Gari kuwa na miss asubuhi au ukipaki muda mrefu

Asanteni sana woooote kwa ushauri wenu. Hakika mmenipa mwanga mzuri. Kesho ntapita garage halafu ntaleta mrejesho.
 
Heshima zenu wakuu.

Kuna gari asubuhi inawaka ila inakuwa kama ina miss hivi na rpm inakuwa chini sanaaaa hadi wakati mwingine inazima.

Ukiiacha kwa kama dakika 2 hivi miss inakata na rpm inatulia vizuri kabisa.

Hii hutokea asubuhi au kama umepaki gari muda mrefu - masaa kuanzia 3 na kuendelea huko.

Gari ni Rav 4 old model (3s engine).

Naombeni msaada wakuu ili nikienda garage angalau niwe na mwanga kidogo.

Naomba kuwasilisha
Mara nyinyi huchangiwa na mafuta kuja kidogo kwenye engine muda ambao yalitakuwa kuja mengi.

Gari hutumia mafuta mengi wakati wa kuwaka, yakija machache lazima imisi.

Kwa gari kama hiyo sababu kuu ni kuharibika kwa sensor za joto. (Yaani joto la hewa na joto la coolant. Zote mbili au moja wapo).

Ukishindwa kutatua nicheck. 0621 221 606
 
Yaani kuwaka haina shida kabisa. Tatizo ikishawaka ndo shida zinaanza. Baada ya dakika 2 hadi 3 inatulia fresh kabisa kama sio ile.

Yangu ina shida hii hii inayomsumbua huyu bwana. Na tatizo linaambatana na gari kula mafuta kuliko kawauda yake...

Nimeshamwona fundi, amefanya diagnosis na kuniambia nibadilishe fuel injection nozzles, fuel injection pump, petrol cleaner, ignition plugs na plug wires zake...

Kwa kifupi, matatizo yoyote ya gari yanasababishwa na kutofanya service ya mara kwa mara kwa wakati unaotakiwa...

Na watu wengi wanaomiliki magari, wale wanaojua kuwasha na kuondoka tu hawaelewi maana ya "CAR SERVICE"...

Wanadhani kufanyia gari service ni tendo la kwenda kubadilisha oil na oil cleaner, basi unakuwa umemaliza...

Wengi wanaoamini hivi, ndiyo ambao hawadumu na magari kwa kuharibika na kisha huamua kuyauza...

Kuna service ya kawaida ambayo in lazima ifanyike kabla ya kuanza au baada ya kutoka safari ndefu..

Lakini BIG CAR SERVICE ambayo unaweza kuifanya mara moja au mbili kwa mwaka kutegemea na matumizi yako ya gari. Service hii huhusisha fundi (car expert) kucheki kila engo ya gari yako na ikibidi kubadilisha mambo mengi kwa kutoa vikuukuu na ku - replace kwa vipya....

You have to be well off and prepared financially...
 
Heshima zenu wakuu.

Kuna gari asubuhi inawaka ila inakuwa kama ina miss hivi na rpm inakuwa chini sana hadi wakati mwingine inazima.

Ukiiacha kwa kama dakika 2 hivi miss inakata na rpm inatulia vizuri kabisa.

Hii hutokea asubuhi au kama umepaki gari muda mrefu - masaa kuanzia 3 na kuendelea huko.

Gari ni Rav 4 old model (3s engine).

Naombeni msaada wakuu ili nikienda garage angalau niwe na mwanga kidogo.

Naomba kuwasilisha

Kabla ua kwenda mbali jaribu kuchek hivi vitu viwili
1) ignition plug
2) Air intake system huenda inavuja sehemu au air mass flow sensor in shida
NB: Kwa wenye vyombo vya moto mjitahidi kuwa mnasoma soma hata You tube kuna vitu unaweza jifunza juu ya gari lako
 
Kabla ya kugundua hii niliambiwa nibaidilishe plug, wire na coil nikafanya hivyo lakini havikufua dafu. Nikaamua nifanye uchunguzi wangu binafsi nikagundua shida ilipo.
Kwa plug si rahisi. Kuna hiyo sensor, Intake air temperature sensor au EGR. Mara nyingi tatizo ndio linakuwa hapo.
 
Sijawahi experience hilo tatizo kwenye hizi Bugggati.




Alisikika Kiduku lilo.
 
Heshima zenu wakuu.

Kuna gari asubuhi inawaka ila inakuwa kama ina miss hivi na rpm inakuwa chini sana hadi wakati mwingine inazima.

Ukiiacha kwa kama dakika 2 hivi miss inakata na rpm inatulia vizuri kabisa.

Hii hutokea asubuhi au kama umepaki gari muda mrefu - masaa kuanzia 3 na kuendelea huko.

Gari ni Rav 4 old model (3s engine).

Naombeni msaada wakuu ili nikienda garage angalau niwe na mwanga kidogo.

Naomba kuwasilisha
Tuanzie hapa.
Je taa ya check engine inawaka!?

Kuwaka gari Ni combustion process ambayo inategemea
Mafuta
Hewa
Na Chanzo Cha mafuta katika muda sahihi,joto, pressure na kiasi sahihi
Hivyo chochote kinachoweza ingilia mkutano huu lazima gari italeta misfire etc

Kama check engine iko on ifanyiwe diagnosis itasema tatiz maana Kuna sensor kadhaa zinaleta iyo
Na hii mifumo yote Ya hewa,mafuta na uchomaji ifuatiliwe.
 
Hapo shida n idle speed sensor valve alaf osha hpo kwenye throttle gari itakuwa piru jomba,Amna kitu yakubadilisha hpo.carborn imejaa hpo kwenye throttle

Sent from my CPH2083 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom