Gamondi ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi Singida Black Stars

Gamondi ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi Singida Black Stars

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Kutoka kuwa kocha mkuu wa Singida Black Stars hadi kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi ambacho ndio cheo kipya cha Miguel Gamondi ambaye kwa sasa ni kocha wa muda wa Taifa Stars.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Wakurugenzi wa Singida BS, leo Jumatatu, Januari 5, 2025 imetangaza mabadiliko katika klabu yao ambapo kocha mkuu wa timu hiyo atakuwa David Ouma.

Kocha Ouma atasaidiwa na makocha wasaidizi Mousa Nd’aw na Muhibu Kanu.

Gamondi amebadilishiwa majukumu na kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu, nafasi itakayompa dhamana ya kusimamia mipango ya kiufundi na maendeleo ya jumla ya timu.

Hata hivyo, Singida BS imesema haina pingamizi lolote kwa mamlaka endapo Gamondi atateuliwa kuwa kocha wa kudumu wa timu ya Tanzania, Taifa Stars.
611628343_18333562036240773_5359612888268037380_n.jpg
 
Kwanza naomba nipewe darasa kidogo majukumu ya hiyo kazi ni yapi?
Kwanza Mipaka yake inaishia wapi?
Anawajibika kwa Head couch au CEO.

Kwa Tanzania hii ambayo mdhamini wa club naye anasajiri, kamati ya usajiri inasajiri, kocha naye anasajiri
Wataishije hawa watu.mbona naona vumbi..
Record inaonyesha hii post ni hewa kwa Tanzania..

Iliwahi kutokea Hans Pujims, aliondolewa ukocha, nafasi yake ikachukuliwa na George Lwandamina; hiyo ni 2018, halafu Pujims akawa Mkurugenzi wa technical bench...safe ikawa hivi;
Peter msola-mwenyekiti
Pujims-Mkurugenzi benchi la ufundi
Lwandamina- kocha mkuu
Juma mwambusi-Kocha msaidizi
Boniface Mkwasa-Meneja

Ukiangalia hiyo orodha, wote hao ni makocha...
Hawakudumu hata siku 10
Walifukuzana.
 
Back
Top Bottom