzingatia nidhamu na kuwa mfano bora kwa jamii lakini wakiingia mahali penye raia wanajisahau na kufanya mambo ya kihuni.
 
Ewe dereva taxi wa hapo habari maelezo,hama kituo hicho kwa muda!wanawarudia hao na unajua wakirudi wanarudi vipi....
 
ngoshwe; Ama kweli hili walilofanya hawa wanajeshi Mi sijaiunga mkono hata kidogo........na faida yake ndiyo kama hivyo!!!
 
Kwanza, nampa pole nyingi mpiganaji aliyeumia. Mola amjalie apone haraka. Pili, nimepata kusema kwamba duniani kote, vyombo kama Jeshi ndivyo vinavyopaswa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia nidhamu. Bahati mbaya kwa nchi kama Tanzania, kuwa askari JWTZ, Polisi, Magereza, Usalama wa Taifa hata Mgambo, ni sifa ya kuvunja sheria. Nimepata kumsema Luteni Jenerali mmoja ambaye kazi yake ni kuendesha gari kwenye service road jijini dar es salaam. Katika ajali hii tunayoijadili, kulikuwa na sababu gani dereva mwanajeshi kuendesha gari kwa kupanda na njia ambayo kisheria imezuiwa? Kama kulikuwa na ulazima, leo Januari 12 ni Sukukuu ya Mapinduzi zanzibar. Jiji la Dar es Salaam halikuwa na magari mengi katikati ya jiji. Kama hivyo ndivyo, kulikuwa na sababu gani kuvunja sheria? Dereva alikuwa anakwepa ili awahi nini? Hapa ndipo ninapotarajia kuona Jeshi likimchukulia hatua dereva wake. Aeleze, kulikuwa na sababu gani kupita njia isiyoruhusiwa wakati barabara ikiwa wazi? Aeleze, kama dereva aliyefuzu, anawezaje kukubali abiria wakajaa hadi pomoni na kukaa juu ya mabomba ya gari? Haya maswali lazima msuhusika ayajibu na ikibidi awajibishwe.

Mwisho, nitoe rai kwa askari wote. Kuwa askari haina maana uwe juu ya sheria. Nchi hii kila kwenye ka-cheo akiamua kuonyesha makeke, nani atasalimika? JWTZ lazima wawe mfano wa kuigwa. Wasishiriki uhuni wa aina yoyote.

Manyerere Jackton
Dar es Salaam

Pamoja na maoni yako ya uchungu mwingi kuna mambo hujayaweka fresh wewe anamsema dereva mwenzako ukiwa kama nani? kazi yako ni usukani na lami mbele yako mambo ya kupandisha watu hasira yanachangia ajali. Pia hakuna Luteni Jenerali anayeruhusiwa kuendesha gari na jeshi letu lina Luteni Jenerali mmoja tu kwa wakati mmoja ambaye ndiye Mnadhimu Mkuu wa Jeshi sasa huyo uliyemuonya huko mtaani yawezekana alikuwa jambazi wa kawaida aliyevalia mavazi ya jeshi na kama gari ilikuwa ya jeshi ilifojiwa
 
Back
Top Bottom