Gari la familia

motonkafu

JF-Expert Member
Dec 2, 2015
1,019
703
Kuna sherehe nyumbani kwa kaka na nimeitwa japokuwa sina tabia ya kufurahi hovyo hovyo nimeamua kwenda ili nimuunge mkono ndugu yangu na niweze kujua mwenzangu amefurahia nini.

Nimefika kwa braza naona shemeji amefurahi sana, watoto wanarukaruka, sherehe yaanza. Lakini kabla sijauliza hawa watu wamefurahia nini, braza anakuja ananinipa tano na kujigamba 'mdogo wangu nimenunua gari ile paleee'. Ninampa hongera na ninafurahi kwani kaka yangu amepiga hatua ya maendeleo, ninaenda kuiona gari.

Nafunua turubai nashikwa na tahamaki 'kaka amenunua gari ya zamani, na kwa kuiangalia itakuwa imetumika sana'. Namgeukia kaka yangu na kumuuliza umenunua bei gani hii gari? Ananiambia ameunganishwa na dalali fulani wa familia na ameambiwa ni gari zuri hivyo amelipa mamilioni bila kuulizia ubora na mwaka liliotengezwa gari hilo. Ninamwambia ukweli kwamba kaka gari hili ni la zamani sana, angalia 'show' yake, angalia mlango wake huu kama dirisha la kibanda cha kufugia sungura, haya ingia ndani angalia viti vyake kama daladala za mbagala. Namuuliza braza limetumia mda gani kutoka Dar lilikonunuliwa mpaka mkoani? Ananiambia siku mbili, tobaaaaa!

Kwa upendo namwambia kaka ungeniuliza, ningekupeleka 'showroom ' za maana ungenunua magari ya kisasa ambayo yanatembea kutoka 'Darisalamu' mpaka Mbeya masaa nane tu. Namwambia siku hizi kuna mabasi ya wafaransa yamejaa raha tupu, hata mjamzito wa miezi tisa atasafiri mpaka mkoani asisikie uchungu lakini hili alilonunua hata mgonjwa wa presha atazimia kwa mtikisiko wake pindi linapoingia stendi.

Braza haamini ninachomwambia na ninamtolea simu hizi za kisasa ambazo hata ukiuliza miti ya maembe iko wapi zitakwambia ilipo, ninachukua jina na namba ya gari hilo natafuta, maskiniiiii inaonyesha gari lilitengenezwa miaka ya sabini na limetumika miaka yote 40 mpaka sasa na wakati wanaliuza walipaka rangi mpya. Braza anaanza kuamini japo mbishi huyu na atanielewa tu.

Kaka ananistua kwamba ameagiza gari lingine la aina hiyo hiyo litakuja mwezi ujao, naanza kuogopa kwamba labda kaka anaichezea mchezo familia ionekane kanunua magari kumbe hela kapeleka nyumba ndogo, naghafirika sasa na kumuonya kaka mbona unakurupuka sana, braza ananituliza na kuniambia yuko tayari kuahirisha manunuzi ya gari la pili kwa sababu anaibiwa hela tu. Ninamwambia amwambie yule wakala mwongo arudishe pesa ili nimpeleke kwenye showroom za maana tukanunue magari makali ya kisasa tuachane na haya ya zamani yaliyotumika yasije yakatumaliza kwa ajali.
 
na madereva walihakikisha gari imemfikia hadi nyumbani japo kaka yako hakuwepo kukabidhiwa funguo. najiuliza kwanini madereva wasindikize gari ilihali kaka aliwatuma madereva kabla ya safari
 
Una kipaji, simulizi yako nzuri.
 
Na wale mafundi 'matesta' walipewa na posho na nauli ya kwenda kuhakikisha gari linafika salama nyumbani..!
 
Hii 'fasihi' yako ya kipuuzi wapelekee wenzio wa Tandale kwenye vyoo vilivyopandiana ndo inawafaa.

-Kaveli-
 
Mkuu kuna mtu anaitwa Lizaboni akikusikia haki ya nani hapatakalika hapa!! Ngoja mimi nikae pembeni nimsubiri Lizaboni atakavyokushukia!
 
Back
Top Bottom