Gari ipi used itanifaa kwa kipato cha 700k kwa mwezi?

Hebu ngoja nione kama na mimi bado nakumbuka sababu za kutokua na gari mpaka leo.

1. Insurance 120000 kwa mwaka sawa na 10000 kwa mwezi.

2. 20km/siku = 440km/mwezi= 30l = 60000

3. 10000 kuhonga kwa makosa mbalimbali.

4. Km huna parking ofisini 2500×22= 55000.

5. Km huna vijana nyumbani kuosha mara moja mwa wiki 3000, 15000 kwa mwezi.

6. Service kila baada ya miezi 6 = 85000, kwa mwezi = 14000.

7. Km huna parking home?

Jumla: 165000 - 265000 kwa magari tajwa hapo juu ya chini ya 1.5cc

Ambayo ni sawa na 23% -37% ya hiyo 700k. Washauri wanasema gari linatakiwa kula chini ya 10% ya kipato chako, hiyo sio sheria. Maana kipato kinaweza kupanda muda wowote
 
Suzuki Jimny, gharama kuzinunua lakini kuzitunza rahisi kwa maana ya uimara na matumizi kidogo ya mafuta cc700.
 
Sidhani kama umemuelewa mtoa mada, haitaji gari ya sh 700,000 bali hicho ni kipato chake kwa mwezi. Hivyo anahitaji kujua gari ipi anaweza akaafford kwa kipato hicho.
Ila bado hayuko direct...kipato cha laki 7 haitoshi kushauriwa....aseme akishatoa matumizi yake mengine anabakiwa na kiasi gani na watu ndio wamshauri based on anachobaki nacho kwa ajili ya gari.

Mia 7 hiyo hajatoa chakula, malazi km analipa kodi, maji, umeme n.k na baada ya kutoa kwa mwezi husika anabaki na kiasi gani ambacho anadedicate ktk gari yake
 
Back
Top Bottom