Gari inayotumia petrol kutoa moshi tatizo ni nini?

Kig

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
1,076
457
Hongeren kwa majukumu wadau wa JF garage
gari yangu ni Noa Old model, ya mwaka 1998. Siku za hivi karibuni imeanza kutoa moshi mara ninapoiwasha hasa asubuhi, huwa inatoa moshi kwa dakika kadhaa halafu inarudi kwenye hali yake ya kawaida. Na kwa kawaida magari yanayotumia petrol huwa hayaoti moshi. Naomba mnisaidie kujua itakuwa na tatizo gani?
 
Sina ujuzi sana ila gari inapowaka wakati wa asubuhi RPM huwa inakuwa juu kidogo ili kuwarm up injini so usikute rpm ikiwa juu inatoa moshi na sio kwamba inatoa moshi asubuhi tu. Ila sababu ya kutoa moshi sijui mkuu
 
Moshi unayoizungumzia ww ni moshi hii ya Kilimanjaro au moshi gani? Embu funguka tujue tunaanzia wapi kukushauri. Eid mubarak
 
Mkuu. Nina the same case, sasa mwezi wa 6 huu na fundi aliniambia hakuna tatizo lolote. Sasa sijajua alikua sahihi au vipi. Ila performance iko poa. Mimi Corolla VVTi NZ_FE engine
 
Jaribu kubadili plug. Huenda hazichomi vizuri. Otherwise ingekuwa inatoa moshi mwingi full time, tungesema inapandisha oil na hapo piston rings zinakuwa zimeisha.
 
Mkuu. Nina the same case, sasa mwezi wa 6 huu na fundi aliniambia hakuna tatizo lolote. Sasa sijajua alikua sahihi au vipi. Ila performance iko poa. Mimi Corolla VVTi NZ_FE engine
Mosh mweusi hauna shida sana ila moshi mweupe na wabluu ndio huwa na tatizo kwa gar za petrol
 
Mimi pia niliambiwa na fundi wangu kuwa ni kitu cha kawaida. Lakini yangu haitoi moshi mwingi sana. Huwa unatoka kidogo ile asubuhi ninapoiwasha
 
Hongeren kwa majukumu wadau wa JF garage
gari yangu ni Noa Old model, ya mwaka 1998. Siku za hivi karibuni imeanza kutoa moshi mara ninapoiwasha hasa asubuhi, huwa inatoa moshi kwa dakika kadhaa halafu inarudi kwenye hali yake ya kawaida. Na kwa kawaida magari yanayotumia petrol huwa hayaoti moshi. Naomba mnisaidie kujua itakuwa na tatizo gani?
Ring zimekwisha engine oil inangia kwenye petrol hata ukipima engine oil inapungua sana
 
mkuu magari mengi sana sijuhizi yanatumia sensor kucontrol emission.
moja ya sensor ni oxygen sensor na sensor nyingine ni knock sensor.
jaribu kufanya uchunguzi kama hizo sensor ni nzima.nchi za watu wanafanya emission test na mara nyingi hizo sensor ndio zinakuwa na shida na ndio zinacontrol air fuel combation ration.si mtaalamu wa magari lakini nimejifunza kupitia uzoefu wa matumizi ya gari
 
Back
Top Bottom