Games kwa ajili ya watoto

Kichwa Ndio Mtu

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2014
Posts
3,079
Reaction score
1,719
Wakuu salam.

Wakuu mimi sio mpenzi wa games kwa hiyo sijui zinapatikana wapi sasa kwa bahati nzuri au mbaya kwangu kuna watoto wa ndugu yangu wamenitembelea hapa likizo hii na wanataka games.

Naomba msaada wenu nazipataje za bure na hata za kununua ili niwawekewe hawa jamaa wafurahie likizo yao yote hapa kwangu, ni web zipi online zina magames mazuri nipakue,wanataka ya kuendesha magari, pikipiko,vita,chalenji nk.

Natanguliza shukrani.
 
Kabla hatujaendelea wana miaka mingapi?

Kama ni wadogo sana mfano chini ya miaka 13 basi hao usiwaekee game za kawaida za mitaani kama vita, sjui gta zitawaharibu tu. Zipo games nzuri za flash za kimasomo zaidi kama kuwafundisha spelling, kuhesabu, kuandika upesi upesi nk nyingi zao zinakuwa ni flash games na ni free. Sipo na pc hapa ningekutestia nikakupa link

Kama wanajielewa ni watoto ambao atleast wamemaliza shule ya msingi wanaweza cheza hizi games za kawaida na utazipata hapa

Ocean of Games

Ila ni vyema ungetaja specs za pc hio utakayoeka games ili upewe recomendation nzuri ya games kutokana na computer yako.

Nenda mycomputer halafu right click then properties kujua processor, ram na vitu vyengine
 

Mkubwa ana miaka 13 yuko form two,mdogo wakeni 11yo na mwingine 8yo.
Nataka niweke kwenye pc ambayo huwa haitumiki ya 32 bit, processor wameandika duo 2.4ghz na ram ya 2gb.
 
Mkubwa ana miaka 13 yuko form two,mdogo wakeni 11yo na mwingine 8yo.
Nataka niweke kwenye pc ambayo huwa haitumiki ya 32 bit, processor wameandika duo 2.4ghz na ram ya 2gb.

Hao usiwaekee games za kawaida za wakubwa japo watakusumbua hakuna umeme hapa ukirudi ntakutaftia list nzuri ya games za age yao.
 
Hao usiwaekee games za kawaida za wakubwa japo watakusumbua hakuna umeme hapa ukirudi ntakutaftia list nzuri ya games za age yao.

Shukrani mkubwa. Uko eneo gani niwambie tanesco wakurudishie umeme mkuu(utani).
 
Shukrani sana chief, kwa hiyo umesema gta haziwafai watoto hawa? CHIEF MKWAWA.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…